SERIKALI YAKOSHWA MAZINGIRA, TAALUMA SHULE YA TURKISH MAARIF ARUSHA


MKUU wa mkoa wa Arusha, John Mongela ameelezea kuridhishwa na uwekezaji wa elimu uliofanywa na Serikali ya Uturuki kupitia shule yao ya Turkish Maarif  hivyo kutoa fursa kwa raia wanchi hiyo kuja kuwekeza kwenye sekta nyingine mkoani hapa.

 

 Aidha amemhakikishia balozi wa Uturuki nchini, Dkt. Mehmet Gulluoglu kuwa endapo wawekezaji hao watafika watawekewa mazingira bora ikiwemo kupatiwa maeneo yanayofaa.

 

Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Richard Ruyango 

Mongela ameyasema hayo leo (Oktoba 30,2021) katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Richard Ruyango kwenye mahafali ya pili ya kidato cha nne na shule ya awali kwenye shule za Turkish Maarif, (Turkish Maarif Schools) zilizopo Ngaramtoni wilayani Arumeru mkoani Arusha. 


Alisema kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Rais, Samia Suluhu Hassan anawakaribisha wawekezaji kutoka nchi mbalimbali hivyo na Uturuki wqnakatibishwa  tunawakaribisheni si tu kuwekeza kwenye elimu, hata kwenye maeneo mengine.

 

“Nafasi zipo sisi kama mkoa wetu wa Arusha, hasa hamashauri yetu ya Arumeru bado tuna maeneo mengi ya kuwekeza karibuni sana kwenye uwekezaji wa aina yoyote sisi tuko tayari kuwapokea lakini pia kuwawezesha kwa ajili ya miundombinu inayohitajika katoia masuala ya uwekezaji karibuni sana,” alisema Mongela na kuongeza.

 

…Mheshimiwa  Balozi nimeambiwa kuwa shule hii ipo chini ya serikali ya nchi yako na zipo katika nchi 45 ambapo mnatoa msaada na mchango mkubwa kama hivi leo tunavyoshuhudia hapa kwetu mnatoa elimu bora. Tunawashukuru na kuwapongeza kwa kuiona Tanzania kama moja ya nchi zinazofaa kwa uwekezaji,".

 

Akiendelea kuongea kwa niaba ya Mongela, Mkuu huyo wa wilaya ya Arumeru alimuomba balozi huyo wa Uturuki pamoja na serikali yao waendelee kuongeza uwekezaji wa elimu  ili muendelee kuweka vitega uchumi kama vilivyopo Arusha jambo litakalowezesha kutoa elimu kwa watoto hapa nchini.

 

"Nimefurahi kusikia shule hii inatoa fursa kwa vijana kwenda kusoma elimu ya juu nchini Uturuki hii ni fursa kubwa ambayo Watanzania tunaipata kupitia shule hii tunawapongezeni sana," alisema Ruyango kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha na kuongeza .

 

...Kwa wenzangu ambao hii ni mara yao ya kwanza kufika hapa kama mimi, nimefurahi mno na ninaahidi nina motto wangu nitamleta hapa baada ya kuona namna shule hii inavyofanya vizuri. Hata mwakilishi wa wazazi Dkt Robert ametuambia hapa shule ni nzuri, mazingira na elimu ni nzuri hivyo tuna kila sababu ya kuleta watoto wetu hapa,”..

 

...Hata kwa upande wa afya wako vizuri kwa sababu wanakula vizuri mahali pazuri, wanalala vizuri wakiumwa wanatibiwa kwa hiyo tunaamini shule hii ni nzuri hivyo tuendelee kuleta watoto ili mwisho wa siku tupate vijana walioiva katika upande wa elimu,".

 

ARUMERU WATUMIA KLINIKI ZINAZOTEMBEA  KUTOA CHANJO.

Ruyango aliwahimiza wazazi kujitokeza kupata chanjo ili kuzuia  na kujilinda na maambukizi ya ugonjwa wa UVIKO 19 huku akiwakumbusha kuwa wazazi wanahitaji kuwalea watoto wao hivyo ni vema wajitokeze kwa wingi kuchanja.


"Chanjo zinatolewa bila malipo yoyote, kwa wilaya yetu ya Arumeru tuna chanjo 700 tumeanza kutoa kwenye maeneo ya vituo vya afya na zahanati zote lakini pia kuna Kiliniki zinazotembea (Mobile Clinic) kwa wale wenye uhitaji upande wa taasisi. Kama kwenye shule hii kuna watendaji ambao hawajachanjwa mnatuambia tunawaletea chanjo hapa bila wao kutembea kwenda mahali popote tuko tayari kutoa huduma hiyo kwa ajili ya wananchi," alisema Ruyango.

Balozi wa Uturuki nchini, Dkt. Mehmet Gulluoglu


Balozi wa Uturuki nchini, Dkt. Gulluoglu, alisema kuwa wanawashukuru wazazi kwa kuleta watoto wao kwenye shule hiyo huku akiwahakikishia kuwa wanazisimamia shule zao ili ziendelee kutoa elimu bora. 

 

“Watoto waliohitimu tuwaombea mafanikio mema ya kuendelea kwenye elimu ili waweze kufikia ndoto zao za kuwa wataalamu wabobevu kwenye mambo mbalimbali wanayojifunza,” alisema Gulluoglu na kuongeza.

 

“Shule na majengo haitoshi, tunahitaji waalimu na wazazi kuwalea watoto wenye ujuzi, maarifa na maadili mema,” . 

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa huduma za Jamii kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki, (EAC), Stephen Niyonzima, akiongea kwenye hafla hiyo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa EAC, Dkt, Peter Mathuki alisema amefurahishwa kuona shule hiyo inahimiza michezo kwa watoto kwani kwa sasa ndiyo inayoongoza kwa kutoa ajira zenye malipo makubwa duniani.

 

“Tumeona vijana wetu wanaocheza mpira wanapoingiza maelfu ya paundi kwa siku kama mshahara. Hivyo endeleeni kuwakuza vijana kwenye michezo kwani mbali na kuwaingizia kipato lakini inawakuza kiakili,” alisema Niyonzima.

 

Akiongea kwa niaba ya wazazi, Dkt Robert Diemba ameushukuru uongozi wa shule hiyo kwa kutimiza ahadi walizotoa katika kuboresha elimu ya watoto kwa kuweka vifaa vya kufundishia na kulea watoto katika mazingira bora.


Hata hivyo alisema kuwa wazazi tuna wajibu wa kulipa ada kwa wakati, kuwasimamia watoto kufanya kazi za nyumbani na kuwasaidia vijana wawwaw kufikia ndoto zao.



Awali, Mkurugenzi wa shule za Turkish Maarif hapa nchini, Taskin Ayranci alisema wanashirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha wanatoa elimu itakayowafanya vijana wa Taifa hili kuwa bora kwenye ukanda mzima wa Afrika Mashariki.

 


Mkurugenzi wa shule za Turkish Maarif Arusha, Holil Server Sahin alisema kuwa waliingia Tanzania miaka minne iliyopita wakafungua shule Zanzibar na kwa sasa shule yao Sekondari inaongoza kwa kufanya vizuri kitaalum kwa Zanzibar kwenye matokeo mtihani wa  mwaka uliopita.

 

Alisema kuwa wanajipanga kuhakikisha shule zao za Arusha na Dar es Salaam nazo zinafanya vizuri kwa kuendelea kufanya maboresho kwenye mazingira, vifaa na waalimu ili kuhakikisha elimu inayotolewa inakuwa bora zaidi.

 

 

Shule hiyo inayomilikiwa na serikali ya Uturuki ilianza Ngaramtoni, Arumeru mwaka uliopita ina jumla ya wanafunzi 486 kati yao shule ya awali, 78, msingi 199, sekondari 194 na kidato cha tano 15.

 


0 Comments:

Post a Comment