Mjumbe wa kamati kuu CHADEMA na mbunge wa Arusha mjini mhe. Godbless Jonathan Lema leo atakuwa mgeni rasmi katika chuo cha Arusha Tumaini Collage akiongea na kachero wetu mbunge huyo wa Arusha mjini amesema atatumia nafasi hii kukemea uhuni unaofanywa na serikali ya CCM.
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema, (CHADEMA), amesema Serikali ya Chama Cha Mapinduzi, (CCM) imeshindwa kutatua la ukosefu wa ajira kwa
vijana nchini hivyo akawataka vijana wanaohitimu elimu wajiandae
kisaikolojia kukabiliana na tatizo hilo ambalo linazidi kuongezeka
siku hadi siku.
Pia, Serikali imeshindwa kuboresha mitaala ili elimu inayotolewa
mashuleni na vyuoni iwafanye wanaohitimu waweze kujiajiri badala ya
kutumia muda mwingi wakizunguka na vyeti vyao mitaani kutafuta ajira
ambazo kimsingi hazipo na zikiwepo hutolewa kwa kujuana.
Lema aliyasema hayo juzi alipokuwa akiongea kwenye mahafali ya tatu ya
Chuo Cha Tumaini Arusha, (ATC), ambapo jumla ya wanachuo 113
walihitimu kwenye fani za utalii, hotelia, ualimu, biashara, lugha za
kimataifa na kompyuta.
Alisema kuwa ni vema vijana ambao wako shule na wale wanaohitimu
wajipange wakijua wakihitimu watafanya nini ili wajiingizie kipato na
ikiwezekana wawaajiri wengine.
“Hapa nimeambiwa mmejengwa vizuri kitaaluma , sasa niwaombe jambo
moja, ukitoka hapa usijielekeze kukimbilia kwenye makampuni makubwa
kwa ajili ya kuajiriwa, amua mimi sasa najiajiri ili baadaye niwaajiri
wenzangu,” alisema Lema.
Alisema kuwa kuna matajiri wengine wanamiliki mahoteli makubwa hapa
mjini si kwa kuwa wana elimu kubwa bali waliamua kuwa wanajiajiri,
wakaamini wanaweza, wakajituma kwa bidii kisha wakafanikiwa hivyo nao
wakiwa na nia hiyo watafanikiwa.
Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho, Ernest Mollel, alisema kuwa kwa
sasa wanatafuta eneo ili waweze kukipanua chuo hicho ambacho kwa sasa
kiko kwenye jengo la Moleli jijini hapa.
Alisema kuwa wamekuwa wakihakikisha wanatoa mafunzo kwa ubora na
kiwango kinachokubalika kitaifa na kimataifa ili kuhakikisha wahitimu
wa chuo hicho wanakuwa bora na wanaoweza kufanya kazi ndani na nje ya
nchi.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Levelos, Ephata Nanyaro, (CHADEMA),
eneo kilipo chuo hicho alimpongeza Mollel kwa kuamua kuwekeza kwenye
kutoa mafunzo ya kuwawezesha vijana kujiajiri .