Bill Gates arejea kuongoza kwa utajiri duniani



Licha ya ufadhili mwingi wa mashirika ya misaada na miradi ya maendeleo, Bill Gates anaendelea kushikilia nafasi ya kwanza katika matajiri wa Marekani
Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa na jarida la Forbes ya watu 400 wenye mali nyingi zaidi, Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa zamani wa shirika la Microsoft Bill Gates anaongoza orodha ya matajiri nchini Marekani. 
Nafasi ya 2 ilichukuliwa na Warren Buffet akiwa na thamani ya dola bilioni 67 huku mmiliki wa Oracle Larry Ellison akiwa wa 3 na dola bilioni 50.
Mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg alishikilia nafasi ya 11 na dola bilioni 34 huku waanzilishi wa Google Larry Page na Sergey Brin wakishikilia nafasi za 12 na 13 wakiwa na thamani ya dola bilioni 31.5 na 31 mtawalia. 
Orodha hiyo ilijumuisha mababe wengine wa teknolojia kama vile mmiliki wa Amazon Jeff Bezos akiwa na dola bilioni 30.5 katika nafasi ya 15 huku Mtendaji Mkuu mwingine wa zamani wa Microsoft Steve Ballmer akishikilia nafasi ya 18 kwa thamani ya dola 22.5.