Katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Dk.
Willbroad Slaa ambae pia ni kiongozi wa msafa a UKAWA kanda ya kaskazini
amesema licha ya kuwepo kwa mvutano wa muundo wa serikali kwenye katiba
mpya,katiba ya mwaka 1977 inayotumika sasa ina mfumo wa serikali tatu.
Dk. Slaa amesema hayo wilayani Bunda mkoa wa Mara kwenye
mkutano wa Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA ambapo amesema katiba ya Tanzania
ya mwaka 1977 inayotumika hivi sasa inabainisha wazi mambo ya muungano na
yasiyokuwa ya muungano na kwamba katiba hiyo imeweka wazi mfumo wa serikali ya
Zanzibar hivyo wajumbe wanapaswa kupitisha rasimu ya katiba mpya ili kuiweka
Tanganyika hadharani kama ilivyo Zanzibar.
0 Comments:
Post a Comment