KAMISHINA wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Profesa, Dos Santos Silayo.
KAMISHINA wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu, (TFS), Profesa, Dos Santos Silayo ametoa ofa ya siku nne kwa washiriki wa maonyesho ya kwanza ya utalii ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, (EAC) kutembelea bure hifadhi wanazozisimamia.
Ameyasema hayo leo, Oktoba 11,2021 wakati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi kufunga maonyesho hayo kwenye viwanja vya TGT jijini Arusha.
Amesema ofa hiyo ya siku nne kuanzia Oktoba 11 mpaka 16, mwaka huu ambapo ofa hiyo inahusisha kutolipia kiingilio.
"TFS una eneo kubwa lililohifadhiwa kwa ajili ya utalii wa Ikolojia kwani linatoa fursa kutembea na kuona misitu mbalimbali na mandhari nzuri iliyopo," anasema Profesa, Silayo na kuongeza.
.... Kwa wale walioshiriki maonyesho tumetoa fursa kwao ya kutembelea bure misitu yetu iliyopo karibu ya Duluti ambayo ipo pamoja na ziwa Duluti ambapo watajionea samaki wa aina mbalimbali na kuvinjari ndani ya ziwa hilo kwa kutumia boti ndogo...
...Kule wataona maeneo yanayotumiwa na watu wa imani mbalimbali kwa ajili ya kuabudu. Pia tuna msitu wetu wa Meru huu ni wa kupanda, una mandhari nzuri kuna maporomoko ya maji kuna maeneo maji yanaporomoka mita 70 wasanii wamekuwa wakifika na kurekodi nyimbo zao hapo sasa tunataka wananchi wafike pale wajionee na kufurahia mandhari hiyo,".
Profesa Silayo amesema wageni hao wanatarajia kuwapeleka kuona misitu mingine iliyopo mkoa wa Pwani wilayani Bagamoyo eneo la Mji Mkongwe ambaoo kuna masalia ya majengo yaliyotumika kwenye utawala za kikoloni na eneo la Kaole lenye majengo ya kale.
"Wataona maji maalum yanayotumika pale kwenye kisima ambacho hakikauki muda wote kinatoa maji ya baraka wanavyoamini na naamini wageni wetu watafurahia kuona mambo hayo....
....Pia wataona muingiliano wa misitu ya kale na bahari kwa maana ya misitu ya mikoko na misitu ya zamani na kwenye msitu wetu wa asili wa Pugu wa Kazi Mzumbe msitu wenye banoanuwai nyingi za mimea na Pugu yenyewe ni mti ambao haupatikani mahali popote duniani zaidi ya pale ....
....Pia ndege wanaopatikana pale ni mahsusi pia kuna panzi wenye rangi ya bendera ya Taifa pia watapata fursa ya kuendesha boti kwenye bwawa la asili lililopo ndani ya eneo hilo ambalo halikauki muda wote,".
Maonyesho ya utalii ya EAC yaliwahusiha washiriki zaidi ya 100 kutoka mataifa mbalimbali ambapo walitumia fursa hiyo kutangaza utalii wa maeneo tofauti ambapo maonyesho yanayofuata yanatarajiwa kufanyika nchini Burundi.
0 Comments:
Post a Comment