SAMIA ATAKA PAPU ITUMIE NDEGE ZA AFRIKA

 RAIS ,  ametaka jengo la Umoja wa Posta Afrika, (PAPU Tower)  litumike kujengeana uwezo baina ya nchi wananchama wa PAPU kwa kubadilishana uzoefu kuongeza ubunifu na kufanya mageuzi ya kiutendaji.

Rais,  Samia Suluhu Hassan akikata utepe kufungua Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU Tower) lililopo Philips Jijini Arusha. Wengine ni Katibu Mkuu wa PAPU, Dkt. Sifundo Moyo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye .


Aidha, Ametaka PAPU  kuangalia uwezekano wa mashirika ya posta barani Afrika kukuza utendaji ikiwa pamoja na kuongeza wigo wa usafirishaji wa vifurushi kwa kutumia mashirika ya ndege ya ndani ya Afrika. 


Pia amezindua stika mpya za posta yenye picha ya jengo hilo ambazo zitatumika kwenye nchi za Tanzania, Algeria, Nigeria, Misri, Morocco, Senegal na Zimbabwe.



Rais Samia amesema hayo leo Septemba 2,2023 wakati akizindua jengo hilo refu kuliko yote jijini Arusha hwli inayolifanya kuwa kivutio kikubwa kutokana na muonekano wake.


Samia amesema kuwa  mageuzi yanayofanyika kwa nchi wanachama yapo katika viwango tofauti vya mafanikio ambapo nchi nyingine zimepoteza matumaini ya huduma za posta.


“Jengo hili lifanye uwiano wa maendeleo ya posta zetu Afrika sote tuwiane tuweze kutoa huduma zinazoweza kutegemewa na watu wetu. Mkiweza kufanya hivyo mtachangia katika ukuaji wa uchumi wa kidijitali na kuifanya umoja wa Afrika kujivunia uwepo wa posta Afrika,” amesema Samia.


Amesema kuwa  huduma za posta zikiimarishwa kutakuwa na safari za ndege za ndani ya bara la Afrika kwa ajili ya kusafirisha vifurushi kutoka nchi moja kwenda nyingine hivyo kuondokana na adha ya kulazimika kwenda bara lingine ili uweze kufika kwenye baadhi ya nchi zilizopo Afrika.


Samia amesema huduma za posta katika nchi nyingi zimepoteza mvuto licha ya umuhimu wake, hivyo ni kazi ya umoja huo kuhakikisha ufanisi wa huduma za posta unaongezeka na kuendana na mabadiliko ya sasa ya kidijitali ili kuwavutia watu wengi kutumia.

“PAPU iwezeshe mashirika ya Posta Afrika kwa kutumia mashirika yetu ya ndege ya ndani badala ya kutumia mashirika ya nje ya Afrika na hii itatulazimisha tuwe na muunganiko ndani ya bara. Posta itulazimishe ndege zetu zisafiri ndani ya Afrika kupeleka vifurushi,” amesema.

Rais Samia amesema kuwa kuna haja ya PAPU kuwa na mfumo mmoja wa biashara mtandao kupitia maduka ya mtandao yanayofanya biashara.

“Ni matarajio yangu kwa kufanya hivi mtakuwa mmefanikiwa kufikia maono ya umoja wa posta duniani kupitia mradi wa wa E-commerce ndani ya Afrika," amesema Rais, Samia na kuongeza.

....Sina shaka Umoja wa Posta Afrika unaweza kuleta mageuzi makubwa kwa kuzingatia mahitaji ya sasa ya bara letu, kama likiplay role (ilichangia) ya kuleta uhuru na sasa inaweza ku play role ya kuleta mabadiliko ya kidijitali katika huduma za posta.”


PAPU Iinaundwa na nchi 45 za Afrika ambapo Rais Samia ameshauri nchi tisa zilizobaki kijiunga na umoja huo ili kizidisha mshikamano zaidi.


Nchi zilizohudhuria Mkutano mkuu wa 41 wa PAPU uliofanyika Agosti 29 na 30, 2023 ni pamoja na nchi za Angola, Algeria, Benin, Botswana, Burkina Faso, Burundi, Congo DRC, Cote D’Ivoire, Egypt, Ethiopia, Ghana, Kenya, Liberia, Madagascar, Malawi, Mali, Morocco, Mozambique, Namibia, Nigeria, Senegal, South Afrika, Uganda, Zimbabwe, Eswatini, Tunisia, Cameroon na Tanzania

0 Comments:

Post a Comment