MIKOA TISA HAINA MAHAKAMA KUU - SSH

Rais, Samia Suluhu Hassan, akikata Utepe kuzindua rasmi Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki katika eneo la National Capital City Jijini Dodoma leo (Oktoba, 06 2021). Wa pili kulia ni Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma, Spika wa Bunge Job Ndugai, Jaji Mkuu wa Zanzibar Othman Makungu wa pili kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Palamagamba Kabudi, Mkuu wa Mkoa Dodoma Antoni Mtaka.


Rais, Samia Suluhu Hassan, kuna mikoa tisa ambayo haina mahakama kuu hivyo akatoa wito kwa mahakama kuhakikisha  mikoa hiyo inapewa kipaumbele kwenye Mpango Mkakati wa Miaka Mitano ijayo utakaowasilishwa kwa wadau na washirika wa maendeleo mwaka huu 

Ameyasema hayo leo wakati akizindua rasmi Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki katika eneo la National Capital City Jijini Dodoma leo (Oktoba, 06 2021)

Amesema serikali pamoja na wadau watajitahidi kufika katika ngazi za Wilaya na Kata ambazo hazina Mahakama, wataongeza idadi ya Majaji na Mahakimu pamoja kuendelea kuanzisha Mahakama zinazotembea katika mikoa mbalimbali 


"Nawapongeza kwa kuimarisha matumizi ya Mahakama ikiwemo kuanza usajili na kusikiliza kesi kwa njia ya mtandao, haya ni mapinduzi makubwa ambayo yamesaidia kurahisisha uendeshaji wa kesi na kudhibiti rushwa katika Mahakama zetu," amesema Rais Samia na kuongeza

...Serikali inaendelea kujenga Mahakama za Mwanzo, Wilaya, Hakimu Mkazi na Mahakama Kuu kwenye maeneo mbalimbali nchini. Miaka mitano iliyopita Serikali ilijenga na kukarabati Mahakama Kuu za Kanda 7, Hakimu Mkazi 7, Wilaya 28 na za Mwanzo 25, tumeanza pia kufanya majaribio kwa Mahakama za kutembea kwenye Mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza.

....Kwa niaba ya Serikali na Watanzania natumia fursa hii kuishukuru Benki ya Dunia kwa kutuwezesha kutekeleza mradi huu ambao umeifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza Barani Afrika, tunaomba waendelee kutushika mkono katika awamu ya pili ya maboresho ya Mahakama,".

Amesema vituo hivyo sita vimegharimu  jumla ya TSH Bilioni 51.5 ambazo ni sehemu ya mkopo wa Dola za Marekani milioni 65 kutoka Benki ya Dunia uliokopwa serikali kwa ajili ya kutekeleza mradi wa maboresho ya Mahakama.

"Haki inayocheleshwa ni sawa na haki inayonyimwa hivyo uanzishwaji wa vituo hivi jumuishi utasaidia kupunguza tatizo la ucheleweshwaji wa kesi," amesema Rais Samia na kuongeza. 

....Naipongeza Mahakama kwani thamani ya fedha (TSH Bilioni 9) iliyotumika katika ujenzi wa Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki inaendana na jengo. Nimefurahishwa kwa kukumbuka huduma za watu wenye mahitaji maalum pamoja na vyumba vya kunyonyeshea watoto katika jengo,".

Kwa upande wake, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma
amesema kuwa Vituo Jumuishi vya Utoaji haki vitashughulika  na mashauri ya kifamilia, watoto, ndoa, talaka na matunzo, ni kituo ambacho Majaji na Wasajili watafanya kazi na watu wengine katika jengo moja.

Amesema  Tanzania imekuwa  nchi ya kwanza kuwa na majengo Jumuishi hivyo itakuwa ni sehemu ambayo nchi mbalimbali zitakuja kujifunza.


"Maboresho ya Mahakama ni uwekezaji ambao umetumia kiasi kikubwa cha fedha lakini ni uwekezaji utakaojenga amani, utulivu na utawala bora,$ amesema  Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Hamis Juma na kuongeza

....Mchango wa Mahakama ya Tanzania ni kuweka mazingira ya amani, usalama na umoja pamoja na kujenga utawala bora ambapo tunaamini uwepo wa vitu hivyo ni kichochea uchumi imara unaoweza kuinua ustawi wa wananchi,".

0 Comments:

Post a Comment