eGA YAWASILISHA MFANO WA RATIBA YA VIONGOZI KIDIGITALI

 

Na Mwandishi wetu – Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati wa kikao cha kupokea mfano wa ratiba ya viongozi katika mfumo wa kielektroniki kutoka kwa Mamlaka ya Serikali Mtando (eGA) kilichofanyika katika Ukumbi wa ofisi hiyo Tarehe 21 Novemba 2023 Jijini Dodoma.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amepokea wasilisho la mfano wa ratiba ya viongozi katika mfumo wa kielektroniki kutoka kwa Mamlaka ya Serikali  Mtandao (eGA).


Mkurugenzi wa Tafiti kutoka  Mamlaka ya Serikali Mtando (eGA) Dkt. Jaha Mvulla  (aliyesimama) akiwasilisha Mfano wa ratiba ya viongozi ya kielektroniki kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi pamoja na wataalam kilichofanyika katika Ukumbi wa ofisi hiyo Tarehe 21 Novemba 2023 Jijini Dodoma.


Mfumo huo wa kielektroniki utasaidia  viongozi kufahamu ratiba zao za utekelezaji wa majukumu ya kila siku katika mfumo ikiwa ni pamoja na kusoma taarifa, kutoa maoni na maelekezo katika eneo la kazi na  uratibu wa shughuli za ndani za  wizara husika. 

Baadhi ya Wataalam kutoka Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) wakisikiliza kikao  akilichofanyika kwa lengo la kuwasilisha Mfano wa ratiba ya viongozi ya kielektroniki kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi kilichofanyika katika Ukumbi wa ofisi hiyo Tarehe 21 Novemba 2023 Jijini Dodoma.



Imeelezwa kuwa mfumo huo utawezesha viongozi  kujipanga katika majukumu ya kila siku na kuondoa mgongano wa ratiba zao  katika ngazi zote.



Ofisi ya Waziri Mkuu iliandaa kikao kazi na wataalam kutoka Mamlaka ya Serikali Mtandao eGA kwa ajili ya kuwezesha  moduli hii ya kalenda ndani ya  mfumo wa DASHBOARD ambapo  mpango kazi huo unaonesha muda ambao eGA  watatumia kukamilisha kalenda hiyo pamoja na  muda wa kuanza kutumika rasmi.


(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

0 Comments:

Post a Comment