Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa,
Freeman Mbowe amezidi kuiandama Serikali ya CCM kuhusu tuhuma za
ufisadi wa trilioni 1 kwenye ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara
kwenda Dar es Salaam, ambapo sasa ameenda hatua nyingine akiitaka
Serikali iweke wazi mkataba wa ujenzi huo ili mbivu na mbichi
zibainike.
Huku akiendelea kusisitiza kuwa ufisadi huo umevunja rekodi za kashfa
mbambali kubwa ambazo zimekuwa zikifanywa na baadhi ya viongozi
serikalini na jamaa zao, ameitaka serikali pia kuweka mkaguzi wa
kimataifa kukagua hesabu za ujenzi wa bomba hilo.
Mbowe ambaye yuko kwenye ziara iliyopewa jina la 'Operesheni Delete
CCM' (ODC), aliyoizindua mkoani Tabora kuanzia Alhamis wiki hii,
alidai kuwa kufuatia kashfa hiyo, sasa Watanzania watapata majibu
kwanini ilitumika nguvu kubwa kuwanyamazisha wananchi wa Mikoa ya
Kusini waliokuwa wakitaka kujua namna watakavyonufaika na rasilimali
ya gesi.
Akizungumza na wananchi wa mjini Tabora katika mikutano miwili
tofauti, Tumbi na Gongoni, Mbowe amesema tuhuma hizo za ufisadi wa
kutisha haziwezi kufumbiwa macho na Mtanzania yeyote mzalendo.
"Tunataka serikali iweke wazi mkataba wa ujenzi wa bomba la gesi
kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam...tunataka kujua mbivu na mbichi
katika ufisadi huu ambao unakwenda kuvunja rekodi ya kashfa zote za
ufisadi ambazo zimekuwa zikiindama Serikali ya CCM kwa muda mrefu
sasa...mmoja baada ya mwingine...hatuwezi kukubali.
"Hatuwezi kukubali kwa sababu hizi ni fedha za Watanzania...utalipa
wewe mama muuza chakula, utalipa wewe Mwalimu unayekopwa na serikali
hii hii, nitalipa mie hapa Mbowe, kila Mtanzania atalipa mkopo huu wa
matrilioni ya fedha ambayo watu wachache wameweka mifukoni mwao kwa
kuongeza gharama za ujenzi wa bomba hilo," alisema Mbowe na kuongeza;
"Tunaitaka serikali kuweka mkaguzi wa kimataifa kuchunguza ufisadi huu
wa trilioni moja na zaidi ambapo wakubwa wameamua kuongeza gharama za
ujenzi wa bomba mara dufu...kutoka trilioni 1 hadi kuwa trilioni 2,
huku moja ya ziada ikienda mifukoni mwa baadhi ya walioko madarakani
na jamaa zao."
Akiwa mjini Igunga Alhamis wiki hii na juzi katika maeneo mbalimbali
wilayani Nzenga, mkoani Tabora, Mbowe alifichua tuhuma nzito za
ufisadi huo ambapo alisema kuwa umetokana na gharama za ujenzi huo
kuongezwa mara mbili ya gharama halisi za awali, akidai kuwa nyongeza
hiyo ya takriban trilioni moja ilikuwa kwa ajili ya 'mifuko' ya baadhi
ya viongozi serikalini na jamaa zao.
Katika tuhuma hizo Mbowe alisema kuwa gharama halisi za ujenzi huo
zilikuwa ni Dola za Marekani Mil. 600 lakini kwa maslahi ya watu ambao
hakuwataja, ikaongezwa na kuwa Dola za Marekani Mil. 1200.
RAIS SAMIA AUMIZWA MAUAJI YA KIBIKI
-
-Simanzi yatanda mazishi yake
-Nchimbi: matukio ya kutia hofu na shaka, hayakubaliki
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano...
42 minutes ago
0 Comments:
Post a Comment