RAIS Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete amesema taarifa ya kifo ilikuwa jambo gumu kulipokea na kulikubali.
Uhusiano yake na hayati Magufuli tangu alipokuwa waziri wake, Kikwete amesema alikuwa jembe lake.
Nilipokuwa Rais, Magufuli alikuwa Waziri wangu kwa miaka 10, alikuwa mmoja wa mawaziri niliowaamini na kumtumaini.
‘’Alikuwa jembe langu ndio maana nilimuweka kwenye wizara tatu zilizokuwa ngumu ili anyooshe mambo.’’ Alisema Kikwete.
‘’Yalikuwa matumaini yangu na matarajio yangu angemaliza kipindi chake cha uongozi salama, akastaafu na kuishi maisha marefu baada ya hapo na kupata nafasi ya kutuzika sisi watangulizi wake ambao ni kaka zake, hili la kututoka kabla ya kumaliza muhula wake na sisi kumzika yeye ni jambo ambalo sikuwahi kulifikiria kabisa.’’ Alisema Kikwete.
Amesema uongozi wake bado ulikuwa ukihitajika Tanzania, na kuwa alikuwa akitamani akamilishe kazi yake nzuri aliyokwisha ianza.
0 Comments:
Post a Comment