NgÅ©gÄ© wa Thiong’o: Mwewe wa Fasihi ya Afrika Aliyeondoka Akiwa na Umri wa Miaka 87

 


NgÅ©gÄ© wa Thiong’o, mmoja wa waandishi mashuhuri wa fasihi ya kisasa ya Afrika, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 87. Kwa zaidi ya miongo sita, NgÅ©gÄ© alisimulia hadithi za mapambano ya ukombozi, udhalimu wa ukoloni, na matumaini ya Afrika huru. Alikuwa mwandishi, mwanafalsafa, na mtetezi shupavu wa lugha za Kiafrika, ambaye alikataa kufungwa na mipaka ya lugha, siasa, wala mateso ya kibinafsi.

Alizaliwa mwaka wa 1938 katika kijiji cha Kamiriithu karibu na Limuru, wakati Kenya bado ilikuwa chini ya utawala wa kikoloni wa Uingereza. Akiwa mtoto wa familia maskini ya wakulima, wazazi wake walifanya juhudi kubwa kumpeleka katika shule ya upili ya Alliance, ambapo aliibuka kuwa mwanafunzi mwenye ari na akili pevu.

Katika mahojiano moja ya baadaye, Ngũgĩ alikumbuka kwa uchungu:
"Niliporudi nyumbani kutoka Alliance nilikuta kijiji kimeharibiwa kabisa na utawala wa kikoloni."

Maisha yake yaliathiriwa sana na vuguvugu la Mau Mau. Kaka yake Gitogo alipigwa risasi mgongoni kwa kukataa amri ya askari wa Kikoloni – bila kujua, kwa sababu alikuwa kiziwi.

Mnamo 1959, Ngũgĩ alielekea Uganda kusomea katika Chuo Kikuu cha Makerere, ambapo aliandika riwaya yake ya kwanza, Weep Not, Child. Chinua Achebe, mwandishi wa Things Fall Apart, aliona uwezo mkubwa ndani yake na kumsaidia kuchapisha kitabu hicho nchini Uingereza.



"Achebe ndiye aliyeniweka kwenye ramani ya fasihi. Aliona kitu ambacho hata mimi sikuwa nimekiona," aliwahi kusema Ngũgĩ.

Lakini urafiki huo baadaye ulivunjika, hasa baada ya Ngũgĩ kumkosoa Achebe kwa kuendelea kuandika kwa Kiingereza.

"Kuna tofauti gani kati ya mwanasiasa anayesema Afrika haiwezi bila ubeberu na mwandishi anayesema Afrika haiwezi bila lugha za Ulaya?" aliuliza katika kitabu chake Decolonising the Mind.


Mwaka wa 1977, NgÅ©gÄ© alifanya uamuzi wa kubadili jina kutoka James Thiong’o NgÅ©gÄ© kuwa NgÅ©gÄ© wa Thiong’o – ishara ya kujikomboa kutoka kwa majina ya kikoloni. Mwaka huo pia alikamilisha Petals of Blood, riwaya ya mwisho kuandika kwa Kiingereza, iliyowakosoa vikali viongozi wa Kenya huru kwa kuwa mabwanyenye wa aina mpya.

Katika mwaka huo huo, alishiriki katika uandishi wa tamthilia Ngaahika Ndeenda (Nitaolewa Ninapotaka), ambayo ilipigwa marufuku na serikali. Hapo ndipo alikamatwa na kufungwa jela kwa mwaka mmoja bila mashitaka.

Lakini hata gerezani hakuvunjika moyo. Aliandika riwaya yake ya kwanza kwa Kikuyu, Caitaani Mutharaba-Ini (Ibilisi Msalabani), kwa kutumia karatasi ya chooni.
"Fasihi ni silaha. Na hata gerezani, bado nilikuwa na kalamu yangu," alisema baada ya kuachiliwa.

Ngũgĩ alilazimika kuingia uhamishoni, akiishi Uingereza na kisha Marekani, ambako alifundisha katika vyuo vikuu vya Yale, New York na California Irvine. Alikaa nje ya Kenya kwa miaka 22, hadi alipopokelewa kama shujaa mwaka wa 2004.



Lakini sherehe ya kurejea nyumbani iliharibiwa na shambulio la kikatili kwake na mkewe.
"Shambulio hilo halikuwa la kawaida. Lilikuwa la kisiasa," alisisitiza.

Pamoja na mafanikio yake, maisha ya NgÅ©gÄ© yaligubikwa na migogoro ya kifamilia. Mwanaye Mukoma wa NgÅ©gÄ© – pia mwandishi – alidai kuwa mama yake alikuwa akidhulumiwa na NgÅ©gÄ©.
"Baadhi ya kumbukumbu zangu za utotoni ni kwenda kumtembelea kwa nyanya yangu ambapo angetafuta hifadhi," aliandika Mukoma.

Ngũgĩ hakuwahi kujibu hadharani madai hayo.

Katika miaka yake ya mwisho, alikabiliwa na changamoto kubwa za kiafya: saratani ya kibofu, matatizo ya moyo na figo. Mwaka 2019, alipitia upasuaji wa moyo mara tatu. Alikuwa mpambanaji hadi mwisho – akishinda hata ugonjwa uliotabiriwa kumuua.

Alifariki dunia lakini ameacha urithi mkubwa wa kiakili, kijamii na kisiasa. Aliwahi kuandika:
"Lugha si tu chombo cha mawasiliano, bali pia ni hazina ya dunia ya watu."

Katika kumbukumbu yake, mwandishi Chimamanda Ngozi Adichie alisema:
"NgÅ©gÄ© alikuwa taa elekezi ya fasihi ya Afrika – dunia ya maneno imepoteza nuru."

NgÅ©gÄ© wa Thiong’o sasa ametoweka, lakini kazi zake – A Grain of Wheat, The River Between, Devil on the Cross, Matigari – na ndoto yake ya Afrika inayojieleza kwa sauti yake yenyewe, zitaendelea kuishi milele.

0 Comments:

Post a Comment