Kapinga Awaasa Kampuni za ETDCO na TCPM kusimamia Majukumu Yao Kwa Weledi



Dar es Salaam, 4 Januari 2024 - Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amekutana na Kampuni za kutengeneza Nguzo za Zege Tanzania (TCPM) na Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme (ETDCO), zinazohusiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Katika kikao hicho kilichofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam, Kapinga amewaasa kutekeleza miradi yao kwa weledi na kwa maslahi mapana ya nchi.

 Ameelekeza TCPM kuwa makini katika uchaguzi wa kampuni za ubia na kuzingatia sifa, na pia ameitaka ETDCO kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati na ubora miradi yote wanayotekeleza.

"Mnapoingia ubia na kampuni fulani, muwe makini na kuchagua wabia wenye uwezo wa kufanya kazi, kwa sababu hatuhitaji ubia wa wabia wasio na uwezo wa kifedha na kazi," alisema  Kapinga.

Fedha zitakazotolewa kwa ajili ya miradi inapaswa kutumika kwa tija na kuleta matokeo chanya. Naibu Waziri alisisitiza umuhimu wa utekelezaji wa ahadi zilizojitokeza katika makaratasi na kuzitaka kuzingatiwa kikamilifu.

Kikao hicho kilihudhuriwa na uongozi wa Kampuni ya TCPM na ETDCO, na Naibu Waziri alimalizia kwa picha ya pamoja na wawakilishi wa kampuni hizo.

0 Comments:

Post a Comment