Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,(RPC), Justine Masejo
WATU wawili wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao kwa kupigwa na radi wakidaiwa kutumia simu 'kuchat' wakati mvua kubwa ikinyesha.
Tukio hilo limetokea katika kitongoji cha Olodonyokeri kijiji na kata ya Olosokokwani wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha
ambapo watu hao walikuwa wakichunga mifugo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,(RPC), Justine Masejo amesema tukio hilo limetokea Februari 17,2022 saa 9 alasiri na kuwataja waliojeruhiwa na radi hiyo kuwa ni Sasines Onarok Babu (25) mkazi wa Olosokokwani na mwingine ni Kishuyan Terya Kiyomi (28).
Amesema kuwa baada ya tukio hilo majeruhi walikimbizwa katika zahanati ya kijiji cha Ololosokwani na kupatiwa matibabu.
"Uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha tukio hilo ni matumiziya simu wakati mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha na kuambatana na radi ambayo ilipelekea vijana hao kujeruhiwa sehemu mbalimbali ya miili yao na radi hiyo",amesema Kamanda Masejo.
Ametoa wito kwa wananchi kuwa makini na kuchukua tahadhari hasa kipindi cha mvua kubwa ambazo huambatana na radi kali huku akiwataka kuacha mara moja matumizi ya vifaa vya umeme ikiwemo simu wakati wa mvua kwani kwa kufanya hivyo kutawaepusha na madhara makubwa yanayoweza kutokea.
0 Comments:
Post a Comment