SABAYA AMEIDHALILISHA TAASISI YA URAIS, AFUNGWA MIAKA 90 NA WENZAKE

 

ALIYEKUWA Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wakitoka mahakamani ya hakimu mkazi Arusha baada ya kuhukumiwa 

ALIYEKUWA Mkuu wa wilaya, Lengai Ole Sabaya amepewa adhabu kali ya kifungo cha miaka 90 baada ya yeye na wenzake wawili kupatikana na hatia ya kufanya makosa mawili ya unyang’anyi wa makundi na kosa moja la unyang’anyio wa kutumia silaha.


Aidha adhabu hiyo itaenda pamoja hivyo kila mmoja atatumikia kifungo cha miaka 30 jela.

 

Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, ametoa adhabu hiyo leo Oktoba 15,2021 majira ya saa 11:47 jioni baada ya kuanza kusoma hukumu hiyo kuanzia majira ya saa 5:56 asubuhi.

 

 

“Kama alivyosema wakili wa serikali mwandamizi, Felix Kwetukia kwamba mshitakiwa wa kwanza Lengai Ole Sabaya alikuwa mkuu wa wilaya aliyeteuliwa na Rais kitendo alichofanya kinadhalilisha taasisi ya Rais,” amesema Hakimu huyo na kuongeza.

 

…Na hakuna ubishi kwamba wote ni vijana na wanahitajika kama walivyoeleza mawakili wao na kwa mujibu wa sheria hakuna ubishi kwamba mikono yangu imefungwa naweza kuwafunga miaka 100 lakini kurudi chini siruhusiwi kufunga chini ya 30...

 

…Mbali ya kwamba wakili wa serikali ameomba viboko wachapwe na walistahili wachapwe manake nao walikuwa wanawatoa wenzao wenge…

 

(Mahakama kicheko)

 

…Lakini mawakili wenzetu wameshindwa kuinyambulisha sheria ya zamani ya watoto walikuwa wanapigwa viboko lakini sheria mpya hawapigwi viboko wamepenyea hapo angalau. Basi mikono yangu imefungwa adhabu ya chini

miaka 30 na viboko…

 

…Kosa la kwanza kila mshitakiwa miaka 30 kila mmoja kosa la pili miaka 30 kila mmoja na kosa la tatu miaka 30 kwa kila mmoja, kwa viboko mawakili wameshinda sitatoa viboko na adhabu ziende pamoja.Mna haki ya rufaa iko wazi,”.

 

 

 

 

 

0 Comments:

Post a Comment