| ALIYEKUWA Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya akiingia mahakamani kusikiliza hukumu kwenye kesi inayomkabili ya unyag'anyi wa kutumia silaha |
JAMHURI yaomba mahakama impe adhabu
kali,aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili kwani
kwa matendo ya unyang’anyi wa kutumia nguvu na kutumia silaha aliyoyafanya
akiwa kazini ameinajisi taasisi ya Rais iliyomteua.
Ombi hilo limetolewa na Wakili wa
serikali, Felix Kwetukia mbele ya Hakimu
Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo kwenye Makahama ya Hakimu Mkazi Arusha baada ya
mahakama hiyo kuwatia hatiani Lengai Ole Sabaya, na wenzake Silvester Nyegu na
Daniel Bura kwa makosa mawili ya unyang’anyi wa kutumia nguvu na kosa moja la
unyang’anyi wa kutumia silaha.
Wakili wa serikali, Felix Kwetukia, mheshimiwa
hakimu hatuna kumbukumbu ya makosa ya jinai waliyowahi kutiwa hatiani ila ni rai
yetu kwamba kwa kosa la pili la unyang’anyi wa kutumia silaha wahukumiwe kama
sheria ya adhabu kifungu namba 287 A kinavyoelekeza.
“Kinasema ni adhabu kwa kufungwa
jela miaka isiyopungua 30 na ni rai yetu kwamba kwa kuwa kifungu hiki kimeeleza
kuwa wanaweza kupewa pamoja na adhabu ya kuchapwa viboko au wasipwe sisi upande
wetu tunaomba wapate adhabu ya viboko.
Kwa kosa la kwanza na la tatu la
unyanganyi wa makundi ambao adhabu yao ni kifungo kisochopungua miaka 30 na
adhabu ya viboko au bila viboko ni rai yetu wachapwe hata kwa kosa la kwanza na
la tatu ni rai yetu adhabu ya viboko iambatane nao,”
Mheshimiwa tumeomba adhabu hiyo kali kwa sababu mhukumiwa
wa kwanza kwa kuwa mteule wa Rais kwa kipindi hicho na kujihusisha na vitendo vya
unyang’anyi wa kutumia silaha na kujiingiza katika unyang’anyi wa nguvu
Alifanya vitendo ambavyo si vizuri
kwa mamlaka yake ya uteuzi na jamii ya Watanzania kwa kadiri ya makuzi na haiba
ya vijana waliolelewa katika malezi mazuri.
Hivyo ni rai yetu adhabu kali
itolewe ili iwe fundisho kwake pamoja na grupu lake
Kwa kuwa alikuwa mteule wa Rais
alikuwa anaidhalilisha mamlaka yake ya uteuzi kwa kutenda mambo kinyume na hati
yake ya uteuzi ilivyokuwa inamwelekeza.
Umri wa washitakiwa wote ambao
wametiwa hatiani ni umri wa vijana ambao wana nguvu ya kufanya kazi walipaswa
kujipatia kipato kwa njia halali na si kujiingiza katika matendo ya uhalifu
hususani unyanganyi wa kutumia silaha kwa msingi huo mheshimiwa hakimu ni rai
yetu ingawa ni mara yao ya kwanza kutiwa hatiani basi kama vifungu vya 287
A vya adhabu na 217 vinavyoelekeza basi adhabu kali dhidi ya watiwa hatiani
wote iweze kutolewa.
MAOMBI YA UNGAMO
Wakili, Moses Mahuna kwa niaba ya
Lengai Ole Sabaya aliiomba mahahakama impunguzie mteja wake adhabu kwani
hiyo ni mara yake ya kwanza kutiwa
hatiani.
“Tunaleta maombolezo kwa niaba ya
mshitakiwa
wa kwanza, baada ya mahakama kumtia
hatiani kwenye makosa hayo mawili ni kweli sheria inatoa adhabu ya kifungo kisichopungua
miaka 30 ambacho kinaweza kuambatana au kisiambatane na adhabu ya viboko,”
ameeleza wakili Mahuna na kuongeza.
…Tunaomba mahakama immtazame
mtuhumiwa wa kwanza kwa jicho la huruma kwa kuwa ni mtenda kosa kwa mara ya
kwanza na hakuna rekodi za nyuma zozote za kutiwa hatiani
Hata hivyo mheshimiwa, mtuhumiwa
huyu wa kwanza amekuwa mtumishi wa umma kwa kipindi kirefu licha haya yaliyopo
hapa mahakamani ni mamnbo mengi amelitendea Taifa katika utumishi wake.
Hivyo ni rai yetu kwamba mahakama
inapotoa adhabu imtazame kwa jicho la huruma hata hivyo mshitakiwa amekuwa
akitoa ushirikiano wa kutosha tokea alipokamatwa.
Alishirikiana na vyombo vya dola
vyotetokea alipokamatwa mpaka akaletwa hapa mahakamani.
Hata hivyo kama ilivyotanguliwa
kusemwa na wakili msomi Felix Kwetukia ni dhahiri kwamba ni kweli kuwa
mtuhumiwa ana umri wa miaka 34 ambaye bado ni nguvu kazi ya Taifa.
Ni rai yetu mahakama izingatie umri
wake huo kwa kuwa adhabu hizi za makosa yake yote haya ni miaka 30 kwa 30 ni
ombi mahakama inapoenda kutoa adhabu izingatie mchango wake kwa Taifa hasa na
umri wake na kumpatia adhabu ambayo itamwezesha kutumikia hiyo adhabu ndani ya
kipindi ambacho kitatosha kumrekebisha na hatimaye kumruhusu kurudi kuendelea
kutoa mchango wake katka Taifa hili.
Na ni ombi letu ikikupendeza adhabu
hizo ziende kwa pamoja, hiyo miaka 30, 30 iende kwa pamoja
manake sipoenda kwa pamoja ni miaka
90 hivyo ni ombi letu mheshimiwa hukumu hiyo isitafsiriwe kama kifungo cha
maisha kwa kifungo cha miaka 90 kumfanya atoke akiwa na miaka 120 (mahakama kicheko).
Jambo linguine ana familia pia
inamtegemea, ana mke na watoto, na ana wazazi pia wanamtegemea kwa hiyo
tunaiomba mahakama izingatie hayo yote.
Wakili, Silvester Kahunduka kwa
niaba ya mshitakiwa wa pili, Silvester Nyegu alieeleza mahakama kuwa ni kweli
kuwa mshitakuwa wa pili ametiwa hatiani
na mahakama yako kwa makosa matatu ambayo yote adhabu yake ni miaka 30.
“ Mheshimwa tunakuja mbele ya
mahakama yako kwa maombolezo kuwa bado ni kijana mdogo ana miaka 26 tu, hii ni nguvu ya uchumi katika Taifa hili lakini vilevile ana familia inayomtegemea kwa
maana ya wazazi wake na ndugu zake kwa maana hiyo tunaiomba mahakama katika kutoa
adhabu ione hilo,” ameomba wakili Kahunduka na kuongeza.
…Jamhuri imeomba wapewe dhabu na
viboko lakini adhabu ya viboko ni maamuzi ya mahakama na adhabu za viboko mara
nyingi zinalalamikiwa mara nyingi kama adhabu ambazo zinautweza utu wa watu…
..Tunaiomba mahakama hii kwa kutumia
mamlaka iliyo nayo katkka kuamua izingatie kwamba hiyo ni adhabu ambayo inakuwa
inalalamikiwa sana na ikiwezekana
mahakama isitoe adhabu hiyo.…
Hakimu akasema kulalamikiwa siandiki kwa sababu adhabu hiyo iko kisheria wakili
akakubalina naye
Wakili, Freedolin Gwemelo kwa niaba
ya mshitakiwa wa tatu, Daniel Bura aliieleza mahakama kuwa hili ni kosa lake la
kwanza hana rekodi yoyote ya kosa la jinai, mshitakiwa bado ni kijana ni nguvu
ya Taifa anayetakiwa kwenye jamii na kutimiza sera ya nchi hii ya ‘kazi
iendelee’.
Hakimu akauliza ni sera au kauli
mbiu wakili Gwemelo akajibu kauli mbiu.
Wakili Gwemelo akaendelea kuomba
kuwa, “mtuhumiwa namba tatu anategemewa na familia yake akiwemo mama yake ambaye
umri umeenda na ni tegemeo kwa wadogo zake kwa hiyo ndiyo jicho la familia yake
kwa sasa…
…Ni rai yetu makosa yanayomkabili
adhabu yake iende kwa pamoja na iwe ndogo ili aweze kuja kuihudumia familia, na
adhabu ya viboko mheshimiwa naomba isiwepo kwa sababu ni adhabu ambayo hailindi
utu na kwa kuwa ipo chini ya uwezo wa mahakama hii basi adhabu hii isiwepo ni hayo
tu mheshimiwa,”.
0 Comments:
Post a Comment