Mwalimu Nyerere kuanza Shahada ya Uzamivu

 



MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Profesa Haruna Mapesa amesema katika siku za usoni wanatarajia kuanzisha Shahada za Uzamivu (PhD) katika chuo hicho.



Amesema hayo leo wakati akizungumza kwenye Kusanyiko la Wahitimu Waliosoma katika chuo hicho kwenye Ukumbi wa Utamaduni.



Katika kusanyiko hilo kulikuwa na mada moja, inayosema Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kinavyojipambanua katika  Kuchagiza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa Vijana.



Amesema kwa sasa wanatoa kozi kuanzia Stashahada, Astashada, Shahada ya kwanza na ya Umahiri, hivyo kwa siku za karibuni wataanza kutoa Shahada ya Uzamivu.


"Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kina walimu zaidi ya 100 wenye PhD, hivyo tuna nguvu na ujasiri wa kuanzia shahada hiyo hapa kwetu, wahitaji wajiandae," amesema.



Amesema ubora wa chuo hicho umezidi kuongezeka, ambapo kila mwaka wahitimu wanaongezeka.


Profesa Mapesa amesema mwaka 2020 wanafunzi 3,154 walihitimu, 2021 wahitimu 4,159, 2022 wahitimu 5,691, 2023 wahitimu 5,499 na 2024 wahitimu 

5,255


Mafanikio hayo ni juhudi za watumishi, serikali na wanafunzi, hivyo dhamira yao ni kuendelea kubakia katika hali hiyo.


Amesema wanaendelea kufanya maboresho kuhakikisha MNMA inaendelea kuwa bora zaidi.


"Mipango ya chuo ni kuboresha mifumo ya teknolojia, kununua kompyuta za kisasa, madarasa janja na vingine vingi ambao vinaenda kisasa," amesema.


Mkuu huyo wa chuo amewataka vijana kulinda amani ya nchi na wasidanganyike kwa lolote kwani watashindwa kutimiza ndoto yao.


Amesema chuo hiki kinamuenzi Mwalimu Julius Nyerere kwa vitendo, hivyo natamani kuona wanafunzi wanakengeuka na kwenda kinyume 


Aidha, Profesa Mapesa ametoa vyeti kwa wahitimu waliofanya vizuri zaidi katika kila kozi.


Mkuu wa chuo amesema wamepokea changamoto ikiwemo uratibu wa baraza la chuo ambapo ameahidi kuwepo mratibu.


Amesema mratibu atahakikisha uchaguzi unafanyika kwa haraka, kuweza kuendesha mambo kwa weledi na wakati.


"Haya ambayo nimesema yanaenda kutekelezwa kwa kasi ya 5G kwani dhamira yetu ni kuhakikisha chuo chetu kinafanya vizuri," amesema.


Profesa Mapesa amesema dhamira yake ni kuona kila kusanyiko linakuwa na mkutano mkuu ambao utaweza kujadilia mambo ya chuo kwa kina.


Amesema pia watahakikisha kunakuwepo na mifumo rasmi ambayo itafanyika kikatiba baraza hilo litakuwa limepiga hatua kubwa na kusaidia chuo.


Katibu wa Kusanyiko la Wahitimu, Jumanne Muruga alipokipongeza chuo kuongeza program hadi kufikia 50, huku idadi ya usajili wa wanafunzi ikiongeze siku hadi siku.


"Kwa sasa MNMA inasajili kwa mwaka zaidi ya wanafunzi 12,197, hii ni hatua kubwa sana ni ushahidi kuwa chuo kimekuwa," amesema.


Muruga alipongeza uamuzi wa chuo kushiriki kikamilifu kwenye michezo hali ambayo inatangaza chuo kitaifa na kimataifa.


Kupitia kusanyiko hilo Katibu huyo aliomba chuo kuweka ofisi ya mratibu wa baraza la wahitimu na kufanyika uchaguzi wa viongozi wapya kwani waliopo wamehudumu kwa muda mrefu.


Kwa upande wake Mtoa Mada katika Kusanyiko hilo, Dk Ahmed Sovu amesema MNMA inamejipaga kuwa kitovu cha teknolojia hapa nchini.


Dkt Sovu amesema dhamira ya chuo ni kuona vijana wanaohitimu wanaenda kuleta mabadiliko yao, jamii na nchi kwa ujumla.




0 Comments:

Post a Comment