YAJUE MAMBO YA POSTA YALIYOMKOSHA SAMIA


RAIS, Samia Suluhu Hassan akimsikiliza akimsikiliza Postamasta Mkuu,  Macrice Mbodo akimweleza juu ya  huduma mbalimbali zinazotolewa na Posta 



RAIS, Samia Suluhu Hassan, ameelezea kuridhishwa na maboresho na mabadiliko ya kiteknolojia yaliyofanywa na shirika la posta nchini  lkenye matumizi ya teknolojia katika utoaji wa huduma za posta na kubuni huduma mbadala.


Ameyasema hayo leo Septemba 2, 2023 wakati wa funguzi wa Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika, (PAPU Tower) lililopo eneo la Philips Jijini Arusha.

 

"Wakati nazungushwa kwenye jengo hili nilitokea upande wa posta Tanzania na kweli nimeona mabadilko  yaliyoendelea," amesema Rais Samia na kuongeza.

.... Nimekuwa najiuliza kabla sijaona hivi kweli posta katika dunia ya leo ina nafasi kweli lakini nilipoona mabadiliko yanayotokea posta ina nafasi muhimu sana katiba mabadiliko ya dunia ya leo,".
Rais, Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Postamasta Mkuu Macrice  Mbodo wakati akimulezea kuhusu Mashine ya ATM ambayo mteja anaweza kujihudumia mwenyewe katika huduma za posta.

Rais Samia amesema kuwa katika hatua nyingine Tanzania imetengeneza mfumo wa  anwani za makazi ambapo mwaka jana 2022 serikali iliendesha operesheni ya mfumo wa anwani za makazi uliotekelezwa nchi nzima.

" Ukipita Tanzania kila nyumba ina namba yake na mitaa imepewa majina kwa hiyo ni rahisi kuwafikia wananchi. Katika zoezi lile anwani 12.7 miloni zilikusanywa na kuiwezesha Tanzania kufanya sensa ya watu ma makazi kwa mafanikio makubwa," amesema Rais Samia na kuongeza.

....Anuani hizo zilizokusanywa ziliiwezesha Tanzania kuanzisha mfumo wa Taifa wa kidigitali (NaPA) ambao hupunguza gharama za muda wa kutoa na kupokea huduma katika sekta zote na baadhi ya taasisi zimeanza kuutumia mfumo huo katika kutoa huduma,".

"Tumeanzisha vituo vya  kutoa huduma mahali pamoja (one stop center) huduma zinazopatikana ni pamoja na huduma za uhamiaji, utoaji hati za kusafiria, mafao ya ajira utapata taarifa zote, Msajili wa Makampuni, (BRELA) na Mamlaka ya Mapato nchini, (TRA) unapata huduma zao ndani ya jengo moja la posta,".

"Hii imesaidia kupunguza gharama za uendeshaji kwa sababu taasisi hisi zingepawa kuwa na ofisi zao kwenye ngazi ya wilaya na kata lakini kwa sababu posta ziko maeneo mbalimbali nchini imetupunguzia gharama ya kujenga majengo ya taasisi hizo,".

"Katika kutekeleza mpango wetu wa Tanzania Kidigitali tuliolenga kuongeza matumizi ya huduma za kidigitali na kujenga jukwaa la kuendesha biashara za kimtandao na kuongeza watoa huduma za posta na vifurushi wa sekta binafsi lengo huduma ziwe za haraka zaidi,".

Jengo hilo la ghorofa 17 linamilikiwa kwa ubia ambapo PAPU  asilimia 60 na Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Mawasiliano,(TCRA) kwa asilimia 40 ambapo ujenzi wake umegharimu Sh54.8 bilioni. 




0 Comments:

Post a Comment