Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo ameahidi utiifu kwa Rais, Samia Suluhu Hassan
Mabeyo amemhakikishia kuwa ulinzi wa nchi na mipaka yake ni salama na vitaendelea kumlinda, kumtii kama Amirijeshi mkuu na kutekelezamajukumu yake kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.
‘’Tunakuahidi utiifu, uadilifu na uaminifu mkubwa kama ilivyo ada ya mila na desturi ya majeshi yetu katika awamu zote zilizopita kwa manufaa ya ulinzi, usalama na ujenzi wa taifa letu’’. Alisema Jenerali Mabeyo.
Aliyasema hayo leo mjini Chato wakati akimpongeza Rais, Samia Suluhu Hassan kwa kuapishwa kuwa Amirijeshi Mkuu.
Kuhusu namna alivyomfahamu na kufanya naye kazi hayati Magufuli Jenerali Mabeyo alisema;
‘’Aliviamini na kuvipenda vyombo vya ulinzi na usalama alihakikisha kuwa anaviwezesha kwa mahitaji ya kiutendaji na utawala ili viweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na weledi mkubwa.’’ alisema Mabeyo na kuongeza
...Alisema hatuwezi kuwa na vyombo vya ulinzi imara bila kuwa na uchumi madhubuti, hatuwezi kutegemea misaada ya kuimarisha vyombo vyetu lazima tuimarishe uchumi wetu ili tuweze kuimarisha vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.’’
Mabeyo amesema walishiriki katika kulinda mgodi wa Tanzanite, na kabla ya kulinda, kujenga ukuta kuzunguka mgodi huo.
0 Comments:
Post a Comment