Showing posts with label Sabaya. Show all posts
Showing posts with label Sabaya. Show all posts



MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha imefuta rufaa iliyokuwa ikimkabili Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake watano baada ya Mkurugenzi  wa Mashtaka Nchini (DPP) Silvester Mwakitalu, kuwasilisha  ombi la kuiondoa Rufaa hiyo namba 155/2022 .

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Sabaya akitoka mahakamani akiwa ameambatana na wakili wake, Moses Mahuna mara 





Rufaa hiyo ilikatwa na Jamhuri baada ya Sabaya na wenzake kushinda kesi  ya Uhujumu uchumi namba 27/2021 katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha ambapo uamuzi huo ulitolewa na Hakimu Mkazi, Dkt Patricia Kisinda.
Rufaa hiyo ilipangwa kusikilizwa  Mfululizo  Mahakama kuu Kanda ya Arusha kuanzia Aprili 29, 2024 mpaka Mei 03, 2024 mbele  ya  Jaji, Salma Maghimbi wa Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam aliyekuwa akisikiliza rufaa hiyo.
Akiwasilisha nia Ya kuliondoa shauri hilo mbele ya Jaji Salma,  wakili wa serikali Akisa mhando aliieleza mahakama hiyo upande wa Jamhuri hauna nia ya kuendelea na rufaa hiyo dhidi ya Sabaya
 “Mhe Jaji, Shauri hili limekuja kwa ajili ya kusikilizwa ,hata hivyo mrufani (Jamhuri) imewasilisha ombi chini ya kifungu cha sheria No.386 (1) cha sheria ya muenendo wa makosa ya jinai marejeo ya mwaka 2022,ombi letu ni kwamba Jamhuri haina nia ya kuendelea na Rufaa hii dhidi ya Sabaya na wenzake,hivyo tunaomba kuiondoa hapa mahakamani," Mhando aliomba mahakamani japo.
Upande wa wajibu rufaa hawakuwa na pingamizi juu ya ombi hilo hivyo Jaji Maghimbi alitoa uamuzi kwamba rufaa hiyo imeondolewa mahakamani rasmi.
Kufuatia uamuzi huo, sabaya anakuwa hana shauri lolote linalomkabili mahakamani na anahitimisha rasmi leo safari ya kesi alizokuwa anakabiliana nazo kuanzia Juni 2,2021 alipopandishwa kizimbani mara ya kwanza.
Wakili wa sabaya,Moses Mahuna mbele ya waandishi wa habari ameeleza kwamba kuanzia sasa,sabaya ni mtu huru na kwa mujibu wa mahakama yenyewe, hana rekodi yotote ya uhalifu na hana shauri lingine lolote katika chombo chochote cha sheria,na kumfanya kumalizana rasmi na Mahakama.


Lengai Ole Sabaya akikumbatiana kwa furaha na mama yake mara baada ya Mahakama ya Rufaa Nchini kutupa rufaa ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini, (DPP)

ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili wameshinda kesi ya rufaa waliyokatiwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, (DPP) baada ya Mahakama ya Rufaa  kusema hakuna ushahidi wa ujambazi wa kutumia silaha wala kundi uliothibitishwa kwenye kesi ya msingi.


Aidha mahakama hiyo ya juu nchini, ilibatilisha na kufuta maelezo ya awali na mwenendo wa Shahidi wa pili, Noman Jasin huku ikieleza kuwa Mahakama Kuu Kanda ya  Arusha ilikosea kubatilisha na kufuta maelezo ya awali na mwenendo  wa shauri lote na kuwaachia huru warufani wote baada ya kubaini shahidi huyo hakuhojiwa na mawakili wa wajibu rufaa wa pili na watatu katika kesi ya msingi.

Uamuzi huo wa majaji watatu wa mahakama ya rufaa wakiongozwa na jaji, Jacobs Mwambegele, Ignas Kitus na Leila Mgonya umesomwa leo Novemba 17,2023 kwa saa 1.10 na Naibu Msajili wa Mahakama Rufaa Nchini, Abeesiza Kalegeya kwenye mahakama kuu kanda ya Arusha.


Kalegeya ambaye awali alipanga kusoma uamuzi huo saa tatu kamili asubuhi lakini alikuja kuusoma saa 7.30 mchana alieleza kuwa mahakama ilifikia uamuzi wa kutupilia mbali rufaa hiyo baada ya kupitia hoja za pande zote na kujiridhisha kuwa kulikuwa na mapungufu ya kisheria.

"Mahakama imeona hata ilipobadilishwa kutoka kutoka unyanganyi wa kutumia silaha kwenda kwenye kosa la kundi makosa hayo hayakuthibitishwa  na haingefaa kwa sababu makosa yote yana adhabu zinazolingana,"alieleza Kalegeya wakati akitangaza kutupa rufaa hiyo na kuongeza.

"Hii rufaa imetupwa, Maamuzi yaliyotolewa na  mahakama kuu Arusha (mahakama ya rufaa ya kwanza) hayawezi kubatilika na rufaa hii inatupiliwa mbali,".

Hivyo kwa uamuzi huo wajibu rufaa, Sabaya  ambaye alikuwa mahakamani hapo na wenzake Silvester Nyegu na Danie Mbura wanaendelea kuwa huru.


Awali Naibu Msajili huyo wa Mahakama ya Rufaa Nchini alirejea hukumu iliyotolewa Mei 6, 2023 na Mahakama kuu Arusha iliyotokana na kesi ya jinai 


https://draft.blogger.com/blog/post/edit/496674253964308653/4916419568569067909 

https://habaritanzaniagracemacha.blogspot.com/2022/05/sabaya-na-wenzake-waachiwa-huru.html



MAHAKAMA ya Rufaa imekwama kusoma uamuzi wake kwenye kesi inayowakabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili baada washitakiwa Sylivester Nyegu na Daniel Mbura, kutokuwa mahakamani.


Aidha mahakama hiyo imepanga kutoa uamuzi huo ijumaa Novemba 17, mwaka huu majira ya saa tatu asubuhi huku ikiagiza washtakiwa wote kuwepo mahakamani .

Akiongea na waandishi wa habari nje ya mahakama wakili wa wajibu rufaa hao, Mosses Mahuna alisema kuwa wajibu maombi hao walikuwa nje ya mkoa wa Arusha na walikuwa njiani kurejea.

Rufaa hii inahusu hukumu ya Mei 8, 2022, iliyomwachia huru Sabaya, Nyegu, na Mbura, ambayo Jamhuri kupitia DPP inapinga.


Leo, Sabaya pekee ndiye aliyekuwapo mahakamani, na kesi imeahirishwa hadi Novemba 17 kutokana na kutokuwepo kwa wenzake.


Awali Novemba 1,2023 mabishano makali ya kisheria yaliibuka baina ya mawakili wa pande zote  wakati wa usiilizaji wa rufaa hiyo mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, wakiingozwa  Jaji Jacobs Mwambegele, Ignas Kitusi, na Leila Mgonya.


Mkuu wa jopo la mawakili wa DPP, Chivanenda Luwongo, aliiomba mahakama kufanyia marekebisho hoja zao ambazo awali zilikuwa saba na kubaki tatu  kudai kuwa Mahakama Kuu ya Arusha ilikosea kuwaachia huru wajibu rufaa.

Wakili huyo aliieleza kuwa Mahakama kuu kanda ya Arusha ambayo ni  ya Rufaa ya kwanza ilikosea kusema kwenye kesi ya msingi iliyowakuta Sabaya na wenzake na hatia kesi yao haina mashiko kwa sababu shahidi namba mbili hakuulizwa maswali na wajibu rufaa namba mbili na tatu na kufuta ushahidi wao wote na akawaachia huru.

Sababu nyingine ni mahakama hiyo kusema usikilizwaji wa awali wa kesi ulikosewa kwa sababu wajibu rufaa wawili (Nyegu na Mbura),kuwa kuna vitu hawakusomewa wakati waliandika kwa maandishi kuwa wametimiza.

 Alitaja sababu ya tatu kuwa ni Jamhuri haikuweza kuthibitisha kesi yao pasipo kuacha shaka,jambo ambalo alisema kesi hiyo ilitibitishwa pasipo kuacha shaka yoyote ambapo upande huo wa jamhuri walirejea ushahidi na vielelezo mbalimbali vilivyowasilishwa kwenye kesi ya msingi.

Aidha wakili huyo alieleza mahakama kuwa ushahidi wa shahidi wa pili wa jamhuri siyo ushahidi pekee uliowatia hatiani wajibu rufani hao na kuwa ushahidi wa mashahidi wengine na vielelezo viliwatia hatiani washitakiwa hao.

Mawakili wa mleta rufaa walisema kwenye kesi ya msingi walithibitisha mashitaka yote bila kuacha shaka,upande wa wajibu rufaa walisema kwamba hawakufanya hivyo huku wakidai kuwa walishindwa kueleza hata eneo lilipo duka,wakati hati ya amshtaka ikisema duka lipo mtaa wa bondeni baadhi ya mashahidi wakidai duka hilo lipo Soko Kuu.

Hata hivyo mawakili wa wajibu rufaa Mosses Mahuna, alipinga hoja hizo akirejea ushahidi uliotolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Mahuna alisema hukumu ya rufaa ya kwanza ilikuwa sahihi na hakukuwa na mapungufu huku akidai  kuwa utaratibu wa hoja za awali haukufuatwa ipasavyo na kuhoji ssbabu zilizowafanya upande wa Jamhuri kushindwa kufanyia marekebisho hati ya mashitaka.


Hukumu inayopingwa ilitolewa Mei 6, 2022, na Jaji Sedekia Kisanya wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, ambaye aliwaachia huru Sabaya na wenzake wawili waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na mahakama ya hakimu mkazi Arusha Oktoba 15, 2021.

 


MAWAKILI wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake... wameenda mahakama ya rufani nchini wakiiomba kufanyia marejeo uamuzi mdogo na mwenendo wa kesi ya rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) dhidi ya wateja wao.


Hatua hiyo imesababisha shauri hilo la rufaa namba 155/2022 lililokuwa likiendelea kwenye mahakama Kuu ya Kanda ya Arusha mbele ya Jaji Fatma Maghimbi kusimama mpaka mahakama hiyo ya juu itakaposikiliza na kutoa uamuzi.

Rufaa hiyo dhidi ya Sabaya na wenzake watano inapinga hukumu iliyotolewa Juni 10, 2022 na Hakimu Mkazi Patricia Kisinda kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, ambapo aliwaachia huru Sabaya na wenzake sita katika kesi ya uhujumu uchumi namba 27/2021.

Wakili wa Serikali waandamizi Felix Kwetukia aliieleza mahakama hiyo leo Jumatatu Februari 20, 2023 kuwa Februari 3, 2023 walipokea maombi ya kufanya mapitio yaliyoandaliwa Januari 27, 2023 yanayoomba Mahakama ya Rufani ifanye mapitio ya mwenendo wa rufaa hiyo na uamuzi mdogo uliotolewa Desemba 14, 2022.

"Kwa msingi huo kwa kuwa kuna maombi ya mapitio ni rai yetu rufaa hii isubiri kwa muda ikisibiri usikilizaji na uamuzi wa maombi ya upande wa wajibu rufaa yaliyopelekwa katika mahakama ya rufani," amesema Wakili wa Serikali Mwandamizi,  Kwetukia.

Kwa upande wake wakili wa wajibu rufani, Mosses Mahuna ameieleza mahakama hiyo kuwa anakubaliana na maombi ya upande wa jamhuri na kuwa hawana nyongeza.

Hata hivyo ameieleza mahakama hiyo kuwa mpaka sasa hawajui maombi hayo yamesajiliwa kwa namba ngapi ingawa wanataarifa kuwa kuwa yameshasajiliwa.

Jaji Maghimbi amesema kuwa shauri hilo litasismama mpaka maombi hayo ya marejeo  yaliyofunguliwa mahakama ya rufani yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Wajibu rufaa kwenye shauri hilo ni Sabaya, Enock Mnkeni, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Ambapo wajibu rufaa waliokuwa mahakamani hapo ni Sabaya na Mnkeni ambapo wajibu rufaa wawili Aweyo na Nyegu wakiwalilishwa na mawakili wao huku mawakili hao wakieleza mahakamani hapo hawana taarifa za wajibu rufaani, Msuya na Macha.

Upande wa jamhuri unawakilishwa na mawakili wa serikali waandamizi, Kwetukia, Timotheo Mmari na Hebel Kihaka huku upande wa wajibu rufaa ukiwakilishwa na mawakili Mahuna, Fauzia Mustapha, Fridolin Bwemelo na Sylvster Kahunduka.


Awali, Desemba 14, 2022 Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilitupilia mbali pingamizi lililokuwa limewasilishwa mahakamani hapo na mawakili wa mjibu rufani wa kwanza,  Sabaya.


Aidha mahakama hiyo ilitupilia mbali hoja ya rufaa hiyo kukatwa nje ya muda pamoja na ufafanuzi kuhusu mrufani wa tatu, Watson Mwahomanhe ambaye awali upande wa wajibu rufaa uliibua hoja ya kutokuonekana mahakamani.

Jaji Maghimbi alisema kuwa rufaa hiyo iliwasilishwa ndani ya wakati na kwa mujibu wa sheria ambapo siku 45 za kukata zinaanza kuhesabiwa pale nakala za mwenendo wa kesi na uamuzi unakuwa umetolewa.

Alisema anakubaliana na hoja ya wakili wa serikali mwandamizi Patrick Mwita ambaye wakati akijibu hoja za pingamizi hilo la awali aliileza mahakama kuwa siku 45 za kukata rufaa zinaanza kuhesabiwa baada ya kukabidhiwa nakala ya mwenendo wa kesi na hukumu.

Kuhusu hoja ya pili iliyotolewa na Mahuna akidai kuwa notisi ya nia ya kukata rufaa inatofautiana na maombi ya rufaa, Jaji alisema anakubaliana na hoja ya wakili wa serikali mwandamizi Patrick Mwita kuwa baada ya kupata mwenendo wa shauri na hukumu ndipo unaweza kuamua nani umkatie rufaa.





 




HUKUMU ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita inatarajiwa kutolewa leo Juni 10,2022.



Hukumu ya shauri hilo linalofuatiliwa na watu wengi ilikuwa itolewe Mei 31, 2022 lakini ilishindikana baada ya hakimu aliyesikiliza shauri shauri hilo, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Patricia Kisinda kuwa nje ya kituo cha kazi.


Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Fadhil Mbelwa aliahirisha shauri hilo namba 27/2021 mpaka  Juni 10, mwaka huu kwa ajili ya kusomwa hukumu.



"Shauri limekuja kwa ajili ya hukumu na liko kwa Hakimu Mkazi Mwandamizi, Patricia Kisinda lakini siku ya leo amepangiwa majukumu mengine ya kikazi nje ya ofisi hataweza kutoa hukumu leo hadi Juni 10, 2022," alisema Hakimu Mbelwa wakati akiahirisha kesi hiyo.



Washitakiwa wengine kwenye kwenye kesi hiyo ni pamoja  na Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.


Mawakili wa Jamhuri waliokuwa mahakamani ni pamoja na Mawakili wa Serikali waandamizi, Janeth Sekule, Felix Kwetukia, Wakili wa Serikali Neema Mbwana na Mwendesha Mashitaka wa Takukuru, Jacopiyo Richard.


Kwa upande  wa utetezi walikuwa  Mawakili Mosses Mahuna, Fridolin Bwemelo, Edmund Ngemela na Sylvester Kahunduka ambao wanawatetea washitakiwa sita isipokuwa Mwahomange ambaye anajitetea mwenyewe mahakamani hapo.



Awali kwenye shauri hilo, Sabaya peke yake anakabiliwa na makosa matatu ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka alipokuwa mkuu wa Wilaya ya Hai huku washtakiwa wengine sita  wakikabiliwa na makosa mengine mawili ya kuongoza genge la uhalifu na utakatishaji fedha.


Makosa hayo wanadaiwa waliyafanya  Januari 21, 2021 katika eneo la kwa Mrombo jijini Arusha ambapo katika kosa la kwanza linalowakabili washtakiwa wote saba ni kuongoza genge la uhalifu, la pili linalomkabili Sabaya peke yake ni kujihusisha na vitendo vya rushwa na la tatu linalomkabili Sabaya pia ni kujihusisha na vitendo vya rushwa ambapo anadaiwa kuchukua Sh 90 milioni.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa kosa la nne linalomkabili Sabaya mwenyewe ni matumizi mabaya ya madaraka huku kosa la tano linalowakabili wote saba likiwa ni utakatishaji fedha ambapo wanadaiwa kupata Shilingi 90 milioni huku wakijua kupokea  fedha hizo zao la kosa la vitendo vya rushwa.

Katika kesi hiyo inayovuta hisia za wengi upande wa Jamhuri ulileta jumla ya mashahidi 13 na vielelezo 12 ambapo awali waliahidi kuleta mashahidi 20 mahakamani hapo huku upande wa utetezi ukileta mashahidi nane akiwemo mke wa Sabaya, Jesca Nassary na washitakiwa wote saba kila mmoja akijitetea.
 
Mashahidi Mashahidi wa Jamhuri ni pamoja na Mkurugenzi msaidizi anayesimamia utawala wizara ya fedha na mipango, Renatus Msangira, (45), Kaimu meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Arusha, Kayobyo Majogolo(41).

Wengine ni mwangalizi  wa geti (mlinzi) na mfanyakazi kwa Mrosso, Adanbest Peter Marandu, (61), pamoja na Philemon Tilatwa Kazidila,(64),  Juma Nuhu, (28) na Mfanyakazi wa Benki ya CRDB, Geofrey Nko.

Mashahidi wengine wa Jamhuri ni afisa uchunguzi wa kielektroniki kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini,(TAKUKURU), Johnson Kisaka, Meneja Benki ya CRDB tawi la Kwa Mromboo, Mary Mayoka Kimasa, (40) na mmiliki wa Mrosso Injector pump, Francis Mrosso.

Wengine ni dalali wa magari kutokea jijini Dar es Salaam, Sabri Abdallah Sharif ,(36), Meneja wa ulinzi na ushirika wa vyombo vya ulinzi na usalama Vodacom PLC,Tegeta DSM James Lisao Wawenje, (39) na Afisa uchunguzi wa TAKUKURU, Ramadhani Rajab Juma, (39).

 Washitakiwa hao wamerudishwa mahabusu kwenye gereza na Kisongo kwani mashitaka yanayowakabili hayana dhamana.

 



 

 

 


HUKUMU ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita imeshindwa kutolewa baada ya hakimu aliyesikiliza shauri shauri hilo, Patricia Kisinda kuwa nje ya kituo cha kazi.


Hukumu ya shauri hilo linalofuatiliwa na watu wengi ilikuwa itolewe leo Mei 31,2022  ambapo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Fadhil Mbelwa ameeleza kuwa haitaweza kusomwa kwani hakimu aliyesikiliza shauri hilo hayupo.


Amesema kuwa kutokana na hakimu Mkazi Mwandamizi, Kisinda anayesikiliza shauri hilo namba 27/2021 kuwa kwenye kazi nje ya ofisi, shauri hilo litarudi mahakamani hapo Juni 10, mwaka huu kwa ajili ya kusomwa hukumu.



"Shauri limekuja kwa ajili ya hukumu na liko kwa Hakimu Mkazi Mwandamizi, Patricia Kisinda lakini siku ya leo amepangiwa majukumu mengine ya kikazi nje ya ofisi hataweza kutoa hukumu leo hadi Juni 10, 2022," amesema Hakimu Mbelwa wakati akiahirisha kesi hiyo.




Washitakiwa wengine kwenye kwenye kesi hiyo ni pamoja  na Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.


Mawakili wa Jamhuri waliokuwa mahakamani ni pamoja na Mawakili wa Serikali waandamizi, Janeth Sekule, Felix Kwetukia, Wakili wa Serikali Neema Mbwana na Mwendesha Mashitaka wa Takukuru, Jacopiyo Richard.


Kwa upande  wa utetezi walikuwa  Mawakili Mosses Mahuna, Fridolin Bwemelo, Edmund Ngemela na Sylvester Kahunduka ambao wanawatetea washitakiwa sita isipokuwa Mwahomange ambaye anajitetea mwenyewe mahakamani hapo.




Awali kwenye shauri hilo, Sabaya peke yake anakabiliwa na makosa matatu ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka alipokuwa mkuu wa Wilaya ya Hai huku washtakiwa wengine sita  wakikabiliwa na makosa mengine mawili ya kuongoza genge la uhalifu na utakatishaji fedha.


Makosa hayo wanadaiwa waliyafanya  Januari 21, 2021 katika eneo la kwa Mrombo jijini Arusha ambapo katika kosa la kwanza linalowakabili washtakiwa wote saba ni kuongoza genge la uhalifu, la pili linalomkabili Sabaya peke yake ni kujihusisha na vitendo vya rushwa na la tatu linalomkabili Sabaya pia ni kujihusisha na vitendo vya rushwa ambapo anadaiwa kuchukua Sh 90 milioni.


Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa kosa la nne linalomkabili Sabaya mwenyewe ni matumizi mabaya ya madaraka huku kosa la tano linalowakabili wote saba likiwa ni utakatishaji fedha ambapo wanadaiwa kupata Shilingi 90 milioni huku wakijua kupokea  fedha hizo zao la kosa la vitendo vya rushwa.

Katika kesi hiyo inayovuta hisia za wengi upande wa Jamhuri ulileta jumla ya mashahidi 13 na vielelezo 12 ambapo awali waliahidi kuleta mashahidi 20 mahakamani hapo huku upande wa utetezi ukileta mashahidi nane akiwemo mke wa Sabaya, Jesca Nassary na washitakiwa wote saba kila mmoja akijitetea.
 
Mashahidi Mashahidi wa Jamhuri ni pamoja na Mkurugenzi msaidizi anayesimamia utawala wizara ya fedha na mipango, Renatus Msangira, (45), Kaimu meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Arusha, Kayobyo Majogolo(41).

Wengine ni mwangalizi  wa geti (mlinzi) na mfanyakazi kwa Mrosso, Adanbest Peter Marandu, (61), pamoja na Philemon Tilatwa Kazidila,(64),  Juma Nuhu, (28) na Mfanyakazi wa Benki ya CRDB, Geofrey Nko.

Mashahidi wengine wa Jamhuri ni afisa uchunguzi wa kielektroniki kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini,(TAKUKURU), Johnson Kisaka, Meneja Benki ya CRDB tawi la Kwa Mromboo, Mary Mayoka Kimasa, (40) na mmiliki wa Mrosso Injector pump, Francis Mrosso.

Wengine ni dalali wa magari kutokea jijini Dar es Salaam, Sabri Abdallah Sharif ,(36), Meneja wa ulinzi na ushirika wa vyombo vya ulinzi na usalama Vodacom PLC,Tegeta DSM James Lisao Wawenje, (39) na Afisa uchunguzi wa TAKUKURU, Ramadhani Rajab Juma, (39).

 Washitakiwa hao wamerudishwa mahabusu kwenye gereza na Kisongo kwani mashitaka yanayowakabili hayana dhamana.

 



 

 

 


UAMUZI wa mahakama Kuu Kanda ya Arusha kubatilisha hukumu ya miaka 30 jela na kumwachia huru aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili imepokewa kwa hisia tofauti.

 

Wakati ndugu jamaa na marafiki wa Sabaya, Sylvester Nyegu na Daniel Bura wakifurahi, wananchi wengine wamesikitishwa na uamuzi huo wakidai kuwa Mahakama Kuu haukutenda haki kwa watu walioumizwa na tukio hilo ambao walijitokeza na kutoa ushahidi mahakamani.

 

Aidha, Diwani wa Sombetini, Bakari Msangi, (CCM) ambaye ni miongoni mwa walalamikaji kwenye shauri hilo amesema uamuzi huo si wa haki kwani alipigwa, kuumizwa na kuibiwa fedha zake jambo aliloeleza kusikitishwa na kuumizwa na uamuzi huo.

 

Uamuzi huo umetolewa na  Jaji, Sedekia Kisanya wa mahakama Kuu Kanda ya Musoma aliyesikiliza shauri hilo la rufaa namba 129/2021 kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha .

 

“Mimi nilipigwa nikanyang’anywa fedha zangu, nilifika mbele ya mahakama nikaeleza ukweli wa kile kilichotokea mahakama ikajiridhisha kuwa tukio lilikuwa ni kweli. Huu uamuzi wa kumwachia huru si wa haki ila Mungu anajua tulieleza ukweli mahakamani,” amee leza Msangi.

 

Kwa upande wake Wakili wa Serikali Mwandamizi, Felix Kwetukia alisema kuwa wanaenda kupitia hukumu hiyo ili wajue hatua watakazochukua.

 

UAMUZI

 

Akitoa uamuzi huo, Jaji Kisanya alisema kuwa baada ya kupitia hoja za pande mbili mahakama imejiridhisha kuna mapungufu ya kisheria kwenye mwenendo wa shauri hilo hivyo akaamuru kuachiliwa huru kwa waleta rufaa hao.

 

“Kwa upande wangu naona haya mapungufu ya mkanganyiko kwenye ushahidi zile ground nyingine nakubaliana na maombi ya waleta  rufaa, nabatilisha mwenendo na hukumu zilizotolewa dhidi ya waleta rufaa,” alisema Jaji huyo akitoa amri na kuongeza.

 

“ Naamuru waleta rufani waachiliwe huru,  waachiliwe huru isipokuwa kama wana mashauri mengine yasiyo na dhamana waendelee nayo,” .

 

Jaji Kisanya alitoa uamuzi huo kunzia majira ya saa 6 mchana ambapo upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili wa serikali mwandamizi, Felix Kwetukia huku upande wa waleta rufaa ukiwakilishwa na mawakili Moses Mahuna, Faudhia Mustafa, Sylvester Kahunduka, Gabriel Rwahira, Edmund Ngemela na Fridolin Gwemelo.

 

HALI ILIVYOKUWA KABLA YA UAMUZI

 

Awali watu waliungia kwenye chumba cha mahakama kuanzia majira ya saa 2 asubuhi ambapo majira ya saa 4 asubuhi warufani waliingia kwenye chumba cha mahakama tayari kupoke uamuzi.

 

Hata hivyo majira ya saa 4:25 karani wa mahakama alitoa taarifa kuwa uamuzi huo utatolewa saa 6 mchana hivyo wanausalama waliokuwa mahakamani hapo wakawatakz watu wote kutoka nje.

 

Ilipofika majira ya saz 5.30 asubuhi shauri hilo liliitwa hivyo watu wakaingia kwenyE chumba cha mahakama pamoja na warufani.

 

SABABU ZA KUFUTA HUKUMU

 

Awali akichambua hoja za mawakili wa pande zote kabla ya kutoa uamuzi Jaji Kisanya alisema kuwa  alipitia hoja 14 za mawakili wa waleta rufaa ambapo waleta rufaa walishitakiwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi kwa makosa matatu ya unyanganyi wa kutumia silaha.

 

Alieleza kuwa upande wa Jamhuri ulipeleka mashahidi 11 na vielelzo nane kuthibitisha mashitaka hayo ambapo upande wa utetezi walipeleka mashahidi sita.

 

 

“Mrufani wa kwanza (Sabaya) alieleza alienda kwenye duka la shahidi wa kwanza (Mohamed Saad) Soko kuu na alikubali kwamba kuna watu wawili aliowakamata kwenye hilo duka na kuwapeleka kituo cha polisi lakini hawakuwapiga wala kuiba kwenye hilo duka,” alieleza Jaji Kisanya akieleza mambo aliyoyasoma kwenye mwenendo wa shauri la msingi.

 

“Washitakiwa wawili walikana hawakuwa kwenye tukio Sylivster alisema alikuwa Bomangombe na mshitakiwa wa tatu  alisema alikuwa Shamsi na akakana majina yake kuwa yeye ni Daniel Mbura na si Daniel Bura  na akaleta vielelezo viwili,”.

 

 Jaji Kisanya alisema kuwa baada ya mahakama kusikiliza ushahidi wa pande zote mahakama iliridhika kuwa kulikuwa na kosa la  kuwa unyanganyi wa kutumia silaha lakini kwa kosa la kwanza hakuona unyanganyi wa kutumia silaha lakini akaona ushahidi uliotolewa aliona ulithibitisha kosa dogo la unyanganyi wa kutumia nguvu na vile aliona likifanywa na mtu zaidi ya moja akaona walifanya unyang’anyi wa makundi (gang robbery). 

 

Waleta rufaa wote walihukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa kosa la kwanza na hayo mengine na yanaonekana yataenda kwa pamoja hivyo wakaamua kuja mahakama kuu kupinga.

 

Jaji Kisanya alieleza mawakili wa waleta rufaa walileta hoja 14 mahakama hapo wakipinga mahakama kuwatia hatiani wateja wao  huku upande wa Jamhuri ukijibu hoja hizo.

 

 

“Hii ikiwa ni rufaa ya kwanza inakuwa katika mfumo wa kusikiliza mahakama inawajibu wa kusoma ushahidi wote na kuufanyia 'evaluation', kuanalysis kabla ya kutokea uamuzi. Masuala ya wajibu wa kuthibitisha kwenye masuala ya jinai pasipo kuacha shaka yoyote isipokuwa kama sheria imeelekeza vinginevyo huo wajibu unakuwa ni wa jamhuri na hauwezi kwenda kwa mshitakiwa,” alieleza jaji Kisanya na kuongeza.

 

“Katika kusikiliza rufaa hii naanza na sababu ya tatu na 11 juu ya uhalali wa mwenendo katika kusikiliza shauri hilo. Mawakili wa waleta rufaa walianisha maeneo mbalimbali ambayo wanaona mwenendo wa mahakama uliosikiliza shauri hilo haukuwa sawasawa,”.

 

“Kielekezo namba nne, tano na nane ilielezwa kwamba vielelezo vilipokelewa wakati kulikuwa na pingamizi mbele yake na kielelezo namba saba na nane ambavyo vilikuwa ni vya kutengeneza  lakini vilipokelewa wakati vilikuwa havihusiani na shauri hilo kwa sababu vinaonyesha duka la shahidi namba moja lipo eneo tofauti na duka lilipo,”.

 

“Upande wa Jamhuri walisema vielelezo hivyo viko sahihi na akarejea mashauri mbalimbali yaliyowahi kufanywa na mahakama za juu.Mahakama ikisoma sheria inaona mamlaka ya kuamua upokeaji wa ushahidi iko kwenye mahakama inayosikiliza shauri hivyo mahakama ya juu haiwezi kupoke malalamiko hayo kama hayakutolewa kwenye mahakama iliyokuwa inasikiliza,”.

 

 “Vielelezo hivyo vilipokelewa na haivikupingwa kwenye mahakama iliyosikilizwa hivyo pingamizi hilo haliwezi kuwekwa kwenye mahakama ya sasa itakuwa inakiuka taratibu kwani mahakama iliyopokea ndiyo ilikuwa ina mamlaka ya kusikiliza pingamizi hilo,”.

 

Jaji Kisanya aliendelea kusoma uamuzi hu kwa kusema mrufani namba tatu, (Daniel Mbura) hakuwa eneo la tukio wanadai kuwa mleta rufaa namba tatu alitoa taarifa ya kuegemea kuwa hakuwa eneo la tukio kama sheria inavyosema wanadai ilikuwa ni wajibu wa upande wa jamhuri kuonyesha kuwa mrufani wa watatu kuonyesha kuwa alikuwa.

 

Alisema kuwa utetezi huo  ulizingatiwa na mahakama ila mshitakiwa namba tatu alishindwa kuita mashahidi aliokuwa nao siku ya tukio na huo utetezi ulipaswa kufanyiwa  kwa kiwango cha mizania huku wakirejea mashauri mbalimbali ya mahakama za juu.

 

Jaji Kisanya alieleza kuwa upande wa Jamhuri walisema kuwa mrufani huyo wa tatu alitambuliwa kuwa alikuwa eneo la tukio hivyo mahakama ilikuwa sahihi kumtia hatiani. 

 

 

“Mrufani namba tatu (Mbura) alitoa taarifa ya kutokuwa eneo la tukio na mahakama ikaangalia huo utetezi lakini haikuzingatia huo ushahidi kwa sababu mrufaa namba tatu hakuita mwanafamia au mpangaji mwenzake aweze kuthibitisha hakuwepo,” alisema Jaji Kisanya akirejea hoja za mawakili wa Jamhuri.

 

Alisema kuwa anakubalia na hoja za wakili wa waleta rufaa, Magafu kuwa mshitakiwa hana wajibu wa kuthibitisha  hakuwa eneo la tukio ilijuwa ni wajibu wa Jamhuri kumthibitisha vinginevyo hata hivyo mahakama iliridhika kwamba huyu mrufani namba tatu alitambuliwa na shahidi namba sita (Msangi).

 

Kwa kuwa mahakama iliyosikiliza shauri yenyewe ilirithika kuwa mrufani wa tatu alikuwa eneo la tukio na alitambuliwa hivyo mahakama ilikuwa sahihi kumweka hatiani.

 

Jaji Kisanya anaeleza Mahakama ya hakimu mkazi Arusha iliyosikiliza shauri ilishindwa kuona hapakuwa na gwaride la utambulisho kwa mrufani namba moja na mbili ila upande wa jamhuri walidai kuwa mashahidi walikuwa  wanawafahamu warufani namba moja na mbili hata kabla ya tukio.

 

Anasema dhumuni la kufanya utambuzi ni kumwezesha shahidi kumtambua mtu aliyefanyia jambo au kumvamia ambaye hakuwa anamfahamu kabla ya tukio.

 

"Mshitakiwa namba moja na mbili walikuwa na urafiki na shahidi namba sita, shahidi namba tano alieleza alikuwa anawafahamu mrufani namba moja kabla ya tukio hivyo hapakuwa ba sababu ya kufanya gwaride la utambulisho," anaeleza jaji Kisanya akichambua hoja za mawakili na kuongeza.

 

... Shahidi namba mbili na tatu , kwenye hukumu ya mahakama iliyosikiliza shauri hilo ushahidi wao haukuzingatiwa hivyo hawakuathiri kwenye uamuzi,".

 

"Mshitajiwa namba moja na mbili hawakukamatwa wala hawakuhojiwa kama sheria inavyotaka ila kama walifikishwa mahakama basi walikamatwa na hili la kutohojiwa la upande wa jamhuri walieleza kuwa mshitakiwa namba moja alieleza kuwa alikataa kuandika maelezo,".

 

"Upelelezi wa jinai unaanza baada ya kosa kuripotiwa kituo cha polisi hivyo kosa namba mbili na tatu hayakuripotiwa lakini yalipelekwa mahakamani kinyume cha sheria.

36

"Shahidi namba sita anaonekana kuwa mtu wa kwanza kuripoti tukio lililotendeka kwenye duka la shahidi namba moja na shahidi namba mbili na namba nne walikuwa wamehojiwa na shahidi namba saba ambaye alipowahoji akaona hawakuwa wamefanya uhujumu uchumi kama mrufani namba moja alivyokuwa ameripoti hivyo hoja hiyo haina msingi,".

 

"Mahakama ilikosea kuiruhusu jamhuri kufanya marekebisho kwenye hati ya mashitaka wakati walikuwa wameshafunga ushahidi wao. Walidai kuwa hayo mapungufu yanaenda kwenye msingi wa kesi,".  

 

 

"Mrufani namba mbili Mbura na tatu, Nyegu walitaka mashahidi wa jamhuri waitwe tena jambo ambalo halikufanyika lakini jamhuri walieleza kuwa hawakuathirika kwa kuwa marekebisho yalikuwa yanahusu mabadiliko ya majina ya mrufani namba moja Sabaya na mawakili wa warufani walikuwa mahakamani na hawakuomba kuitwa kwa mashahidi hao,".

 

"Ni ukweli kuwa hati ya mashitaka inaweza kubadilishwa wakati wowote shauri likiendelea pale jamhuri inapoona inafaa ilimradi uamuzi haujatoka. Kwenye shauri hilo lilibadilishwa wakati shahidi wa kwanza akiwa amemaliza kutoa ushahidi wa msingi hivyo hiyo hoja haina msingi,".

 

Jaji Kisanya anaeleza kuwa hapakuwa na ubishi kuwa mrufani namba mbili na namba tatu waliulizwa kama watahitaji mashahidi waitwe anaweza kuwa mmoja au wote ili kutoa ushahidi upya au baadhi ya maeneo na anayepaswa kufanya hivyo ni mshitakiwa mwenyewe kwenye kumbukumbu haionyesha kama mawakili wa utetezi waliitaka mahakama iwaite mashahidi hao upya.

 

"Hakuna ubishi kuwa mabadiliko yaliyofanywa kwenye hati ya mashitaka kutoka Sayaba kuja Sabaya nakubaliana na wakili wa serikali kuwa mshitakiwa namba mbili na tatu hawakuathiriwa na mabadiliko hayo na waliwakilishwa na mawakili waliooaswa kuiongoza mahakama kufanya hayo.

 



MAHAKAMA ya hakimu Mkazi Arusha imepanga kutoa uamuzi kwenye kesi ya uhujumu Uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita Mei 31, mwaka huu.

 

Aidha, Mshitakiwa wa tatu, Watson Mwahomange ambaye kwenye shauri hilo alikuwa akijitetea mwenyewe ameshindwa kufika mahakamani hapo kutokana na kuugua akiwa mahabusu huku mahakama ikimpa siku moja  kusaini hoja za majumuisho zilizowasilishwa kwa maandishi.

 

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Patricia Kisinda anayesikiliza shauri hilo namba 27/2021 alipanga tarehe hiyo leo Machi 31, 2022 baada ya mawakili wa pande zote kuwa wamewasilisha hoja zao za majumuisho kwa maandishi na mshitakiwa, Watson ambaye ametakiwa kuzisaini na kuzirejesha mahakamani kesho.

 

“Mshitakiwa wa tatu, (Watson Mwahomange) ambaye hajasaini hoja zake za majumuisho nampa siku moja kufanya hivyo kesho (leo) awe amesaini na kuzileta mahakamani, kesi itatajwa April 13 kwa sababu washitakiwa wako mahabusu hukumu Mei 31, 2022,” amesema Hakimu Kisinda akiahirisha shauri hilo.

 

Awali, askari magereza, Inspekta Ramadhan Misanga ameieleza mahakama hiyo kuwa mshitakiwa wa tatu, Mwahomange anaumwa hajafika mahakamni hapo huku akieleza kuwa wana  hoja zake za majumuisho za maandishi ambazo hazijasiniwa hivyo akaomba apewe muda ili ampelekee gerezani akazisaini.

 

“Mheshimiwa hakimu taarifa za mahabusu namba tatu Watson Mwahomange tunazo sisi maafisa wa magereza kwamba leo hatujaja ane tumemuacha gerezani akiwa anaumwa,” amesema Inspekta Misanga na kuongeza.

 

…Mimi asubuhi niliitwa na mganga mkuu wa gereza akanipa taarifa za kuumwa kwake amenipa cheti alichoandika yeye daktari ili nije nacho mahakamani ili maneno ninayotoa yabarikiwe ili yawe na uthibitisho wa daktari,”.

 

Hakimu Kisinda akaomba hicho cheti akakiangalia kisha Inspekta Misanga akaendelea kuieleza mahakama hiyo kuwa ana hoja za majumuisho za maandishi za mshitakiwa huyo ambazo hazijasainiwa.

 

“ Kwa hiyo tunaiomba mahakama, itupe muda baada ya hapa tukamsainishe ili ziweze kuletwa mahakamani,” alieleza Inspekta Misanga.

 

Kwa upande wa Jamhuri Wakili wa Serikali Mwandamizi, Felix Kwetukia alieleza mahakamani hapo kuwa waliwasilisha hoja zao za majumuisho jana asubuhi huku wakili wa utetezi Faudhia   Mustafa akisema hoja zao waliziwasilisha Machi 30, mwaka huu.

 

Kwenye shauri hilo linalovuta hisia za wengi Sabaya pamoja na  Enock Nkeni, (41) maarufu  Dikdik, Watson Mwahomange, (27) maarufu Mamimungu,John Aweyo, maarufu  Mike One, Silvester  Nyengu, (26) maarufu Kicheche, Jackson Macha, (29) na Nathan Msuya, (31) wanakabiliwa na mashitaka ya kuongoza genge la uhalifu, kujihusisha na vitendo vya rushwa, utakatishaji fedha na matumizi mabaya ya madaraka.


Awali, ilidaiwa mahakama hapo kuwa washitakiwa hao   waliyafanya makosa hayo  Januari 21, 2021 katika eneo la kwa Mrombo jijini Arusha.

 

Kwenye shauri hilo, Sabaya peke yake anakabiliwa na makosa matatu ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka alipokuwa mkuu wa Wilaya ya Hai huku washtakiwa wengine wote wanakabiliwa na makosa mengine mawili ya kuongoza genge la uhalifu na utakatishaji fedha.

 

Makosa hayo wanadaiwa waliyafanya  Januari 21, 2021 katika eneo la kwa Mrombo jijini Arusha ambapo katika kosa la kwanza linalowakabili washtakiwa wote saba ni kuongoza genge la uhalifu, la pili linalomkabili Sabaya peke yake ni kujihusisha na vitendo vya rushwa na la tatu linalomkabili Sabaya pia ni kujihusisha na vitendo vya rushwa ambapo anadaiwa kuchukua Sh90 milioni.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa kosa la nne linalomkabili Sabaya mwenyewe ni matumizi mabaya ya madaraka huku kosa la tano linalowakabili wote saba likiwa ni utakatishaji fedha ambapo wanadaiwa kupata Shilingi 90 milioni huku wakijua kupokea  fedha hizo zao la kosa la vitendo vya rushwa.

 

 

Katika kesi hiyo inayovuta hisia za wengi upande wa Jamhuri ulileta jumla ya mashahidi 13 na vielelezo 12 ambapo awali waliahidi kuleta mashahidi 20 mahakamani hapo huku upande wa utetezi ukileta mashahidi nane akiwemo mke wa Sabaya, Jesca Nassary na washitakiwa wote saba kila mmoja akijitetea ingawa awali waliahidi kuleta zaidi ya mashahidi 10.

 

Mashahidi Mashahidi wa Jamhuri ni pamoja na Mkurugenzi msaidizi anayesimamia utawala wizara ya fedha na mipango, Renatus Msangira, (45), Kaimu meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Arusha, Kayobyo Majogolo(41).

 

Wengine ni mwangalizi  wa geti (mlinzi) na mfanyakazi kwa Mrosso,Adanbest Peter Marandu(61), pamoja na Philemon Tilatwa Kazidila,(64),  Juma Nuhu, (28) na Mfanyakazi wa Benki ya CRDB, Geofrey Nko.

 

Mashahidi wengine wa Jamhuri, afisa uchunguzi wa kielektroniki kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini,(TAKUKURU) Johnson Kisaka, Meneja Benki ya CRDB tawi la Kwa Mromboo, Mary Mayoka Kimasa(40) na mmiliki wa Moroso Injector pump, Frances Mrosso.

 

Wengine ni dalali wa magari kutokea jijini Dar es Salaam, Sabri Abdallah Sharif ,(36), Meneja wa ulinzi na ushirika wa vyombo vya ulinzi na usalama Vodacom PLc,Tegeta DSM James Lisao Wawenje(39) na Afisa uchunguzi wa TAKUKURU, Ramadhani Rajab Juma, (39)