MWENYEKITI WA HALMASHAURI ABURUZWA MAHAKAMANI AKIDAIWA KUMKISHIFU KIGOGO MSTAAFU SERIKALINI



MWENYEKITI wa halmashauri ya Monduli, Isaac Joseph Copriano,(45) amepanda mahakamani kujitetea kwenye kesi anayodaiwa kumkashifu na kumtusi aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro, Erasto Sanare.


Sanare ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM) mkoani Arusha anaomba kulipwa fidia ya shilingi milioni 200  kwa madhara aliyopata kutokana na maneno ya kashfa anayodai yalitolewa na Isaac dhidi yake.

Shauri hilo la madai namba 23/2022  linasikilizwa na hakimu mkazi, Aisha Ndossy wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha ambapo Sanare anawakilishwa na mawakili,  Kapimpiti Mgalula na Judith Reuben huku Isaac akiwakilishwa na mawakili Peres Parpai, Sendeu Nicolas na Yonas Masiaya.

Isaac anadaiwa kutoa maneno hayo Novemba 7,2022 akiwa Sinoni wilayani Monduli akiwa na watu wengine pamoja na waandishi wa habari ambapo anadaiwa kusema "ndugu yangu Sanare amejiongezea eka moja na pointi kwenye eneo ambalo hajapewa..huu ni wizi  imekuwa mambo ya kujirudiarudia sana kwa kiongozi huyu,".


Akitoa utetezi  wake  Agosti 31,2023,  Isaac ameieleza mahakama kuwa hajui kama Sanare aliwahi kuwa kiongozi zaidi anamfahamu kama mwananchi wa kawaida.

Akiongozwa na mawakili wake, mwenyekiti huyo wa halmashauri ya wilaya ya Monduli amesama kuwa akiwa kwenye eneo la mgogoro linalomilikiwa na taasisi ya Nanina ambayo Sanare ni mkurugenzi wake alitoa maagizo kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo aiandikie barua taasisi hiyo isitishe kufanya maendeleo yoyote kwenye eneo hilo.

Amedai kuwa alifikia uamuzi huo baada ya yeye na  timu aliyokuwa nayo ambao walielekezwa na aliyekuwa Mkuu wa wilaya hiyo, Frank Mwaisumbe kupima eneo hilo kujiridhisha kuwa taasisi ya Nanina imejiongezea eneo kama malalamiko ya wananchi na diwani wa eneo hilo, Nelson Lowassa.

"Siku hiyo hapakuwa na wananchi ni wataalam, eneo la mgogoro upande mmoja eneo la Nanina na upande mwingine ni eneo la halmashauri," amesema Isaac na kuongeza

....Sikuwa na chombo cha habari kwenye eneo hilo kwani ili kitambulike lazima awe amesajiliwa. Mlalamikaji kwa sasa ni mwananchi wa kawaida sijui kama ni kiongozi wa Mila," 

Hata hivyo Isaac akihojiwa na wakili Judith amesema hapakuwa na mwananchi wa eneo hilo wakati walipoenda kulipima wala hakuna mwananchi aliyefika mahakamani hapo kutoa ushahidi juu ya malalamiko hayo.

Mawakili wa Isaac walisema kuwa wamekamilisha ushahidi wao ambapo wameleta mashahidi watatu akiwemo diwani wa kata ya Engutoto na Afisa ardhi mteule wilaya ya monduli, Waziri Juma Hatibu 

 Hakimu mkazi, Ndossi ameahirisha shauri hilo mpaka septemba 15, 2023 majira ya saa 3 asubuhi kwa ajili ya kutoa uamuzi ambapo amewaagiza mawakili wa pande zote kuwasilisha hoja za majumuisho Septemba 13, 2023.


Awali akiongozwa na wakili wake Parpai, Osaac aliieleza mahakama kuwa mbali ya uenyekiti wa halmashauri lakini pia ni mkandarasi.

Akaeleza kuwa majukumu yake kama mwenyekiti wa halmashauri ni kusimamia baraza la madiwani , kukagua wa shughuli za maendeleo na kusikiliza kero za wananchi 

Isaac akaeleza kuwa eneo walilompa Nanona lilikuwa na ekari 10 hivyo baada ya kumpa Nanina ekari tano zilibaki tano ni za halmashauri ya Monduli. 

Ameendelea kuieleza mahakama hiyo kuwa mnamo novemba 7,2022 majira ya saa tatu asubuhi aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Monduli, Frank Mwaisumba alimuita ofisini kwake na akamuagiza afuatilie kero ya mgogoro wa ardhi.

" Nilipofika ofisini kwa DC ofisini nikawakuta wataalam wa ardhi na taasisi nyingine TAKUKURU na polisi. DC wa wakati huo alinieleza kero aliyosema ni ya muda mrefu tukajiridhishe juu ya kero ya eneo tuliyoipa taasisi ya Nanina iliyopo Sinoni kata ya Engutoto," ameeleza Isaac na kuongeza.

...Tuliondoka kwenda eneo linalolalamikiwa nikiongozana na watu Hao tukafika kwenye eneo hilo tukakuta Kuna maeneo yamewekwa uzio na lingine limejengwa kisima," 

"Tulipofika tulihakiki eneo alilopewa Nanina je limeingia eneo lingine tukiwa na wataalam tukakuta limeingia eneo ambalo hatukuwapa,".

"Mkurugenzi wa Nanina hakuwepo walati upimaji ulifanyika. Baada ya kupima nikatoa maelekezo DED amuandikia barua Mkurugenzi wa Nanina asitishe maendelezo mpaka baraza  tutakapokaa kuangalia,".

Isaac akaendelea kujitetea mahakamani hapo kuwa 
"Niseme sijamchafua Sanare nilikuwa naelekeza watu wowote wenye ardhi Monduli asijiongezee ardhi bila kufuata utaratibu akijiongezea huo ni wizi," amesema Isaac na kuongeza

...Sikutaja jina la mtu ila nilielekeza kwa watumishi kuwa kitendo hiki mtu akifanya huo ni wizi...Nikitembelea miradi nikikuta kuna uzembe sementi au vifaa huwa nasema  huu upotevu ni wizi. Wizi ni pale mtu anapochukua kitu ambacho hakupewa,".





AKIHOJIWA NA WAKILI JUDITH ANAYEMWAKILISHA MLETA MAOMBI

WAKILI; Tarehe 7/11/  2022 ulienda kwenye eneo la migogoro 
SHAHIDI; ni kweli 
WAKILI; Kuna sehemu umesema wewe ulikuwa mwenyekiti wa halmashauri 
SHAHIDI; Sijui 
WAKILI; Lile eneo la mgogoro mlilotembelea lilikuwa la nani?
SHAHIDI; Kwenye mpaka kati ya Sanare na halmashauri 
WAKILI; Ulisema mlienda kama timu baada ya pale kuna ripoti yoyote iliyoandaliwa kuonyesha kuwa kweli huyu mtu amejiongezea ekari moja na point 
Shahidi; Hakuna  ripoti ilitolewa 
Wakili;  hapa mahakamani umeitoa 
Shahidi; Kimya  baada ya muda kimya ...sijaitoa
Wakili; Umesema kulikuwa na malalamiko mengi ya wananchi 
Shahidi; kweli 
Wakili; Siku mlipotembelea kulikuwa na wananchi kwenye eneo hilo
Shahidi; Hakuna 
Wakili;  na hapa mahakamani hakuna mwananchi amekuja kuthibitisha hilo 
Shahisi; hakuna 
Wakili; Utakubaliana na mimi kuwa hata siku Ile ulipokuwa ukiongea ulikuwa ukimrefer huyuhuyu Erasto Sanare 
Shahidi ; sikumbuki 
Wakili; unatambua Erasto Sanare amewahi kuwa diwani mwenyekiti wa CCM na Mkuu ww mkoa wa Morogoro.
Shahidi; sikumbuki 
Wakili; tucheze video 
Shahidi; sikumbuki 
Wakili tunaomba uicheze video 
Video inawashwa inafika eneo anaonekana Isaac akisema "....mkurugenzi wa Nanina ni kiongozi na alikuwa kiongozi zamani 
Wakili ; Umesikia 
Shahidi; Sijataja jina lolote 
Wakili; mtu akiwa mwizi chombo cha kithibitisha hilo kipo
Shahidi; Sijui 
Wakili; Neno wizi umelitaja mara ngapi tofauti na hii video 
Shahidi; nimesema sikumbuki mara ngapi 
Wakili; imekuwa ni tabia yako ya kutaja 
Shahidi ; inategemea na eneo 
Wakili; neno wizi ulilitaja ....
Shahidi;  sikumbuki 
Wakili; unamfahamu mkurugenzi wa Nanina 
Shahidi!  simjui 
Wakili; ulitoa Hati kwa mtu usiyemfahamu 
Shahidi; halmashauri Haitoi Hati ni kamishina wa ardhi 
Wakili; mlipokuwa shamba majukumu yako yalikuwa ni yapi 
Shahidi; kuangalia 
Wakili! nani aliyekuwa ameshika kamba
Shahidi; sijui 
Wakili icheze video
Wakili Kwa mujibu wa hicho kisehemu (kilichoonyeshwa) nani alikuwa kashika kamba 
Shahidi; nilikuwa nahakiki
Wakili;  ukiwa kama mkiti wa halmashauri kuna shauri lolote lilikuwa dhidi ya mkurugenzi wa Nanina au Nanina schools na ikathibitika wamejiongezea ardhi
Shahidi;hakuna 
Wakili; wewe ni mtaalam wa IT kujua video inayotolewa ni aina gani 
Shahidi: siyo 

SEHEMU YA MASWALI YA MAWAKILI WA MJIBU MAOMBI 
WAKILI;  umeulizwa nani aliyeomba ardhi 
SHAHIDI; ni Nanina 
WAKILI; Uliulizwa kama kulikuwa na wananchi wakati mlipoenda kuhakiki 
SHAHIDI; Hawakuwepo 
WAKILI; Kwani kutaja nafasi mtu alizopitia ni kashifa 
SHAHIDI; Hapana 
W
SHAHIDI; Nilitaja kwa mtu mwingine yoyote akijipatia eneo huu ni wizi 
WAKILI; Kwenye video watu wangapi wanashika kamba
SHAHIDI;  Isaac na Hatibu ambaye ni afisa ardhi wa wilaya 
WAKILI; Amekuuliza wewe ni mtaalam wa IT
SHAHIDI; Haihitaji utaalam unaona ni Monduli online TV 




0 Comments:

Post a Comment