
Lengai Ole Sabaya akikumbatiana kwa furaha na mama yake mara baada ya Mahakama ya Rufaa Nchini kutupa rufaa ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini, (DPP)
ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili wameshinda kesi ya rufaa waliyokatiwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, (DPP) baada ya Mahakama ya Rufaa kusema hakuna ushahidi wa ujambazi wa kutumia silaha wala kundi uliothibitishwa kwenye kesi ya msingi.
Aidha mahakama hiyo ya juu nchini, ilibatilisha na kufuta maelezo ya awali na mwenendo wa Shahidi wa pili, Noman Jasin huku ikieleza kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilikosea kubatilisha na kufuta maelezo ya awali na mwenendo wa shauri lote na kuwaachia huru warufani wote baada ya kubaini shahidi huyo hakuhojiwa na mawakili wa wajibu rufaa wa pili na watatu katika kesi ya msingi.
Uamuzi huo wa majaji watatu wa mahakama ya rufaa wakiongozwa na jaji, Jacobs Mwambegele, Ignas Kitus na Leila Mgonya umesomwa leo Novemba 17,2023 kwa saa 1.10 na Naibu Msajili wa Mahakama Rufaa Nchini, Abeesiza Kalegeya kwenye mahakama kuu kanda ya Arusha.
Kalegeya ambaye awali alipanga kusoma uamuzi huo saa tatu kamili asubuhi lakini alikuja kuusoma saa 7.30 mchana alieleza kuwa mahakama ilifikia uamuzi wa kutupilia mbali rufaa hiyo baada ya kupitia hoja za pande zote na kujiridhisha kuwa kulikuwa na mapungufu ya kisheria.
"Mahakama imeona hata ilipobadilishwa kutoka kutoka unyanganyi wa kutumia silaha kwenda kwenye kosa la kundi makosa hayo hayakuthibitishwa na haingefaa kwa sababu makosa yote yana adhabu zinazolingana,"alieleza Kalegeya wakati akitangaza kutupa rufaa hiyo na kuongeza.
"Hii rufaa imetupwa, Maamuzi yaliyotolewa na mahakama kuu Arusha (mahakama ya rufaa ya kwanza) hayawezi kubatilika na rufaa hii inatupiliwa mbali,".
Hivyo kwa uamuzi huo wajibu rufaa, Sabaya ambaye alikuwa mahakamani hapo na wenzake Silvester Nyegu na Danie Mbura wanaendelea kuwa huru.
Awali Naibu Msajili huyo wa Mahakama ya Rufaa Nchini alirejea hukumu iliyotolewa Mei 6, 2023 na Mahakama kuu Arusha iliyotokana na kesi ya jinai
https://draft.blogger.com/blog/post/edit/496674253964308653/4916419568569067909
https://habaritanzaniagracemacha.blogspot.com/2022/05/sabaya-na-wenzake-waachiwa-huru.html
0 Comments:
Post a Comment