Miili ya Mateka Wanne Waliyotekwa na Hamas Yarejeshwa Israeli

 

Miili ya mama aliyefahamika kwa jina Shiri Bibas na wanawe, wawili Ariel na Kfir, na mateka mwingine Oded Lifshitz aliyekuwa na umri wa miaka 83 wakati akitekwa nyara, imeachiliwa kutoKa Ukanda wa Gaza    katika hafla iliyofanyika kwenye eneo la zamani la makaburi ya mji wa Khan Yunis.


Rais wa Israel, Isaac Herzog, ameelezea majonzi ya taifa nzima baada ya miili ya wanne waliochukuliwa mateka na Hamas katika shambulio la tarehe 7 Oktoba 2023 kurejeshwa Tel Aviv. Miili hiyo inasemekana kuwa ni ya mama na watoto wawili kutoka familia ya Bibas pamoja na Oded Lifschitz, mzee wa miaka 84 na mwanaharakati wa amani.


Herzog aliongeza kuwa: "Hakuna la kusema," akionyesha huzuni na kutaka radhi kwa kutoweza kuwafikisha salama. 


Aliandika kupitia mtandao wa kijamii wa X: "Nawaomba msamaha wanne hawa kwa kutoletwa nyumbani salama."


Kwa upande mwingine, familia ya Bibas ilieleza kuwa "imekumbwa na msukosuko," na kusisitiza kwamba "hadi tutakapopata uthibitisho wa uhakika, safari yetu haijaisha." Hii ni mara ya kwanza kwa Hamas kurudisha miili ya mateka waliofariki tangu kuanza kwa usitishaji mapigano mwezi uliopita. 

Israel inasema itathibitisha utambulisho wa miili hiyo baada ya uchunguzi wa kitaalamu.

Hamas ilisema miili hiyo ni ya familia ya Bibas na Lifschitz, ambao hatima yao imekuwa na athari kubwa kwa taifa la Israeli. 


Afisa wa Msalaba Mwekundu alionekana kutia sahihi nyaraka kwenye meza pamoja na wapiganaji wa Hamas kabla ya miili hiyo kuwekwa kwenye magari ya Msalaba Mwekundu kwa ajili ya usafirishaji.

0 Comments:

Post a Comment