BAADHI YA NUKUU MUHIMU KUTOKA KWA MWALIMU NYERERE

Wise Quotes from Mwalimu Nyerere:
Inawezekana tatizo la paka kwa panya lingekwisha kama paka angefungiwa kengele
shingoni: taabu ni kumpata panya wa kuifanya kazi hiyo. Na panya watakuwa wajinga sana wakidhani kuwa paka watajifunga au watafungana kengele shingoni"
***********************
'Hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa mawazo, ni umaskini mbaya sana' 01/5/1995
***********************
'Mtu mwenye akili akikuambia maneno la kipumbavu, na anajua ni ya kipumbavu na anajua unajua ni ya kipumbavu
-ukayakubali, atakudharau!!! 01/5/1995
***********************
"Siku inakuja ambapo watu watachagua kifo kuliko fedheha na ole wao wale watakoiona siku
hiyo! Na ole wao wale watakaoifanya siku hiyo
isiepukike. Natumaini na kusali kuwa siku hiyo kamwe haitofika" –Mwalimu Nyerere (Januari,
1966)
***********************
"Rushwa ni adui wa haki. Tunamtaka Rais ambaye atalitambua hilo na ataichukia rushwa hata ukimuangalia anaonesha kweli anaichukia
rushwa, sio Rais ambaye anayesema kweli rushwa ni adui wa haki.... Lakini ukimuangalia
usoni unashangaa na kusema.... aaaah kweli hata huyu?
***********************
"Poverty is not the real problem of the modern world. For we have the knowledge and resources
which could enable us to overcome poverty. The real problem-- the thing which causes misery, wars, and hatred among men--is the division of mankind into rich and poor."
***********************
Amini nawaambieni enyi Waswahili wachache
mnaotawala; mnategemea kweli kuwa mtawaongoza Watanzania kwa lazima wakati
wamepoteza matumaini, na mtegemee kuwa watasalia wamekaa kimya kwa amani na utulivu?
***********************
Amani ni zao la matumaini, pindi matumaini yatakapotoweka kutakuwa na vurugu katika jamii.
***********************
Wakati wengi wa wananchi wanapopoteza matumaini unajenga volcano. Volcano hii
italipuka siku moja. Labda kama watu hawa ni wajinga.
***********************
Kukubali kukandamizwa namna hiyo wakati wanayo nguvu inayotokana na wingi wao, ni kwa
sababu ni wajinga tu.
***********************
Hivyo basi Watanzania watakuwa ni wajinga na matahira, kama watakubali kuendelea
kukandamizwa na watu wachache (viongozi) katika nchi yao wenyewe....
***********************
Source inapatikana kwenye
hiki kitabu "Reflections On Leadership in Africa" VUB
University Press, 2000.

Sent from Grace Macha

0 Comments:

Post a Comment