Korea Kaskazini Yaangusha Maputo 260 Nchini Korea Kusini

Korea Kaskazini Yaangusha Maputo 260 Nchini Korea Kusini



Korea Kaskazini imeangusha takriban maputo 260 yaliyokuwa yamebeba takataka maeneo ya Korea Kusini, na kusababisha mamlaka kuwaonya wakazi wake kusalia majumbani.


Jeshi la Korea Kusini pia lilionya umma dhidi ya kugusa maputo meupe na mifuko ya plastiki iliyowekwa ndani yake kwa sababu ina "uchafu na takataka".


Puto hizo zimepatikana katika majimbo manane kati ya tisa nchini Korea Kusini na sasa yanachambuliwa.


Korea Kaskazini na Kusini zimetumia puto katika kampeni zao za propaganda tangu Vita vya Korea katika miaka ya 1950.


Awali jeshi la Korea Kusini lilikuwa limesema linachunguza iwapo kulikuwa na vipeperushi vyovyote vya propaganda za Korea Kaskazini kwenye puto hizo.


Tukio la hivi majuzi linawadia siku chache baada ya Korea Kaskazini kusema italipiza kisasi dhidi ya "kutawanywa mara kwa mara kwa vipeperushi na takataka nyingine" katika maeneo ya mpaka na wanaharakati Kusini.


"Siku ya Jumanne usiku, wakaazi wanaoishi kaskazini mwa mji mkuu wa Seoul na katika eneo la mpaka walipokea jumbe za maandishi kutoka kwa mamlaka ya mkoa wao zikiwataka "kujizuia na shughuli za nje". Pia waliombwa kuandikisha ripoti katika kituo cha kijeshi kilicho karibu au kituo cha polisi ikiwa wataona "kitu kisichojulikana"."

0 Comments:

Post a Comment