RAIS SAMIA KUZINDUA MIRADI MITATU ARUSHA

 

Rais, Samia Suluhu Hasani anatarajiwa kuzindua hospitali ya wilaya ya Arusha, pamoja na mradi mkubwa wa maji na kiwanda cha nyama Cha Elia Food Overseas LTD  wilayani Longido.

Aidha anatarajiwa kufanya mikutano ya hadhara jijini Arusha na wilayani Longido kwa nyakati na siku tofauti.


Mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongela ameyaswma hayo leo, Oktoba 14,2021 wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya ziara ya Rais Samia ya kikazi ya siku mbili katika Mkoa wa Arusha kuanzia oktoba 16 mwaka huu.

 

Alisema kuwa Rais Samia atawasili mkoani hapa, Oktoba 16 mwaka huu ambapo siku inayofuata Oktoba 17,2021 Rais Samia atatembelea mradi wa maji uliopo Chekereni, wilaya ya Arumeru ambao ni sehemu ya mradi mkubwa wa Maji unaoendelea wenye thamani ya sh. bilioni 520.

Pia siku hiyo atazindua mradi wa hospitali ya wilaya iliyopo Engutoto jijini hapa unayojengwa na fedha za ndani za halmashauri ya jiji la Arusha.

"Baada ya uzinduzi huo Rais Samia anatarajia kuhutubia wananchi katika uwanda wa mpira wa sheikh Amri Abeid," alisema Mongela.

Mkuu huyo wa mkoa aliongeza kuwa siku inayofuata Oktoba 18 ,Rais Samia  atazindua kiwanda Cha Nyama Cha Elia Food Overseas LTD kilichopo Namanga  wilayani Longido.

Mongela alisema baada ya uzinduzi huo Rais ataelekea Makao makuu ya wilaya ya Longido Kwa ajili ya kuzindua Mradi Mkubwa wa Maji .

"Katika ziara hiyo Rais Samia  atahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika uwanja wa kituo Cha mabasi  wilayani  Longido "Alisema Mongela

Mkuu huyo wa mkoa alitoa Rai Kwa wananchi kujitokeza Kwa wingi kumlaki kiongozi huyo .






0 Comments:

Post a Comment