Mkuu wa Kurugenzi Kuu ya Jeshi na Naibu Mkuu wa Majenerali, Jenerali Vadym Shamarin, amekamatwa, hii ikiwa ni mara ya nne kwa mwezi mmoja kuwakamata maafisa wa ngazi ya juu nchini Urusi.
Shamarin anashukiwa kupokea hongo, hatua ambayo inaendeleza jitihada za kukabiliana na ufisadi ndani ya idara za serikali.
Kukamatwa kwake kunafuatia kesi za awali dhidi ya maafisa wengine wa juu, akiwemo Naibu Waziri wa Ulinzi Timur Ivanov, ambaye alikamatwa Aprili 24.
Wachambuzi wa mambo wanaamini mabadiliko haya yanaweza kusababisha mageuzi katika sera za jeshi, hasa katika suala la mawasiliano, baada ya mchanganyiko wa masuala ya ufisadi na ubora duni wa mifumo ya mawasiliano kuletwa mwangani.

0 Comments:
Post a Comment