IAA KUHAKIKISHA MATOKEO YA TAFITI YANAWAFIKIA WANANCHI

 




 CHUO cha Uhasibu Arusha, (IAA), kimezindua kitengo maaluma cha kuhariri na kuchapisha vitabu na machapisho ya kielimu, (IAA PRESS Unity).



Uzinduzi huo umefanyika  Mei 12, 2021 chuoni hapo ambapo mgeni rasmi alikuwa ni  Mkurugenzi wa Utawala na rasilimaliwatu toka Wizara ya Fedha na mipango , Michael John.

Amesema kuwa uzinduzi huo umekuja muafaka kwani kwa muda sasa kumekuwa na changamoto ya kupata taarifa za kielimu zinazazotokana na tafiti kwani mara nyingi zimekuwa zikiishia kwenye makabati mara baada ya tafiti kufanyika na kukamilika. Lakini pia changamoto nyingine imekuwa katika upatikanaji wa vitabu vya ngazi mbalimbali za kielimu.



"Leo tuko hapa kushuhudia kuanzishwa kwa press unity, chimbuko la maarifa kwa maana kuwa tafiti zitafanyika, lakini pia zitahaririwa kuchapwa. Kisha kuhakikisha maarifa hayo yanawafikia watu wengi hivyo kuchangia katika  maendeleo ya nchi yetu," amesema Michael na kuongeza.


"Vitabu vingi vimekuwa vikitoka nje ya nchi hivyo kukosa uhalisia wa kwetu na hata vichache vya ndani vimekuwa na tatizo ya kiuandishi na kuwa na viwango duni katika maudhui na muonekano,".

Michael aliwapongeza IAA kwa kuamua kutatua changamoto hiyo jambo alilodai kuwa anatumaini kuwa wataitendea haki sekta hii kwa kutoa machapisho yenye ufasaha yatakayoleta chachu ya maendeleo katik nchi yetu.
Wakufunzi, wafanyakazi na wanachuo wa IAA wakifuatilia uzinduzi huo



"Serikali kupitia wizara ya fedha na mipango iko nanyi wakati wote na itajitahidi kufanya kila liwezekanalo kufanya IAA ni miongoni mwa vyuo vyenye hadhi bora sio tu Tanzania bali kimataifa," amesisitiza Mkurugenzi huyo wa Utawala na rasilimali watu wa wizara ya Fedha na Mipango.


Awali mkuu wa Chuo hicho, Prof. Eliamani Sedoyeka amemweleza mgeni rasmi kuwa wameanzisha kitengo hicho ili kuhakikishs matokeo ya tafiti yanawafikia walengwa kwa wakati.

"Kwenye matazamio ya elimu, kilele cha taasisi yoyote ni katika kutengeneza na kusambaza ujuzi na maarifa kwa maana ya kwamba tumefundisha na kufanya tafiti. Mwisho wake ni kutoa kwa mlaji kuwa tumefanya tafiti na matokeo yake yanasema hivi," amesema Prof Sedoyeka na kuongeza

"Kwa taasisi yoyote ya elimu ya juu kilele cha mafanikio ni kufanya  utafiti, ukaweza kutengeneza maarifa mapya na ukaweza kuyasambaza kwa jinsi rahisi iweze kuwafikia wale wanaoweza kuitumia,".
Mkuu wa Chuo IAA, Eliamani Sedoyeka


Prof. Sedoyeka amesema kuwa wamefanya badiliko la kimfumo na kisera ndani ya IAA ambaoi wanafunzi wote wa uzamili hatavaa joho bila kuchapisha tasnifu (dessertation) zao.

"Sio tu inatusaidia kusimamia ubora wa hiyo dissertation bali itasaidia matokeo ya huo utafiti uliofanyika kuwafikia watu wengi zaidi," amesema Prof Sedoyeka na kuongeza. 

"Tumezoea tafiti nyingi zinaishia kwenye makabati. Ukijitahidi sana sana itaenda maktaba. Sasa tunajitahidi tafiti hizo zionekane kwa wananchi,"

 "Mwaka huu tunategemea kuwa na wanafunzi zaidi ya 200 wanaofanya 'masters' . Wote hao hawatahitimu bila ku'publish'. Lazima tutoe 'good publication' sio tu "publication',".

Wakufunzi, wafanyakazi na wanachuo wakifuatilia uzinduzi huo


Mkuu huyo wa Chuo, amesema kuwa tayari wameshafanya mazungumzo na Taasisi ya Elimu Tanzania, (TET) zm ao wao ndiyo  wanasimamia mitaala na machipisho ya vitabu kwa shule za awali, msingi na sekondari na vyuo vya ualimu hapa nchini.

"Kuna uhitaji mkubwa sana wa vitabu na sisi hapa tuna waalimu wabobezi kwelikweli kwenye maeneo yaleyale vitabu vinahitajika.Kwa sisi kuwa na IAAPRESS tutakwenda kuwa na uhakika si kwa mahitaji ya shule tu lakini kwa mahitaji ya nchi na ndiyo eneo tumejipanga kujikita,' amesisitiza Prof Sedoyeka.

0 Comments:

Post a Comment