| Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya leo akiteta jambo na wakili wake, Moses Mahuna wakiwa kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha. |
MAHAKAMA ya hakimu Mkazi Arusha imelionya gazeti la Mwananchi kuacha kuandika habari za kupotosha juu ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya na wenzake sita.
Uamuzi huo mdogo umetolewa leo na Hakimu Mkazi, Patricia Kisinda anayesikiliza shauri hilo la uhujumu uchumi namba 27/2021 baada ya mawakili wa utetezi kulalamikia taarifa za upotoshaji zilizotolewa na gazeti hilo mara mbili tofauti.
Baada ya kusikiliza hoja za mawakili hao wa utetezi zilizowasilishwa na Wakili mwandamizi, Moses Mahuna na zile za mawakili wa serikali waandamizi, Ofmed Mtenga na Felix Kwetukia huku upande wa gazeti la mwananchi ukiwa hauna uwakilishi hakimu huyo aliahirisha kwa muda shauri hilo kwa ajili ya kuandaa uamuzi huo.
'"Mahakama inaamini kila mtu ana haki ya kupata habari na vyombo vya habari vina haki ya kuhabarisha umma hivyo haki hiyo haiwezi kuchukuliwa na mahakama ila mahakama inavitaka vyombo vyote vya habari kuhakikisha wanatoa habari sahihi," amesema Hakimu Mkazi, Kisinda akitoa uamuzi.
Amesema kuwa kwa hatua ya sasa mahakama inatoa onyo kwa Mwananchi kuacha kuripoti habari zinazopotosha umma na kuripoti habari sahihi.
"Wasipofanya hivyo mahakama haitakuwa na namna nyingine zaidi ya kutoa zuio kwa wahusika kama ilivyoombwa na mawakili wa utetezi,", Amesema hakimu Mkazi Kisinda wakati akimalizia kutoa uamuzi huo
Awali mawakili wa utetezi, kwenye shauri hilo waliiomba
mahakama ilizuie gazeti la mwananchi na kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii isiripoti kesi hiyo kwa madai kuwa wanapotosha.
Wakili mwandamizi, Mahuna aliwasilisha ombi hilo leo mbele ya hakimu mkazi, Kisinda mufa mfupi baada ya shahidi wa nane, Johnson Kisaka kupanda kusimama kwenye eneo la kutolea ushahidi wake.
Mahuna aliielza mahakama hiyo kuwa wanaleta maombi yao chini ya kifungu cha 392 A 1 cha mwenendo wa makosa ya jinai wakiiomba mahakama ilizuie gazeti la Mwananchi kuripoti kesi hiyo.
Aliomba mahakama hiyo ilizuie gazeti la Mwananchi na wafanyakazi wa gazeti hilo wasiruhusiwe kuripoti kwenye vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi juu ya kesi hiyo.
"Mheshimiwa si gazeti hilo tu, na vyombo vingine vinavyoshabihiana na gazeti hilo iwe radio au televisheni visiruhusiwe," aliomba Mahuna
Akiwasilisha hoja zake za kwa nini anaomba gazeti hilo lizuiwe kuripoti kesi hiyo Mahuna alieleza mahakama,
"Mheshimiwa 'concern' yetu iko namna kesi hii inavyokuwa 'reported na media specifical' gazeti la mwananchi na kurasa zao za social media hasa instagram mwananchi_ officia oficial," ameeleza na kuongeza.
....Jana shahidi aliwasilisha cheti cha uthibitisho wa mfumo kurekodi wa kamera ila mwananchi wakaandika kinaonyesha namna sabaya na wenzake walivyorekodiwa wakiwa kwenye benki ya CRDB tawi la Kwa Mromboo ....
....Kwenye 'proceeding' za mahakama hii hakuna mahali kuna kitu hicho hata kwenye cheti hicho ambacho ni 'exhibit' namba nne hakuna mahali wanapomzungumzia Sabaya na wenzake kuonekana kwenye eneo hilo...
....Hii si ya kwanza kwa gazeti la Mwananchi. Alikuja hapa shahidi wa pili meneja waTRA, Hosea Majogolo, gazeti hilohilo likaandika meneja wa TRA amkana Sabaya wakati hapakuwa na kitu kama hicho kwenye proceeding...
....Hatujui wanafanya hivyo kwa manufaa ya nani, wanachokifanya kina effect kwetu kwa mawakili wa serikali na mahakama kwani uamuzi utakaotoka ukiwa tofauti na hicho wanachoripoti utaleta impression sio nzuri kwa umma,".
Baada ya wakili Mahuna kumaliza kuwasilisha maombi hayo Hakimu Mkazi, Kisinda alitaka kujua endapo kuna mwakilishi wa gazeti la mwananchi mahakamani hapo akajibiwa hayupo.
Hata hivyo wakili wa Serikali Mwandamizi, Ofmed Mtenga akaomba kuchangia kwa kile alichoeleza mahakama hiyo kuwa madai yaliyotolewa dhidi ya gazeti la Mwananchi ni jambo lililofanyika nje ya mahakama hiyo hivyo hazipaswi kuwa sehemu ya mwenendo wa shauri hilo.
Aliieleza mahakama hiyo kuwa kama upande wa utetezi wana malalamiko walipaswa wayalete mahakamani tofauti na si kuyaingiza ndani ya mwenendo wa shauri hilo ili nao Mwananchi wapate nafasi ya kujibu.
"Sasa kuleta malalamiko dhidi ya mtu ambaye si 'part' ya kesi hii ni kuleta mkanganyiko kwani hata ikikatiwa rufaa kwenye mahakama za juu haina mlango wa kujadiliwa," ameeleeza, Wakili Mwandamizi Ofmed na kuongeza.
....Ni maombi yangu hii 'part ya allegation' ingewekwa pembeni kwani imekuja sehemu ambayo si sahihi. Zisiwekwe kwenye mwenendo wa kesi yetu,".
Kwa upande wake Wakili wa Serikali Mwandamizi, Felix Kwetukia aliieleza kuwa anakubaliana na wakili Mahuna kuwa maombi yanaweza kuwasilishwa mahakamani kwa mdomo ila akasisitiza maombi hayo yanapaswa kuwasilishwa kwa mjibu maombi.
Aliieleza mahakama kuwa sheria hiyo inataka mjibu maombi apewe muda wa kujibu maombi hayo jambo alilouliza mjibu maombi ni nani?.
Kwetukia aliendelea kuieleza mahakam hiyo kuwa mjibu maombi huyo hayupo mahakamani hapo na ndiye angeweza kuieleza mahakama hayo aliyoyaandika kwa minajili gani .
"Hata sisi tungependa hizo 'allegation' anazotuhumiwa nazo azijibu lakini kwa utaratibu uliofuatwa hapana labda yaletwe maombi yanayojitegemea kama ni jinai au madai lakini kwenye kesi nyingine tofauti na hii," amesema Wakili Kwetukia na kuongeza.
"Ndani ya mwenendo huu ni Jamhuri dhidi ya Sabaya na wenzake sita hatuna Mwananchi news paper wala mwananchi kwenye mitandao ya twitter na instagram kwa heshima kabisa nimuombe wakili Mahuna na wenzake watafuta 'proper remedies' kwa hao wanaowalalamikia
mbao anaomba mwananchi waptiwe 'gag order',".
Hata hivyo wakili Mahuna alipinga hoja hizo kwa kile alichoieleza mahakama hiyo kuwa kifungu cha sheria alichotumia kipo sahihi na kuwa maombi hayo ya mdomo dhidi ya gazeti la mwananchi yapo sahihi mahakamani hapo.
"Mwananchi anaripoti kwa kuwa mahakamani au bila kuwepo na ndiyo maana mahakama yako iliuliza kama wapo ili waweze kurespond lakini hawakuwa inashangaza na kushtua kama vile wanataka kuzuia 'discretion' ya mahakama katika 'kuregulate proceeding' za kesi hii na kitu kinachozungumzwa hata hakijatolewa hukumu," alieleza wakili mwandamizi Mahuna.
Hata hivyo wakili wa serikali Mwandamizi, Kwetukia alisimama akaonya "wakili asituwekee maneno sisi hatujasema Mwananchi wasiekewe 'gag' ila tumesema utaratibu sahihi ufuatwe,".
0 Comments:
Post a Comment