Serikali imeondoa zuio la mikutano ya
Vyama vya Siasa lililokuwa limetangazwa
mwezi Mei mwaka juzi kuzuia mikutano
hiyo kufanyika katika mikoa ya Lindi na
Mtwara. Zuio hilo limeondolewa na
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Mhe. Mathias Chikawe.
Mikutano hiyo ilizuiliwa kutokana na
vurugu za wananchi waliokuwa wakipinga
ujenzi wa mradi wa bomba la gesi
kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam
hali iliyosababisha kuvunjika kwa amani
na utulivu katika mikoa hiyo. Katika
vurugu hizo, watu kadhaa walipoteza
maisha na wengine kujeruhiwa huku
magari na nyumba zikichomwa moto.
Hatua hii ya sasa imechukuliwa baada ya
Serikali kuridhika kuwa hali na amani na
utulivu imerejea katika mikoa hiyo na
kuwa mikutano hiyo sasa inaweza
kuendelea kwa kufuata sheria na
utaratibu uliowekwa.
Aidha Jeshi la Polisi litaendelea kutoa
ushirikiano katika uendeshaji wa mikutano
ya kisiasa inayoendelea katika maeneo
mbalimbali nchini na kuwa vibali vya
mikutano vitaendelea kutolewa kufuatana
na mazingira yatakayokuwepo katika eneo
ambapo Chama husika kitakuwa
kimeomba kibali.
Ni matumaini ya Serikali kuwa Vyama
vya Siasa vitatumia fursa hii kuendesha
mikutano yao kwa amani na utulivu kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi kama
taratibu za uendeshaji wa mikutano hiyo
zinavyoelekeza.
Imetolewa na:
Isaac J. Nantanga
MSEMAJI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
07/10/2014
SERIKALI YATOA TAKRIBANI SHILINGI BIL. 41 KUBORESHA MIONDO MBINU SUA
-
NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO
Takribani shilingi bilioni 41 zimetolewa na serikali kupitia Mradi wa Elimu
ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) unaofadhiliwa...
2 hours ago
0 Comments:
Post a Comment