TUENDELEE KUYAENZI MAZURI YALIYOFANYWA NA HAYATI BALOZI DKT. DIODORUS KAMALA.

 TUENDELEE KUYAENZI MAZURI YALIYOFANYWA NA HAYATI BALOZI DKT. DIODORUS KAMALA.



Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Africa Mashariki Wakili Stephen Byabato(Mb) amewahimiza wananchi wa wilaya ya Missenyi kuendelea kumuombea Marehemu Balozi Dkt. Diodorus Kamala aliyetangulia mbele ya haki na kumshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha aliyoishi hapa Duniani.



Wakili Byabato amesema hayo wakati akitoa salamu za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia kifo cha  Balozi Diodorus Kamala ambapo amesema kuwa ameleta salamu za pole kutoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuondokewa na kiongozi mahiri na shupavu aliyewahi kuhudumu katika nyadhifa mbalimbali kwa nyakati tofauti tofauti kwenye serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 


Ameongeza kuwa pia ameleta salamu za pole kutoka kwa wasaidizi wa, Rais akiwemo Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu Dkt. Dotto Biteko pamoja na Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba ambaye alitamani kuwepo lakini hakuweza kujumuika nao kutokana na majukumu aliyoagizwa, Viongozi hao wote wamemtuma afikishe salamu za pole kwa Mke wa Marehemu, Watoto Ndugu na wanakagera wote kwa ujumla.



Wakili Byabato amesema kuwa Balozi Dkt. Kamala alikuwa mwanafamilia katika  Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Africa Mashariki ambapo alitumia kipaji chake kutumikia Taifa la Tanzania kwa nguvu zake zote na uzalendo mkubwa kwa kusimamia masirahi ya Taifa na pale alipokabidhiwa jukumu la Kitaifa alilifanya kwa moyo wote kwa kutumia elimu yake na karama yake ya uongozi kushauri katika maswala mbalimbali.



"Marehemu Balozi Dkt. Diodorus Kamala aliteuliwa na Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Rais mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Naibu Waziri wa ushirikiano wa Africa mashariki mwaka 2005 mpaka 2008 na baadae aliteuliwa kuwa Waziri wa ushirikiano wa Afrika mashariki kuanzia mwaka 2008 mpaka mwaka 2010"


Aidha amesema kuwa watamkumbuka kwa mengi ikiwa ni pamoja na jinsi alivyosimamia kidete msimamo wa Tanzania kuwa swala la Ardhi ya Tanzania au nchi nyingine lisiingizwe katika itifaki ya soko la pamoja pia kusimama na  kuhakikisha ujenzi wa Jengo la makao makuu ya Jumuhiya ya Africa Mashariki unaanza, linajengwa na kukamilika kwa viwango vinavyostairi ambapo mpaka sasa linatumika.

0 Comments:

Post a Comment