Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo Abdul Nondo Atekwa, PolisiWahfuangua jalada Uchunguzi Unaendelea



Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya chama cha upinzani cha ACT Wazalendo, Abdul Nondo, amerepotiwa kutekwa asubuhi ya leo, Disemba 1, 2024, na watu wasiojulikana alikokuwa katika mkoa wa Kigoma, akiwa na viongozi wengine wa chama hicho. 


Viongozi hao walikuwa wakiongoza kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024, katika mikoa ya magharibi mwa Tanzania.


Taarifa za kutekwa kwa Nondo zimetolewa na ACT Wazalendo kupitia taarifa kwa umma iliyosainiwa na Naibu Katibu wa haki za binadamu na vyombo vya uwakilishi wa wananchi. 


Taarifa hiyo inasema kuwa Nondo aliwasili katika kituo cha basi cha Magufuli, eneo la Mbezi jijini Dar es Salaam, kwa usafiri wa basi la Saratonga lenye namba za usajili T221 DKB. 


Hata hivyo, alitekwa na watu wasiojulikana waliokuwa wakiwa na gari lenye usajili T 249 CMV, aina ya Landcruiser rangi nyeupe.


Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa kutekwa kwa Nondo kulikuwapo na purukushani, ambapo mkoba wake wa nguo na pingu iliyokuwa ikibebwa na mmoja wa watekaji zilidondoka. Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo, mkoa wa Dar es Salaam, Monalisa Ndala, na Afisa Harakati na Matukio Taifa, Wiston Mogha, waliokuwa wamefika mapema katika kituo hicho, walitambua haraka kuwa mtu aliyetekwa ni Abdul Nondo baada ya kugundua nguo zake kwenye mkoba uliodondoka pamoja na notebook yake.


"Tulifanikiwa kutambua kuwa aliyetekwa ni Abdul Nondo kwa sababu tulizitambua nguo zake kwenye mkoba uliodondoka pamoja na notebook yake," alieleza Monalisa Ndala.



Kwa upande mwingine, Jeshi la Polisi limezungumza kuhusu tukio hili kupitia taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David A. Misime. Polisi wamesema kuwa katika majira ya saa 11 alfajiri ya leo, Disemba 1, 2024, walipokea taarifa kuhusu mtu mmoja mwanaume ambaye alikamatwa kwa nguvu na kuchukuliwa na watu waliokuwa wakitumia gari la Landcruiser lenye usajili T 249 CMV.


"Polisi imesema mashuhuda walieleza kuwa vitu vilivyodondoshwa kutoka kwa begi dogo vilivyokuwa na vitu vya Abdul Omary Nondo," alisema David A. Misime. Polisi wamesema uchunguzi kuhusu tukio hili umeanza mara moja na jalada limefunguliwa.


ACT Wazalendo inaendelea kufuatilia taarifa zaidi kuhusu tukio hili na imezitaka mamlaka husika, hasa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camillus Wambura, kuhakikisha kuwa Abdul Nondo anachukuliwa hatua za haraka na anaachiwa huru.


"ACT Wazalendo inatoa wito kwa Jeshi la Polisi kufuatilia haraka tukio hili na kuhakikisha kwamba Bw. Nondo anaachiwa huru mara moja," alisema taarifa hiyo kutoka kwa chama hicho.


Hili linajiri wakati tukio la karibuni la utekaji lililotokea mwezi Septemba mwaka huu, ambapo aliyekuwa mjumbe wa sekretarieti ya Chadema, Ally Kibao, alitekwa na baadaye kuuawa jijini Dar es Salaam. Tume ya Uchunguzi ya ACT Wazalendo imetaka uchunguzi wa kina ufanyike ili kuhakikisha haki inatendeka.


Jeshi la Polisi limeahidi kuendelea kufuatilia na kutoa taarifa zaidi wakati uchunguzi ukikamilika.

0 Comments:

Post a Comment