HUKUMU RUFAA YA DPP DHIDI YA SABAYA SASA NOVEMBA 17



MAHAKAMA ya Rufaa imekwama kusoma uamuzi wake kwenye kesi inayowakabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili baada washitakiwa Sylivester Nyegu na Daniel Mbura, kutokuwa mahakamani.


Aidha mahakama hiyo imepanga kutoa uamuzi huo ijumaa Novemba 17, mwaka huu majira ya saa tatu asubuhi huku ikiagiza washtakiwa wote kuwepo mahakamani .

Akiongea na waandishi wa habari nje ya mahakama wakili wa wajibu rufaa hao, Mosses Mahuna alisema kuwa wajibu maombi hao walikuwa nje ya mkoa wa Arusha na walikuwa njiani kurejea.

Rufaa hii inahusu hukumu ya Mei 8, 2022, iliyomwachia huru Sabaya, Nyegu, na Mbura, ambayo Jamhuri kupitia DPP inapinga.


Leo, Sabaya pekee ndiye aliyekuwapo mahakamani, na kesi imeahirishwa hadi Novemba 17 kutokana na kutokuwepo kwa wenzake.


Awali Novemba 1,2023 mabishano makali ya kisheria yaliibuka baina ya mawakili wa pande zote  wakati wa usiilizaji wa rufaa hiyo mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, wakiingozwa  Jaji Jacobs Mwambegele, Ignas Kitusi, na Leila Mgonya.


Mkuu wa jopo la mawakili wa DPP, Chivanenda Luwongo, aliiomba mahakama kufanyia marekebisho hoja zao ambazo awali zilikuwa saba na kubaki tatu  kudai kuwa Mahakama Kuu ya Arusha ilikosea kuwaachia huru wajibu rufaa.

Wakili huyo aliieleza kuwa Mahakama kuu kanda ya Arusha ambayo ni  ya Rufaa ya kwanza ilikosea kusema kwenye kesi ya msingi iliyowakuta Sabaya na wenzake na hatia kesi yao haina mashiko kwa sababu shahidi namba mbili hakuulizwa maswali na wajibu rufaa namba mbili na tatu na kufuta ushahidi wao wote na akawaachia huru.

Sababu nyingine ni mahakama hiyo kusema usikilizwaji wa awali wa kesi ulikosewa kwa sababu wajibu rufaa wawili (Nyegu na Mbura),kuwa kuna vitu hawakusomewa wakati waliandika kwa maandishi kuwa wametimiza.

 Alitaja sababu ya tatu kuwa ni Jamhuri haikuweza kuthibitisha kesi yao pasipo kuacha shaka,jambo ambalo alisema kesi hiyo ilitibitishwa pasipo kuacha shaka yoyote ambapo upande huo wa jamhuri walirejea ushahidi na vielelezo mbalimbali vilivyowasilishwa kwenye kesi ya msingi.

Aidha wakili huyo alieleza mahakama kuwa ushahidi wa shahidi wa pili wa jamhuri siyo ushahidi pekee uliowatia hatiani wajibu rufani hao na kuwa ushahidi wa mashahidi wengine na vielelezo viliwatia hatiani washitakiwa hao.

Mawakili wa mleta rufaa walisema kwenye kesi ya msingi walithibitisha mashitaka yote bila kuacha shaka,upande wa wajibu rufaa walisema kwamba hawakufanya hivyo huku wakidai kuwa walishindwa kueleza hata eneo lilipo duka,wakati hati ya amshtaka ikisema duka lipo mtaa wa bondeni baadhi ya mashahidi wakidai duka hilo lipo Soko Kuu.

Hata hivyo mawakili wa wajibu rufaa Mosses Mahuna, alipinga hoja hizo akirejea ushahidi uliotolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Mahuna alisema hukumu ya rufaa ya kwanza ilikuwa sahihi na hakukuwa na mapungufu huku akidai  kuwa utaratibu wa hoja za awali haukufuatwa ipasavyo na kuhoji ssbabu zilizowafanya upande wa Jamhuri kushindwa kufanyia marekebisho hati ya mashitaka.


Hukumu inayopingwa ilitolewa Mei 6, 2022, na Jaji Sedekia Kisanya wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, ambaye aliwaachia huru Sabaya na wenzake wawili waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na mahakama ya hakimu mkazi Arusha Oktoba 15, 2021.

0 Comments:

Post a Comment