MANENO YA DR.SLAA
Tumepata taarifa za ziara yake ya kwenda China. Siwezi kusema atakwenda tarehe ngapi maana mimi si kazi yangu kutangaza tarehe za ziara za Kikwete ambazo sasa hata tumechoka kuhesabu maana zimeshakuwa nyingi mno zaidi ya 300+ ndani ya miaka kumi.
Kilichotushtua si Kikwete kwenda ziara, maana siku hizi wala si habari tena, kilichotushtua ni hicho kinachompeleka huko China… ukimsikiliza Kikwete kwenye mazungumzo anapenda kuonekana
mtu anayeoenda amani, mshikamano
lakini si kweli.
Amejigeuza Ofisa Manunuzi. Kwa miezi kadhaa sasa kumekuwa na
jitihada za kupata helkopta tatu mpya… zingelikuwa ni kwa ajili ya Jeshi letu la Wananchi nisingekuwa na shida, shida inakuja namna zinavyotafutwa.
Zinatafutwa kwa
utaratibu ule ule wa kifisadi uliotumika kununua ndege ya rais wakati ule na hata rada.
Tena anamtumia kampuni moja hivi
ambayo tumekuwa tukiituhumu katika ufisadi. Sasa sisi tunahoji, hivi ni kwa nini Serikali ya CCM inashindwa kwenda kiwandani na
kufanya order ya manunuzi kiwandani moja kwa moja hadi itumie taratibu za kifisadi au
mafisadi kufanya kazi hizi… Kikwete anajua kuwa ninajua.
Maana ameshalalamika kwa watu wake wa
vyombo vya dola kwamba taarifa hizi
zimefikaje kwa Dokta Slaa…
Wametumia fedha zetu za mikopo kutoka Ujerumani…ndege
zinanunuliwa Ufaransa…anatuma
fisadi kwenda kufanya manunuzi hayo badala ya Serikali…
Kinachoonekana na taarifa na sisi hapa tunahoji je ni kweli ndege hizo zinataka kutumika kwa manufaa ya CCM?
Rais pia ameomba kwenda Beijing
kufuatilia mitambo ya Police Surveillance System…wanataka
mitambo hiyo ifike hapa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015… ujumbe huu umeandikwa na mtu anaitwa Mbelwa…Kairuki.
Waandishi wa habari mtakuwa mnajua huko Wizara ya Mambo ya Nje.
Anamwandikia Waziri wa Mambo ya
Nje…ujumbe huu umeandikwa
tarehe 7/10/2014…
Sasa hizo ndege anayotaka kununua
iko mji mwingine huko China si ule
aliopangiwa katika ziara yake, sasa imeagizwa irushwe hadi pale.
Atakapokuwa ili eti Rais mwenyewe awezekuiona… nimeangalia kwenye budget component hiyo kitu hakuna.
Kwa kawaida vitu vya kijeshi huwa havitajwi kwenye bajeti, lakini kwenye randamana ungeweza kuona mpango wa kununua kitu kama hicho. Hakuna.
Sasa kinachoonekana ni kwamba kwa
sababu wamejua mwaka 2015
wanaondoka madarakani, wanaanza
kujiandaa kwa mapambano badala
ya maridhiano.
Nataka kumwambia Rais Kikwete
kwamba nchi haiongozwi kwa misuli,
haiongozwi kwa kutunishiana misuli.
Wanataka kufanya kama walivyofanya
majuzi kutunga Katiba Mpya kwa mitutu ya bunduki.
Sasa tena uchaguzi unakaribia wanaanza maandalizi ya mitutu…
tunamwambia Kikwete sisi tutakuwa wa mwisho kuona nchi hii inaingia katika vurugu. Ndiyo maana ili kuepusha mambo mabaya yasitokee kila taarifa kama hii tukiipata tutapiga kelele. Silaha kubwa ya mnyonge ni kupiga kelele.
Katika mwendo huo huo wa Rais Kikwete kugeuka kuwa Ofisa Manunuzi, sasa amejigeuza kuwa
Bwana TCRA, wanapanga kukutana
na Kampuni ya HUAWEI ya China ili
wanunue mtambo utakaowekwa ikulu
kwa ajili ya kunasa simu za akina Dokta Slaa…
Mitambo hiyo inapelekwa ikulu
badala ya…ingepelekwa Usalama wa Taifa ningeelewa, ingepelekwa kwenye Jeshi letu ningeelewa, lakini ikulu?
Tunasisitiza hatuna tatizo kama mambo haya ya ndege, helkopta au mitambo ya mawasiliano
yangekuwa yanafanywa kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi, lakini ni tatizo kubwa kama rais ndiye anakuwa Ofisa wa Manunuzi au Ofisa wa Mawasiliano, TCRA.
Sasa wanatafuta na kuhangaika kutafuta kila njia ya kubaki madarakani.
Tunamuonya Rais Kikwete kuwa hizo
pesa anazotaka kuchezea kwa yeye
kuwa Ofisa Manunuzi si za mfukoni mwake. Aache kuchezea fedha za Watanzania.
Tulimuonya pia hivi hivi
wakati alipochezea fedha za Stimulus Package. Kama anataka
kutukamata atukamate lakini sisi tutasema.
Haya ndiyo mambo ya madhara ya katiba inayopendekezwa, kama ambavyo tumeshasema vizuri mapema.
Sent from My iphone
TBS Yatoa Wito Kwa Wafanyabiashara Kuboresha Ubora wa Bidhaa kwa Kutumia
Teknolojia na Ubunifu
-
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewataka wafanyabiashara kutumia
teknolojia na kuongeza ubunifu unaozingatia kanuni ...
12 minutes ago
0 Comments:
Post a Comment