Serikali ya imethibitisha kuwa kimbunga ‘Hidaya’ kinaendelea kusogea kuelekea maeneo ya  pwani ingawa kasi ya kimbunga hicho inapungua.


Msemaji mkuu wa serikali ya Tanzania, Mobhare Matinyi amesema hayo wakati akiongea na vyombo vya habari.


“Mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa baharini inaonesha uwezekano wa kasi ya kimbunga hicho kupungua zaidi ndani ya saa 12 zijazo, jambo ambalo ni taarifa njema huku kikiendelea kusogelea pwani ya Tanzania. Kimbunga hiki kinatarajiwa kuendelea kuwepo hadi tarehe 5 Mei na kitaendelea kupungua nguvu kwa mujibu wa vipimo vya wataalamu wetu.” Alifafanua.


Msemaji huyo mkuu wa serikali ameeleza zaidi kuwa “Uwepo wa kimbunga Hidaya karibu na pwani ya nchi yetu kunatarajiwa kutawala na kuathiri mfumo wa hali ya hewa hapa nchini ikiwa ni pamoja na kusababisha vipindi vya mvua kubwa na upepo mkali katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani ikiwa na pamoja na kisiwa cha Mafia, Dar es Salaam, pamoja na mikoa ya Tanga, Morogoro na visiwa vya Unguja na Pemba. Tayari vipindi vya mvua na upepo vimeanza katika mikoa ya Pwani na Lindi”.


Amewataka wakazi wa maeneo yaliyotajwa kuathirika na kimbunga ‘Hidaya’ kuendelea kufuatilia taarifa za mamlaka ya hali ya hewa na maelekezo ya taasisi za serikali na pia kuchukua tahadhari.


Mara ya mwisho Tanzania Bara kupigwa kimbunga kikali ilikuwa mwaka 1952 wakati huo ikiitwa Tanganyika na kuathiri eneo la mkoa wa Lindi. Kabla ya hapo kimbunga kingine kikali kiliipiga Zanzibar mwaka 1872.


Katika miaka ya karibuni kulitokea kimbunga Jobo mwaka 2021 ambacho hakikuwa na athari kubwa zaidi ya mvua za wastani na upepo. Hali kama hiyo ilitokea mwaka 2019 wakati wa kimbunga Kenneth huko mkoani Mtwara lakini kilikuwa na madhara makubwa nchini msumbiji na Malawi.



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi na watendaji wa Serikali waondoe ukiritimba kwenye suala la upatikanaji wa habari ili kuwawezesha wanahabari kupata taarifa sahihi na kufanya kazi zao kwa ufanisi.


 


“Viongozi na Watendaji wa Serikali na Mashirika zingatieni Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa ya Mwaka 2016 na ondoeni ukiritimba katika suala la upatikanaji wa habari ili wanahabari wawezeshwe kupata taarifa sahihi na wafanye kazi zao kwa ufanisi wa hali ya juu,” amesema.


 


Ametoa wito huo leo (Ijumaa, Mei 3, 2024) wakati akizungumza na wanahabari na wadau wengine kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.


 


Kuhusu upatikanaji wa habari sahihi, Waziri Mkuu pia amewataka wakuu wa taasisi waweke mazingira mazuri kwa waandishi wa habari ili kuwawezesha kuzingatia weledi na kurahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu kwa ngazi zote za jamii.


 


Aidha, amevitaka vyombo vya habari viunde madawati maalum yatakayoratibu masuala ya mabadiliko ya tabianchi. “Madawati hayo yatafute fedha kwa ajili ya kutekeleza mpango wa mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu kuandika kitaalamu masuala ya mabadiliko ya tabianchi na madhara yake kwa jamii na Taifa. Suala hili likamilike ili katika maadhimisho ya siku hii mwakani, iwepo taarifa ya utekelezaji,” amesisitiza.


 


Kuhusu habari za uchunguzi, Waziri Mkuu amesema uandishi wa habari hizo unahitaji rasilimali fedha za kutosha ili kutoa mafunzo na kuifanya kazi yenyewe. “Niwaombe wadau wote muhimu wakiwemo taasisi, asasi za kiraia na mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi washirikiane na vyombo vya habari katika kufanikisha utafiti na uandishi wa habari za uchunguzi na kuvisaidia vyombo vya habari kukua kitaaluma na kiuchumi.”


 


Akigusia changamoto zinazowakabili waandishi wa habari wanawake, Waziri Mkuu amezitaka Wizara za Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na ile ya Maendeleo ya Jamii Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, zihakikishe zinakamilisha awamu ya pili ya Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (NPA-VAWC II). “Hatua hiyo itasaidia ushughulikiaji wa changamoto za mashambulio ya kimwili kwa waandishi wa habari wanawake,” amesema.


 


Ametumia fursa hiyo kuwahimiza wanahabari wote wazingatie uzalendo, weledi na maadili ya taaluma ya uandishi kwa kutoa mchango chanya kwa jamii kwani wasipofanya hivyo tasnia hiyo inaweza kuwa chanzo cha kufifisha maendeleo na hata kuhatarisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.


 


Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema vyombo vya habari vinayo nafasi kubwa ya kuitangaza nchi pamoja na kuijengea taswira chanya kimataifa na kuwapomgeza wanahabari kwa kazi wanayoifanya ya kuuhabarisha umma.


 


“Vyombo vya habari vimekuwa na mchango mkubwa katika kuhamasisha uwekezaji, kutangaza vivutio vya utalii na kuchangia katika kuinua uchumi wa Taifa letu. Kwa niaba ya Serikali na wananchi wote wa Tanzania ninavipongeza sana vyombo vyetu ya habari kwa kazi kubwa inayofanywa katika kuutumikia umma.”


 


Akisisitiza umuhimu wa vyombo hivyo, Waziri Mkuu amesema vina mchango mkubwa wa kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika shughuli na utekelezaji wa mipango ya Serikali pamoja na kampeni muhimu za kitaifa.


 


“Waandishi wa habari wana nguvu ya kuongeza sauti kwa jamii kuhusu mmomonyoko wa maadili, athari za kimazingira, kufichua rushwa na uzembe na kuunga mkono masuluhisho yatakayochochea maendeleo endelevu na ustahimilivu katika maeneo muhimu.


 


Kaulimbiu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani kwa mwaka 2024 inasema: “Uandishi wa Habari na Changamoto za Mabadiliko ya Tabianchi.”


 


Mapema, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, alisema hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini imeimarika ikilinganishwa na ilivyokuwa awali.


 


“Hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini inaendedelea kuimarika. Bado hatujafika tunakotaka kwenda lakini kwa hakika hatupo tulipokuwa jana. Tumefika hapa kutokana na juhudi za Mheshimiwa Rais, tumetekeleza 4R za Mheshimiwa Rais na ndiyo maana tuko hapa tulipo,” alisema.


 


Mkutano huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo mabalozi wa Marekani, Uswisi, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa, UNESCO, Asasi za Kiraia, Wawakilishi kutoka Muungano wa Klabu 28 za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Jukwaa la Wahariri na wanavyuo.



MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha imefuta rufaa iliyokuwa ikimkabili Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake watano baada ya Mkurugenzi  wa Mashtaka Nchini (DPP) Silvester Mwakitalu, kuwasilisha  ombi la kuiondoa Rufaa hiyo namba 155/2022 .

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Sabaya akitoka mahakamani akiwa ameambatana na wakili wake, Moses Mahuna mara 





Rufaa hiyo ilikatwa na Jamhuri baada ya Sabaya na wenzake kushinda kesi  ya Uhujumu uchumi namba 27/2021 katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha ambapo uamuzi huo ulitolewa na Hakimu Mkazi, Dkt Patricia Kisinda.
Rufaa hiyo ilipangwa kusikilizwa  Mfululizo  Mahakama kuu Kanda ya Arusha kuanzia Aprili 29, 2024 mpaka Mei 03, 2024 mbele  ya  Jaji, Salma Maghimbi wa Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam aliyekuwa akisikiliza rufaa hiyo.
Akiwasilisha nia Ya kuliondoa shauri hilo mbele ya Jaji Salma,  wakili wa serikali Akisa mhando aliieleza mahakama hiyo upande wa Jamhuri hauna nia ya kuendelea na rufaa hiyo dhidi ya Sabaya
 “Mhe Jaji, Shauri hili limekuja kwa ajili ya kusikilizwa ,hata hivyo mrufani (Jamhuri) imewasilisha ombi chini ya kifungu cha sheria No.386 (1) cha sheria ya muenendo wa makosa ya jinai marejeo ya mwaka 2022,ombi letu ni kwamba Jamhuri haina nia ya kuendelea na Rufaa hii dhidi ya Sabaya na wenzake,hivyo tunaomba kuiondoa hapa mahakamani," Mhando aliomba mahakamani japo.
Upande wa wajibu rufaa hawakuwa na pingamizi juu ya ombi hilo hivyo Jaji Maghimbi alitoa uamuzi kwamba rufaa hiyo imeondolewa mahakamani rasmi.
Kufuatia uamuzi huo, sabaya anakuwa hana shauri lolote linalomkabili mahakamani na anahitimisha rasmi leo safari ya kesi alizokuwa anakabiliana nazo kuanzia Juni 2,2021 alipopandishwa kizimbani mara ya kwanza.
Wakili wa sabaya,Moses Mahuna mbele ya waandishi wa habari ameeleza kwamba kuanzia sasa,sabaya ni mtu huru na kwa mujibu wa mahakama yenyewe, hana rekodi yotote ya uhalifu na hana shauri lingine lolote katika chombo chochote cha sheria,na kumfanya kumalizana rasmi na Mahakama.






























 

 Government Unveils Strategies to Address Menace of Rogue Wildlife


The government, through the Ministry of Natural Resources and Tourism, has outlined various strategies to address the challenge of rogue and destructive wildlife in various parts of the country, including the Mbarali District.


 This includes the implementation of the National Strategy for Resolving Human-Wildlife Conflicts (2020-2024), the Elephant Management and Conservation Strategy (2023-2033), and the Wildlife Corridor Rescue Action Plan (2022-2026).



Speaking at the Parliament in Dodoma on May 2, 2024, the Minister of Natural Resources and Tourism, Angellah Kairuki, highlighted steps taken to combat the menace of rogue wildlife, particularly elephants. 


These measures include conducting patrols to control rogue and destructive wildlife, establishing conservation officer stations, and providing training in elephant-friendly techniques for 1,626 instructors from 28 districts facing significant challenges from rogue wildlife.


Furthermore, the ministry has been providing education to communities, with 2,053 individuals from five villages in the Mbarali District receiving training on dealing with elephant encounters. Additionally, 41 instructors from these villages have been trained in elephant-friendly techniques in collaboration with conservation stakeholders.


To enhance community involvement in conservation efforts, the ministry has trained 882 Village Game Scouts on conservation and techniques for dealing with rogue wildlife. Collaboration with research institutes has resulted in fitting 157 elephants with GPS satellite collars across five ecological systems to monitor their movements and mitigate conflicts.


The minister emphasized the government's commitment to continuing efforts to address rogue wildlife, including the allocation of funds for purchasing three helicopters to facilitate the relocation of elephants back to protected areas. In Mbarali District, three elephants are scheduled to be fitted with collars on May 8 and 9, 2024, for monitoring purposes.


In conclusion, Minister Kairuki assured Members of Parliament that the Ministry of Natural Resources and Tourism will continue to acquire equipment and resources to effectively manage human-wildlife conflicts and safeguard both communities and wildlife.











Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa wafanyakazi wa SMZ wataongezewa posho ya shilingi 50,000 ya nauli ili kuleta ufanisi katika kazi na kurahisisha masuala ya usafiri kwa ajili ya nauli za kwenda kazini na kurudi nyumbani.



Amesema shilingi bilioni 34 zimetengwa na Serikali kwa ajili ya posho ya usafiri kwa watumishi wote wanaostahiki kulipwa posho.



Rais Dk.Mwinyi amesema hayo  katika sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi) zilizofanyika uwanja wa Gombani, Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 1 Mei 2024.


Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali imejipanga kutengeneza ajira 300,000 kwa wananchi wake  kwa mujibu wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025. 


Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu Serikali kupitia shughuli utekelezaji wa miradi ya maendeleo  ajira mpya zipatazo 187,651 zimepatikana  sawa na asilimia 104 ya lengo la ajira 180,000 kwa miaka mitatu iliyopita.


Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali imedhamiria kuhakikisha inaongeza fedha kwa ajili ya posho ya likizo , zikiwa  zimetengwa shilingi bilioni 2.5 katika bajeti mpya ya mwaka 2024/25.