Showing posts with label Habari kuu. Show all posts
Showing posts with label Habari kuu. Show all posts

 Jaji, Buswalo Mganga awali alikuwa Mkurugenzi wa Mashitakan Nchini, (DPP)

 






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula kwa mwenyeji wake Rais Yoweri Museveni wa Uganda alipowasili Ikulu ya Entebbe leo.```




 




RAIS wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Mhe Sam Kutesa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe alipowasili nchini Uganda kwa ziara ya kikazi ya siku moja leo .



 

TAASISI ya Kiislam ya Twariqa Tul Qadiriyya imesitisha shughuli zao zote kwa siku 21 kuungana na Watanzania wengine kwenye maombolezo ya kifo cha Hayati, Rais John Magufuli aliyadai kuwa aliwaunganisha wananchi wote bila kujali tofauti zao za kiumani.

Aidha, wamempongeza Rais, Samia Suluhu Hassan kwa kuapishwa kuwa Rais wa sita wa Tanzania huku wakiomba wananchi wote bila wamuombee ili Mungu amuepushe na mabaya aweze kuendeleza mambo yote mazuri waliyoyapanga akiwa na Hayati, Rais Magufuli.


Mwenyekiti wa Taifa wa taasisi hiyo, Sheikh Salimu Mubarak maarufu kama Dar-Weish Mti Mkavu alitoa tamko hilo jana jijini hapa akiwa na viongozi kutoka wilaya mbalimbali za mikoa ya Arusha, Dodoma, Tanga na Dar es Salaam waliokuwa wakihudhuria kikao cha bodi ya taasisi hiyo.

"Mimi kama Mwenyekiti wa Taifa wa Twariqa Tul Qadiriyya kwa siku 21 nahairisha masherehe yote, maulid, zikikiri na shughuli zote mpaka maombolezo ya kitaifa yamalizike," alisema Sheikh Salimu na kuongeza.

...Naomba mnapokwenda kwenye mikoa yenu mkawahabarishe wote juu ya masimamo wetu huu kwa sababu ya msiba huu tulio nao kama Taifa. Hayati Rais Magufuli hajazikwa lakini ametuingia moyoni sana,"...

...Alituunganisha soote Watanzania tukawa watu wamoja. Sisi na Wazanzibar tumekuwa wamoja tumeona juzi (machi 23, mwaka huu) matokeo yake. Zanzibar tulidhani hawatampokea ni Waislam lakini kazi waliyoifanya Allah Wakbar hatukuielewa,"...

...Watu wametupa kanga zao akina mama, mashati yao vijana wanajeshi wetu, askari polisi na watu wa chama cha msalaba mwekundu walifanya kazi kubwa kuhakikisha watu wanakuwa salama,".

Sheikh Dar-Weish alisema Hayati, Rais Magufuli alifanya kazi kubwa kuwaunganisha Watanzania wote, Waislam, Wakristu, Wapagani, Wabanian na dini zote na matokeo yake yameonekana namna watu wanavyomlilia kila kona ya nchi.

Aidha alielezea kufurahishwa na hatua ya Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kusitisha kwa muda hotuba yake aliyokuwa akiitoa katika hafla ya kitaifa ya kumuaga Hayati Rais Magufuli mkoani Dodoma  ili kusubiri kumalizika kwa adhana kwa kile alichoeleza imeonyesha ni namna gani kiongozi huyo anaheshimu uhuru wa kuabudu.

WAHIMIZA USHIRIKIANO NA RAIS SAMIA

"Tunaungana na Rais wa sasa, Samia Suluhu Hassan, ni mwanamke lakini ndiyo Rais wetu, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kutupatia Rais ambaye anafahamu kwa kina  kile kinachopaswa kuendelea kufanyika," alisema Sheikh Dar-Weish na kuongeza.

... Mama Samia alikuwa na Rais Magufuli kwa miaka mitano wakiendesha nchi, anamfahamu hayati Rais Magufuli kuliko sisi. Sisi hata tukasema yapi mazuri lakini bado hatujafikia yale anayofahamu Rais Samia,"..

...Tunamuombea Rais Samia kwa Mwenyezi Mungu aendeleze pale alipoacha Hayati Rais Magufuli. Yeye na Mawaziri wake wawe kitu kimoja kupona kwa wao ndiyo kupona kwetu raia,".


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Twariqa Tul Qadiriyya, Rehema Athuman aliwaomba wananchi wote kwa umoja wao waungane kuomboleza na  kumuombea heri Hayati, Rais, Magufuli mbele za Mungu na kumuombea pumziko jema.


Naye, Katibu mkuu wa  Twariqa Tul Qadiriyya, Abdi Kisiu, Hayati, Rais, Magufuli wakati wa uhai wake aliwanyanyua wanyonge na kuwaunganisha wananchi wote bila kujali tofauti zao za kiimani huku akitolea mfano namna alivyoweza kuchangisha fedha kanisani kwa ajili ya kuwajengea  msikiti, Chamwino Dodoma.


Alisema kuwa kila alipokuwa akipelekewa matatizo hakuyadharau alikuwa akifanya kazi akishirikiana na viongozi wote wa dini bila kubagua.








 

 





 WAZIRI Mkuu ,  Kassim Majaliwa leo tarehe 20 Februari, 2021 ameongoza mamia ya waombolezaji kwenye maziko ya aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, Mhandisi, John William Kijazi yaliyofanyika kwenye makaburi yaliyoko katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Augustino Manundu Korogwe, Tanga.




Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Salum Hamduni


 JESHI la polisi mkoani Arusha linamshikilia Mbise Lukumo, (30) kwa tuhuma za mauaji ya wanawake mbalimbali jijini hapa likiwemo la Anna Edward,(44) aliyeuawa januari 25, mwaka huu na kupelekea maandamano makubwa ya wanawake.


Kamanda wa polisi mkoani hapa, Salum Hamduni amewaeleza waandishi wa habari leo ofisini kwake kuwa, Lukumo ambaye ni mkazi wa Olasiti, jijini hapa alikamatwa januari 27, mwaka huu.

"Baada ya kuhojiwa alikiri kuhusika na tukio hilo la mauaji pamoja na matukio mengine yaliyotokea siku za nyuma," alisema kamanda Hamduni.

Aliyataja matukio mengine ya mauaji ya wanawake mtuhumiwa huyo anayodaiwa kukiri kuyafanya ni pamoja na lile la Mei 21, 2019 lililotokea Lolovono jijini Arusha ambapo Lukumo alikiri kushirikiana na  wenzake kumuua Stella Daniel, (22).

Tukio lingine ni lile la januari 16, mwaka huu lililotokea maeneo ya Ngaramtoni ya chini ambapo mtuhumiwa huyo anadaiwa akishirikiana na wenzake walimuua mwanamke, Bahati Prosper, (35).

"Baada ya kumhoji zaidi aliwataja washirika wenzake ambao ni Lembeka Olomorojo, (65) mkazi wa Osunyai jijini Arusha ma Bashiri Msuya ,(64), mganga wa kienyeji mkazi wa Kirika B, kata ya Osunyai jijini Arusha," amesema kamanda Hamduni na kuongeza.

"Hata hivyo chanzo cha tukio hilo imebainika kwamba  ni imani za kishirikina. Mara baada ya upelelezi kukamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya mashitaka kwa hatua zaidi za kisheria,".

Januari 30, mwaka huu wanawake waliandamana na kufunga barabara ikiwa ni njia ya kufikisha ujumbe kwa serikali juu ya matukio ya mauaji ya wanawake yaliyoonekana kukithiri.

Maandamano hayo yalifanyika siku ya mazishi ya Anna mkazi wa kona ya A to Z kata ya Matevezi jijini Arusha ambapo mandamano hayo yalivuta hisia za wengi jijini hapa.

 

 



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa, ameiagiza mifuko na programu zote za uwezeshaji zifanye tathmini ya shughuli na huduma zake ili kubaini mafanikio, changamoto na maeneo yanayohitaji uboreshaji hususan eneo la masharti ya utoaji mikopo kwa wajasiriamali.


Ameyasema hayo  Februari 9, mwaka huu wakati akifungua amefungua maonesho ya nne ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi yanayoendelea katika Viwanja vya Shiekh Amri Abied jijini Arusha. 



Waziri Mkuu ameitaka mifuko inayotoa dhamana kwa wafanyabiashara na wajasiriamali mbalimbali nchini, iimarishe usimamizi, uratibu na utendaji wake kwa kutengeneza mipango maalum ya kila mwaka inayoonesha malengo ya dhamana zitakazotolewa katika mwaka husika.
 

Amesema mipango maalumu itakayoandaliwa na mifuko inayotoa dhamana kwa wafanyabiashara na wajasiriamali inatakiwa iwasilishwe Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na baadaye taarifa za utekelezaji zitolewe katika kipindi cha kila robo mwaka.
 
“Wasimamizi na Watendaji wa mifuko na programu pamoja na walengwa jiepusheni na vitendo vya rushwa kwani rushwa ni adui wa haki na ni kikwazo kikubwa cha maendeleo. Pia, watendaji wa mifuko na programu za uwezeshaji pamoja na taasisi za fedha hakikisheni mnatoa huduma bila urasimu wala ubaguzi wa aina yoyote. Nasisitiza wananchi wanapofika kwenye ofisi zenu wapokelewe kwa staha, wasikilizwe na kupatiwa huduma stahiki kwa wepesi.”
 
Aidha, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  amezitaka Halmashauri nchini zihakikishe zinatenga asilimia 10 ya mapato yake ya fedha za ndani ili zitumike kutoa mikopo kwa vijana (asilimia 4), wanawake (asilimia 4) na watu wenye ulemavu (asilimia 2). Pia, ametoa wito kwa Mabaraza ya Madiwani katika kila Halmashauri kufuatilia utekelezaji wa maagizo haya ya Serikali ambayo yameridhiwa na Bunge na kutungiwa sheria mahsusi.”


MAHAKAMA Kuu kanda ya Arusha imemuru kuuzwa kwa awamu mali za hoteli ya kitalii ya Impala ili kulipa madeni ya malimbikizo ya mishahara ya wafanyakazi wa hoteli hiyo na Naura  yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 500.

Wafanyakazi wa hoteli za Impala na Naura Sping wakimsikiliza Kaimu Afisa kazi mkoani Arusha, Emmanuel Mweta aliyekuwa akiwaeza uamuzi uliotolewa na mahakama

Aidha imeamuru fedha zitakazobaki mara baada ya wafanyakazi hao kulipwa zikabidhiwe benki ya NBC ambayo inaidai hoteli hiyo zaidi ya shilingi bilioni 1.5
Jaji, Mohamed Gwae ametoa amri hizo,  Januari 8, mwaka huu wakati akitoa uamuzi kwenye maombi ya pingamizi yaliyowasilishwa na kampuni ya Impala na benki ya NBC wakipinga kutekelezwa kwa amri ya ukamataji na uuzwaji wa mali za Impala ili kulipa madeni ya mishahara.


Amri hiyo ilitolewa  na Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha , Masijala ndogo ya kazi.
"Kwa kuwa hakuna 'secured creditor' mwingine zaidi ya benki ya  NBC ambaye hana pingamizi ila anataka alipwe kile kutakachobaki baada ya mali kuuzwa na wafanyakazi kulipwa madai yao," alisema jaji Gwae akitoa uamuzi wake na kuongeza.


...unaposema kiuzwe ila kisiuzwe chini ya kiwango ambacho kimethaminiwa. Msiuze kwa mradi tu unauza.


Nilikuwa najiuliza kwenye hiyo kesi nyingine ambapo kuna Kiwanja namba 16, 17, 18 na 19 vile ni tofauti na vile 20, 21, 22 na 23 sasa kwa nini kwani vile havitoshi mpaka muuze vyote? ...


...Naomba majibu hawa waliofanyia tathmini manake mimi sivijui sisi tunaongelea kwenye makaratasi hatujaviona najua Impala manake nimelala najua Naura na Ngurdoto,".


Mkurugenzi Pelagia alimfafanualia Jaji Gwea kuwa viwanja hivyo ni tofauti ingawa hivyo ambavyo namba zake zimefuatana vimeungana viwanja viwili vina hati moja.


"Kwa nini msiuze hivi 20, 21, 22 na 23 kwanza hivi kama isipopatikana ndipo muuze hivyo vingine. Wanasema usishangilie kifo cha mwenzako manake na wewe utakuja kufa tu hakuna yeyote atakayeenda mbinguni bila kufa," alisema Jaji Gwea wakati akitoa uamuzi wake huo na kuongeza.


...Mimi natoa amri hii viuzwe kwanza viwanja namba 20 mpaka 23 kama hakuna utimilifu wa hiyo tuzo ndiyo mnaenda kwenye mambo mengine,".


Baada ya uamuzi huo Pelagia alisema kwa kuwa mmliki wa Naura na Impala ni mmoja hivyo fedha zitakazopatikana zitalipa madeni ya yote jambo ambalo jaji aliweleza kuwa hayo hayaihusu mahakama kama wanaweza kufanya hivyo wafanye kinachotakiwa wafanyakazi walipwe kabla mali hazijauzwa.


HOJA ZA BENKI YA NBC

Awali akipitia hoja za waleta maombi, Jaji Gwae alisema kuwa Benki ya NBC iliwasilisha hoja tano za pigamizi kupitia wakili, Wilbard Massawe kutoka kampuni ya Mawalla.


Alisema wakili Massawe aliieleza mahakama kuwa hana shida na kuuzwa kwa mali zilizokamatwa ila izingatiwe tu kwamba benki ina maslahi na benki itakuwa tayari kupata kile kitakachokuwa kimebaki baada ya wafanyakazi kulipwa madeni yao.


"Hata hivyo kwenye hoja zao walisisitiza kutambuliwa kuwa wanaidai Impala hivyo walipwe fedha zitakazobaki mara baada ya wafanyakazi kulipwa madeni yao?" alisema Jaji Gwae akisoma hukumu hiyo.


Alisema kuwa Kaimu afisa kazi mkoani Arusha, Emanuel Mweta, alikubaliana na hilo kwa kile alichoeleza kuwa kwa kuwa NBC haipingi wafanyakazi kulipwa malimbikizo ya mishahara yao.


HOJA ZA IMPALA


Jaji Gwae alisema kuwa, Wakili wa Impala, Richard Massawe aliwasilisha maombi ya pingamizi chini ya hati ya kiapo akidai kuwa mali zilizoamriwa kukamatwa zina thamani kubwa kuliko madeni ya mshahara wanayodaiwa.


Alidai mali zilizoamriwa kukamatwa na kuuzwa zina thamani ya zaidi ya shilingi bilioni tano wakati madeni ya malimbikizo ya mishahara ni zaidi ya shilingi milioni 500.


Jaji alitupilia mbali pingamizi la Impala walilokuwa wanadai Kaimu Afisa kazi wa mkoa, Mweta hakuwa sahihi kufungua maombi hayo mahakamani kwani sheria inataka kamishina wa kazi ndiyo ayafungue.


"Nimepitia sheria nimeona afisa kazi anaweza kufungua mashauri hayo kwani anamwakilisha kamishina wa kazi.Ukizingatia mleta maombi namba moja (Impala) na utayari wake wa kuwalipa wafanyakazi nimeona maombi haya hayana msingi," alisema Jaji Gwae na kuongeza.


...Kwa kuwa yule anayedaiwa kuwa kuna suala la 'guarantee' ambapo mkopo ulichukuliwa (NBC Bank) anasema yeye hana pingamizi. Kama wangekuwa wale ndo wanapinga ingetakiwa waangaliwe manake wale ndiyo wana 'secured creditor',".


Jaji Gwae alisema kuwa kwa kuwa NBC anayetaka atambuliwe  baada ya kuuzwa hivyo vitu hivyo kwa msingi huo kuna hivyo viwanja ambavyo vimeshafanyiwa tathmini ya juu bilioni 1.8 lakini wao (Impala)  wanasema ni bilioni 8 ingawa hakuna tathmini nyingine iliyofanyika.


"Kwa kuzingatia kwamba kutoka Novemba mwaka jana kesi hii iko hapa mahakamani lakini kwa kuzingatia pia wale wanaowakilishwa na mjibu maombi, Afisa kazi, (wafanyakazi) hawajalipwa mshahara mpaka leo, na kwa kuzingatia kwamba mleta maombi habishi kwamba anadaiwa na wafanyakazi naamuru uuzwaji wa mali iliyokamatwa kwa amri ya msajili iuzwe haraka baada ya kutangaza," alisema jaji Gwea akimaliza kutoa uamuzi kwa upande wa hoteli ya Impala. 


HOTELI YA NAURA SPRING


Jaji Gwae pia alisoma uamuzi kwenye maombi ya pingamizi ya hoteli ya Naura Spring dhidi ya utekelezwaji wa amri ya Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha , Masijala ndogo ya kazi ya kuuzwa kwa magari matano na viwanja vinne.


"Sitarudia hoja zote za mawakili na afisa kazi manake ni zilezile ila mali zilizokamatwa ni magari matano na yamefanyiwa utathmini Kesi hii inahusu utekelezaji na 83/2020 ndiyo walifungua kwa msajili," alisema Jaji Gwae.


Alisema "hoja ya mawakili wa Impala kuwa wakurugenzi, Kama Rando (Mrema) hakuwa mkurugenzi lakini Pelagia Mrema yupo lakini pia wasimamizi wa mali za marehemu wapo tulitegemea wafanye kiapo kwamba huyu hakuwa mkurugenzi kubatilisha kikao cha Machi 14, 2019 kilichowateua Rando na Janet,".


....Kama wale kina Herode waliokuwa wanaiwakilisha kampuni kwenye kesi  kama wasingekuwa wanatambuliwa na mkurugenzi, Pelagia lakini pia kwa wasimamizi wa mirathi wa marehemu, Mrema, Micheli Mrema wangefanya kiapo cha kuwakana vinginevyo wakili utabaki unasema tu ila wao hawajasema chochote," alisema Jaji Gwae.


WAFANYAKAZI WA IMPALA WANENA

Baadhi ya wafanyakazi wa hoteli za Impala na Naura wakiwa kwenye viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Masijala ndogo ya Kazi Arusha 



Kiongozi wa wafanyakazi wa Impala na Naura Jacob Joel alisema wanaishukuru mahakama na serikali kupitia ofisi ya idara ya kazi ambayo ndiyo waliowawakilusha kwenye shauri hilo.


 "Tunaishukuru sana  mahakama kwa kutupatia haki yetu maana kwa sasa hivi ni takribani miezi 16 tumekuwa tukisota bila kupata mishahara," alisema Jacob.


Alisema wafanyakazi wa Impala wanadai zaidi ya milioni 397 na wafanyakazi wa Naura wanadai zaidi ya shilingi milioni 107 ikiwa ni malimbikizo ya mishahara.
" Tunadai zaidi zaidi ya milioni 500 maana mpaka sasa bado hawajatusimamisha kazi, bado tunatambuliwa kama wafanyakazi kwa sababu bado hawajatupa barua za kutusimamisha kazi," alisisitiza Jacob.



 Kamanda wa polisi mkoani Arusha, (RPC), Salumu Hamduni

MKAZI wa Elerai jijini Arusha, Badru Abdallah, (38) anadaiwa kumchoma kwa pasi mtoto wake mwenye umri wa miaka 12.


Kamanda wa polisi mkoani hapa, Salumu Hamduni ameeleleza kupitia taarifa yake aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari kuwa tukio hilo lilitokea januari 16, mwaka huu majira ya saa mbili usiku.

Mtoto mdogo jina limehifadhiwa miaka 12, alijeruhiwa kwa kuchomwa na pasi ya umeme mgongoni na Baba yake mzazi aitwaye Badru Abdallah, (38), )mrangi na mkazi wa Elerai," alisema kamanda Hamduni.


Alisema kuwa  mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi na mara baada ya upelelezi kukamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya mashtaka kwa ajili ya hatua zaidi. 



 Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Salum Hamduni

Mkazi wa Sakina, Olaiis Wavii (46) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake mwenye umri wa miaka mitatu.


Inadaiwa mtoto huyo anayesoma shule ya awali ya New Life alibainika kuwa na tatizo la kutokwa na haja ndogo mfululizo ndipo ikabidi afanyiwe uchunguzi wa kitababu ikabainikwa kuwa anabakwa.

Kamanda wa polisi mkoani Arusha, (RPC), Salum Hamduni ametoa taarifa kwa vyombo vya habari jana na kueleza kuwa mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la polisi.

Alisema kuwa tukio hilo lilijulikana januari 25, mwaka huu majira ya saa  4:30 asubuhi 
kwenye  katika kijiji cha Olosiva, kata ya Olorieni wilayani Arumeru.

Kamanda Hamduni alisema kuwa alibaini  tukio hilo nk  afisa ustawi wa jamii wa eneo hilo, (hakumtaja jina) wakati akiwa anaendelea na shughuli
zake maeneo ya kijiji hapo.

" Afisa ustawi wa jamii alibaini kuwa mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitatu jina limehifadhiwa mwanafunzi wa shule ya awali iitwayo NEW LIFE iliyopo Olasiva Sakina akiwa anatokwa na mkojo mfululizo," alisema Kamanda Hamduni na kuongeza.

...Ndipo alipotoa taarifa katika kituo cha polisi na baadaye kufanya uchunguzi wa kitabibu ndipo alipo gundulika kuwa mtoto huyo amebakwa,". 

...Jeshi la polisi Mkoani hapa lilianza uchunguzi wa tukio hilo na kubaini baba mzazi aitwaye OLAIIS S/O WAVII (46) mmasai na mkazi wa sakina ndiye aliyembaka mtoto huyo,". 

RPC, Hamduni, alisema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi na mara baada ya upelelezi kukamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya mashtaka kwa ajili ya hatua.

"Natoa wito kwa wazazi na walezi wenye tabia ya kujihusisha na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kuacha vitendo hivyo mara moja kwani ni kinyume na taratibu za nchi," alisema Kamanda Hamduni na kuongeza.

....Pia niyaombe madhebu ya dini kuwakumbusha na kuwapa elimu waumini wao kwenye nyumba za ibada,". 


 Serikali imetoa miezi mitatu kwa wenye shehena ya vifungashio visivyokidhi viwango vya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) vinaondolewa sokoni.



Agizo hilo limetolewa  Januari 8, 2020 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Ofisi hiyo jijini Dodoma kuhusu matumizi ya vifungashio vya plastiki kutumika kama vibebeo vya bidhaa.

Ummy alisema hatua hiyo ya Serikali imechukuliwa baada ya kuwepo kwa vifungashio vinavyotumika kama vibebeo vilivyozagaa madukani, sokoni na maeneo mbalimbali.

Alisema kuwa pamoja na mafanikio yaliyopatikana kutokana na katazo la mifuko ya plastiki siku za hivi karibuni kumejitokeza changamoto ya matumizi ya vifungashio vya plastiki aina ya tubings visivyokuwa na sifa na hivyo kutokukidhi matakwa yaliyowekwa na TBS.

Aidha, Waziri Ummy aliongeza kuwa vifungashio hivi kwa sasa vinazalishwa kwa wingi na kwa ukubwa mbalimbali na vimekuwa vikitumika kama mifuko ya kubebea bidhaa sokoni na kuleta dhana kuwa mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku imerudi kivingine kama “vifungashio”.

Alisema mifuko hii imeanza kuzagaa kwenye mazingira ya mitaa yetu na vijiji vyetu kwa kasi kubwa,  na hivyo kurudisha nyuma mafanikio makubwa tuliyoyapata katika kipindi chote cha kupambana na changamoto ya mifuko ya plastiki.

Kwa mantiki hiyo Waziri Ummy aliwataka wasambazaji, wazalishaji wa vifungashio hivi na waagizaji kuacha mara moja kuzalisha, kusambaza, kuuza na kutumia vifungashio hivyo na kusisitiza kuwa baada ya kipindi hicho Serikali haitatoa tangazo lingine lolote kuhusiana na katazo la matumizi ya vifungashio visivyokuwa na ubora.

Waziri huyo alisema Serikali itachukua hatua kali kwa mujibu kisheria na katika kipindi hiki tunaendelea na operesheni maalumu kuwabaini wanaokwamisha mafanikio haya kwa kuzalisha na kusambaza vifungashio hivyo na hatutawavumilia watu hawa.



Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Joseph Malongo alisema Ofisi hiyo itashirikiana na TBS kuanza kampeni ya kupitia tena mifuko ya ‘non woven’ kwani kuna uwezekano wa kuwepo kwa mifuko isiyo na viwango.

Malongo alisema Serikali ilipoweka katazo la mifuko ya plastiki iliweka pia viwango vya mifuko ya aina hiyo akitaja kuwa ni lazima iwe na uzito wa gramu 70 kwa mita ya mraba moja ili itumike kwa zaidi ya mara moja.

Aliongeza kuwa pia lazima mifuko hiyo iwe na nembo ya TBS ili kuonesha kuwa imekidhi vigezo vinavyotakiwa pamoja na kutambulisha jina la mzalishaji.

Kigezo Kingine ni viwe na lakiri (Seal), ikimaanishwa kuwa kifungashio kinatakiwa kifungashwe na anayefungasha bidhaa yake ili kuuza kabla ya kwenda sokoni.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Ruvuma, Hamza Mwenda ahakikishe anawakamata viongozi wa AMCOS kwa tuhuma za kutoa fedha za wanachama na kuwapa madiwani ili wakawashawishi madiwani wenzao wakubali kubadilisha eneo la ujenzi wa ofisi za Halmashauri ya Wilaya mji wa Mbinga mkoani Ruvuma.


Aliyasema hayo jana Januari 4, 2021 wakati akizindua jengo la Ofisi ya Halmashauri hiyo.

Madiwani waliohusika katika mvutano huo ni wa kata za Mkumbi (Bruno Kapinga), kata ya Lukalasi (Bosco Ndimbo) na wa kata ya Linda (Haule), ambao wanadaiwa kuchukua fedha kutoka kwa watendaji wa AMCOS kwa ajili ya kwenda kushawishi madiwani wenzao wakubali kuhamishwa kwa eneo la ujenzi wa makao makuu ya halmashauri hiyo.



Pia, Waziri Mkuu alikagua nyumba 7 za Wakuu wa Idara za  Halmashauri ya Mji wa Mbinga zilizojengwa  na Serikali kwa gharama ya sh. Milioni 321.771.


Awali ,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga, Grace Quintine alimweleza Waziro mkuu kuwa lengo la miradi hiyo ni kuboresha mazingira ya makazi ya watumishi wa halmashauri ikiwa ni pamoja na kupunguza kilipa posho za nyumba kwa kila mwezi


 



Maria na Consolata wakiwa kidato cha sita mwaka 2017
Image captionMaria na Consolata wakiwa kidato cha sita mwaka 2017

"Maumbile ya Maria na Consolta ndio sababu kubwa iliyochangia kifo chao" Daktari Mseleto Nyakiloto ameeleza hayo alipozungumza na BBC.
Mseleto Nyakiloto ambaye ni daktari bingwa wa upasuaji na mganga mfawidhi wa hospitali ya Iringa ameeleza chanzo kilichopelekea wasichana hao kufariki ni tatizo la njia ya hewa.
"Mmoja alitangulia na mwingine alifariki baada ya dakika kumi,Maria ndio alikuwa ana tatizo la kiafya kwa kuwa mapafu yake yalishindwa kufanya kazi na huyu mwingine alikufa kutokana na viungo vingi katika mwili wao wanavitumia kwa pamoja".Dr.Nyakiloto aeleza
(HABARI KWA HISANI YA BBC)

ta

Miguu yao ilikuwa imechukua sehemu kubwa ya mwili,
Kwa Maria mguu wake wa kulia ndio ulikuwa na nguvu wakati Consolatha ulikuwa wa kushoto na miguu yao mengine ilikuwa haifanyi kazi.
Walikuwa na vichwa viwili,mioyo miwili na mikono minne.
Na walikuwa wanatumia viongo vingine kwa pamoja kama tumbo,ini,sehemu ya uke na haja.
Maria alikuwa na matatizo ya kiafya tangu alipozaliwa ,alikuwa na shida ya kupumua ingawa licha ya kuwa alikuwa ana uwezo wa kula chakula zaidi ya mwenzie.
Maria alikuwa akila kwa niaba ya ndugu yake kwa takribani miaka mitano na nusu ndipo Consolata na yeye alipoanza kula mwenyewe.

Wanatumia baadhi ya viungo kwa pamoja

Dr Rainer Brandl aliiambia BBC Network Africa mwaka 2004, kuwa mapafu yao yalikuwa hayako sawa kwa namna ambayo hawawezi kuimili miili yao na hayawezi kuongezeka zaidi.
Na kilichobaki ni kuwaombea ili waendelee kuishi kwa matumaini. 
Katika maisha yao kutegemeana ndio jambo la kubwa na kawaida katika maisha yao,kwa mfano Maria akitaka kwenda chooni atamjulisha mwenzie na vivyo hivyo kwa Consolata.






Hata hivyo daktari huyo aliongeza kwa kusema kwamba mzunguko wa hewa na damu ndio umesababisha kifo cha cha mwingine hivyo matarajio ya mmoja kupona yasingewezekana.


Maria na Consolata walikuwa wakitumia kwa pamoja baadhi ya viungo vyao
Image captionMaria na Consolata walikuwa wakitumia kwa pamoja baadhi ya viungo vyao






Aidha daktari Nyakiloto amesema mapacha wa aina hii wapo wa aina nyingi ingawa muda wa maisha yao huwa unatofautina kutokana mazingira pia; kuna wale ambao hata hawafikii hatua ya kuzaliwa,wengine wanakaa muda mfupi wanafariki na wengine ndio wanajitahidi wanafikia umri mkubwa kama ya kina Maria na Consolata wameweza kufika miaka 21.


Maria na Consolata walipokuwa na miaka sita
Image captionMaria na Consolata walipokuwa na miaka sita

Mwaka 2004,BBC iliandika juu ya watoto hawa mapacha ambao walikuwa na miaka sita kuwa maisha yao yako kwenye mashaka.
Tatizo kubwa ambalo lilikuwa linawasumbua ilikuwa mapafu yao yana uzito mkubwa kuliko mwili wao.
Madaktari walikuwa na hofu juu ya tatizo la mmoja linaweza kusababisha mwingine kuathirika na kuwafanyia upasuaji,kutaongeza tatizo kuwa kubwa zaidi.





Maria aliwahi kula kwa ajili ya mwenzake kwa miaka mitano.

Moja ya nyumba iliyoathirika na Mvua
Kufuatia Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini baadhi maeneo yameathirika na mvua hizo za awali.

Katika Mkoa wa Arusha Habari Tanzania tunaripoti Tukio la January 2 katika wilaya ya Meru ambapo kaya nne ziliathirika na mvua hizo kwa kuvunjiwa nyumba zao na uharibifu Mkubwa wa vyakula.

Kaya zilizoathirika na mvua hizo zipo kwenye kitongoji cha Nkoamangashi katika Kata ya Kikatiti. Familia hizo ni kama ifuatavyo Famila Charles Litoi mbise, Familia ya Bw. Frank Charles, familia ya Emanuel Wariaeli, na Familia ya Ndugu Afraeli Emanuel. 

Kufauatia athari hizo Viongozi wa maeneo hayo Kitongoji hadi kata wakawa karibu zaidi kuzinusuru familia hizo kutokana na janga hilo.

Diwani wa kata ya Kikatiti Mh. Elias Mungure akawataka wasamaria wema kuungana na wanakitongoji hao ili kufidhia hasara zilizotokea na kuzinusuru kaya hizo dhidi ya njaa baada ya vyakula kuharibiwa.
Diwani wa Kata ya Kikatiti Mh Elias Mungure akitoa maelekezo wakati akiwapa pole wahanga wa Tukio hilo.
Mungure ameyasisitiza hayo wakati alipoitembelea kaya hizo nakutoa mifuko 8 ya Saruji pamoja na Gunia moja la Mahindi na kuahidi kuwapatia mabati kwa ajili ya kuezeka nyumba za Mara baada ya marekebisho.
Mifuko 8 ya Saruji na Chakula kwa familia zilizoathirika na mvua iliyonyesha hapo Jana.

Awali  Mwenyemiti wa kitongoji hicho Jacob Emanuel alieleza tukio hilo lilivyotokea na kuwa wa kwanza kutoa msaada wa haraka pamoja na kutoa taarifa kwa viongozi wengine kwa ajili ya msaada zaidi.

Wakati mvua hizo zikinyesha na tukio hilo kutokea majira saa tisa za alasiri mmoja wa mwana kaya alieleza ilivyokuwa huku kwa bahati nzuri Hakukua na mtu aliyejeruhiwa.

Mashuhuda wanasema mvua kubwa iliyoambatana na Upepo mkali , mawe ya barafu iliezua mabati ya nyumba na pelekea kuta za nyumba kuvunjika bibaya , Ripoti hii pia ilishuhudia hali ya nyumba hizo pamoja na Miti mikubwa ya maeneo hayo ilivyovunjwa vunjwa ovyo. 
Mwanamuziki anayefahamika kwa jina maarufu Kwenye mtandao wa YouTube la 'Sister Fey' Amemuomba Ruge Mutahaba na Clouds Media kwa ujumla kumsaidia kupromote Kazi zake, halikadhalika Diamond Platnumz pamoja na Label yake ya WCB Wasafi na Mtangazaji Nguli Millard Ayo. Play hii Video hapa Chini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari hivi karibuni katika Mahojiano Maalum Amesema Sera ya Elimu bure imekuwa na mafanikio katika Wilaya hiyo kwani imekuwa hamasa kubwa kwa jamii za kifugaji katika Wilaya ya Karatu.

Bw. Moris amewaambia Waandishi wa Habari kuwa pamoja na Sera ya Elimu bure kuwa msaada Mkubwa katika Wilaya hiyo kumekuwa na changamoto kadhaa inayoikabili sekta ya Elimu ikiwa ni pamoja na baadhi ya wanafunzi wa jamii ya kifugaji kuwa na tabia ya kutoroka masomo Mara kwa Mara kitendo kinachodhoofisha Maendeleo ya Elimu katika Wilaya hiyo.

Licha ya Miundombinu ya majengo kuwa changamoto katika baadhi ya Halmashauri mbalimbali nchini kwa mujibu wa Mkurugenzi Moris  Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Haina tatizo la uhaba wa Miundombinu ya Madarasa.

Aidha Mkurugenzi Moris ameleza kuwa Karatu ina makabila ambayo haipatikani maeneo mengine ya Mkoa wa Arusha ikiwemo jamii ya Wahazabe jamii na Jamii za kifugaji jamii ambayo ina mifumo ya kuhama hama hivyo kupelekea watoto wao kushindwa kuhudhuria masomo.

Kufuatia adha hiyo Halmashauri imekuwa ikilazimika kufanya misako ya Mara kwa Mara ili kuwarudisha wanafunzi wanotoroka shule ili kuendelea na masomo hivyo kukwamisha shule hizo kufanya vizuri.

Mkurugenzi Moris amesema Halmashauri yake imedhamiria kujenga Bweni katika baadhi ya maeneo ambayo imezungukwa na Jamii nyingi za kifugaji na jamii ya wahazabe jamii inayoishi kwa Uwindaji na kula matunda.

Katika Hatua nyingine Moris ameongeza kuwa Ujenzi wa Bweni hizo ukikamilika itasaidia kuhakikisha kuwa wanafunzi hao kutoroka masomo yao hivyo itachangia kuongeza ufaulu katika shule zao.

Katika matokeo ya Darasa la Saba mwaka 2017 Halmashauri ya Karatu imeshika nafasi ya 6 kati ya Halmashauri saba za Mkoa wa Arusha.
Katika kutekeleza  juhudi za serikali ya awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli ya kuwa Tanzania ya viwanda Shirika lisilo la kiserili la ACE - AFRICA limetoa msaada wa mashine ya kusagia na kukobolea nafaka kwa kikundi cha wajasiriamali cha Loluvo kijiji cha Oloitushula kata ya Musa kwa lengo la kufanya kiwanda cha usindikaji wa unga wa nafaka.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mashine hiyo Meneja wa Idara ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ndugu Salumu Lubuva kwenye ofisi ya kijiji cha Oloitushula amesema kuwa shirika la ACE AFRICA linaunga mkono juhudi za serikali kwa vitendo kwa kuwezesha wananchi kujiunua  kiuchumi  ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2035 kwa Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Lubuva amesema kuwa shirika limetoa mashine kwa kikundi cha Loluvo yenye thamani ya shilingi 6,200,000/= kwa lengo la  kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kubadilisha maisha yao, familia zao na jamii kwa ujumla.

Amefafanua kuwa mashine hiyo inatakiwa kufanyika kiwanda cha kusindika unga na kuweka kwenye vifungashio na kuuza kwa wingi zaidi.

Aidha Lubuva amefafanua kuwa kabla ya kuwakabidhi mashine wajasiriamali hao walianza kwa kuwawezesha kwa kuwapa mafunzo ya kuwajengea uwezo kuweza kuendesha biashara ikiwa ni pamoja na  kutunza kumbukumbu za mapato na matumizi, kutunza kuweka na kukopo, masoko na kuziona fursa. 

Hata hivyo Lubuva amewaasa wajasiriamali hao kusimamia vizuri mradi huo kwa endapo watashindwa kuendeleza mashine hiyo itanyang'anywa na kupeleka kwa wahitaji wengine na zaidi amewataka wajasiriamali  hao kuhakikisha wanakabiliana na changamoto za migogoro ya kuendesha biashara ya pamoja kwenye vikundi.

"Inapotokea kutokuelewana ni  vema kukaa na kuzungumza kwa kushirikisha viongozi wa kata na kijiji pamoja na shirika letu ili kutatua mgogoro na kusonga mbele" amesema Lubuva

Naye mkuu wa kitengo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi shirika la Ace Africa ndugu John Emanuel amesema kuwa wametoa mashine hiyo ili ifanyike kuwa  kiwanda kidogo ambapo licha ya kutoa huduma ya kusaga na kukoboa nafaka za wananchi wanaowazunguka wanapaswa kwenda mbele zaidi kutengeneza unga kwa kufunga kwenye mifuko na kuuza ndqni na nje ya kata ya Musa.

"Mradi huu wa mashine muufanye kuwa kiwanda cha kusindika  na kupark  unga ili  kuuza ndani na nje ya kata ya Musa hata mkoa mzima wa Arusha na Tanzania nzima" amesema John

Mwenyekiti wa kikundi cha Loluvo ndugu Upendo John ameonesha furaha yake na kukiri kuwa mashine hiyo ni mkombozi  wa kujikwamua kiuchumi na jamii ya wananchi wa Oloitusha.

Aidha amefafanua  kuwa  licha ya kuwa mashine hiyo kuwapatia fedha za kuinua vipato lakini pia mashine hiyo itawezesha kusaidia jamii yao kupata huduma ya kusaga na kukoboa karibu  zaidi tofauti na hapo awali huduma ya mashine haikuwepo kijijini hapo.

"Hii ni kiwanda kidogo mashine imekuja kutukomboa kwa kuwa tumekuwa tukipata huduma ya kusaga umbali wa zaidibya kilomita kumi,  tunaenda kusaga Nengun'gu  kule Monduli au Kisongo madukani sasa huduma ipo nyumbani" amesema mwenyekiti huyo

Evaline Wlison mwanakikundi amethibitisha kuamini kuwa mashine hiyo itawakwamua kiuchumi na kuahidi kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano ili kufikia malengo waliyoyakusudia wakati wa kuomba msaad huo wa mashine.

Aidha  Shirika la Ace Africa linategeme kutoa mashine tatu ikiwa mashine mbili zimeshatotolewa moja kwa kikundi cha wajasiriamali wa kijiji cha Oloitushula na Ngorbob kata ya Matevesi na wanategeme kutoa mashine nyingine kijiji cha Olelosi kata ya Kimnyaki.

Shirika la Ace Africa linafanya shughuli mbalimbali za kijamii kwenye kata 12 za Tarafa ya Mukulat katika halmashauri ya Arusha ikiwa ni pamoja na uelimishaji wa Haki na ulinzi na usalama wa mtoto, Afya ya Lishe pamoja na uwezeshaji vikundu vya wananchi kiuchumi.

PICHA ZA MATUKIO YA MAKABIDHIANO YA MASHINE HIYO.