Watanzania
wametakiwa kuwa makini na watu wanaodaiwa kuwa wanafanya unafiki wa kumuenzi
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa maneno ya jukwaani, huku wakimnanga kwa
kufanya vitendo vya kifisadi na ubadhirifu kinyume na mafundisho yake.

Badala
yake, hasa wakati huu ambapo taifa linapitia kwenye changamoto za kuandika
Katiba Mpya, wananchi wametakiwa kumuenzi Baba wa Taifa kwa vitendo, kwa
kupigania katiba mpya inayozingatia maoni ya wananchi kwa ajili ya maisha yao
na hatma ya taifa.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
alipoongoza msafara wa viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwenda
kuzuru kaburi la Baba wa Taifa na kuijulia hali familia ya Mwalimu Nyerere, kijijini
Mwitongo, Butima juzi, Jummane.
Viongozi
hao walipokelewa nyumbani kwa Mwalimu Nyerere na mmoja wa watoto wa familia
hiyo, Madaraka Nyerere ambaye aliwatembeza katika kaburi la Hayati Baba wa
Taifa, ambapo walipata fursa ya kuweka mashada ya maua katika kaburi hilo.
Akiwakaribisha
viongozi hao, Madaraka alisema kuwa pamoja na kwamba Mwalimu Nyerere alikuwa mwanachama
wa CCM, lakini familia hiyo inatunza hadhi yake ya kuwa Baba wa Taifa kwa
kuwakaribisha watu mbalimbali hata kama ni wanachama au viongozi wa vyama vya upinzani,
kutembelea kaburi hilo.
Dkt.
Slaa aliyekuwa ameongozana na Mjumbe wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF),
Mustapha Wandwi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha
NCCR-Mageuzi, Hemed Msabaha pamoja na Kiongozi wa Shura ya Maimamu, Suweid
Sadiq;
0 Comments:
Post a Comment