HIKI HAPA CHANZO KIFO NA WASIFU WA ZALOTHE,

Rais Samia Suluhu Hassan akitoa Heshima za mwisho kwenye Jeneza la Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha Kamishna Mstaafu Marehemu Zelothe Stephen Zelothe wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Oktoba, 2023


FAMILIA ya Kamanda wa jeshi la polisi Mstaafu na mwenyekiti wa CCM Mkoani Arusha, marehemu Zelothe Stephen Zelothe wametoa ratiba ya maziko ya mpendwa wao huku wakieleza kuwa kifo mpendwa wao huyo kimetoka na saratani ya tumbo.

Samia Suluhu Hassan akizungumza na  Flora Zelothe Mjane wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha Kamishna Mstaafu Marehemu Zelothe Stephen Zelothe wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Oktoba, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia Kifo cha Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha Kamishna Mstaafu Zelothe Stephen Zelothe Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Oktoba, 2023




Sehemu ya taarifa hiyo inasema,"Marehemu alianza kuugua mwezi wa Julai/Saba, hali iliyosababisha kupelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu na ikagundulika kuwa alikuwa na saratani ya tumbo.

"Alitibiwa huko na kurudi nyumbani/Tanzania na kupangiwa tarehe ya kurudi mwezi Septemba, kwa wiki tatu. Baadaye alirudi nyumbani mwezi Oktoba, kuendelea na matibabu katika hospitali ya EMMH.".





WASIFU MFUPI WA MPENDWA WETU 
SACP (RTD) ZELOTHE STEPHEN ZELOTHE

Ndugu Zelothe Stephen Zelothe alizaliwa tarehe 30 November 1950 katika Kijiji cha Ilkiranyi katika wilaya ya Arumeru (sasa Arusha), Mkoani Arusha, akiwa mtoto wa pili katika familia ya Stephen Oldarasu na Dina Oldarasu yenye watoto tisa (9). Watano (5) wa kiume na wanne (4) wa kike.

Imani

Mpendwa wetu Stephen Zelothe alibatizwa na alipata Kipaimara mwezi Desemba mwaka 1967 katika kanisa la KKKT Olosiva, wilaya ya Arusha, Mkoani Arusha.

Elimu

Bw. Stephen Zelothe alimaliza elimu ya msingi katika shule ya Mringa, wakati huo Mringa Upper Primary School, mwaka 1966. Baada ya hapo alijiunga na Elimu ya Sekondari katika Shule ya Enaboishu, Mkoani Arusha, na kuhitimu kidato cha nne (4) mwaka 1968. 

Baada ya hapo, Stephen Zelothe alijiunga na chuo cha mafunzo ya Jeshi la polisi katika chuo cha mafunzo ya polisi Moshi, Police Training School. na kuhitimu mwaka 1970. 

Aliendelea na mafunzo mbalimbali nchini Tanzania ikiwemo ya Usalama 
Barabarani, Uongozi, Mafunzo ya Kupambana na Uhalifu. Pia alichukua mafunzo nchi za nje ikiwemo Japan mwaka 1998 na 2000, Marekani (mwaka 2001 na 2007), Ujerumani (mwaka 2005) na Uingereza (mwaka 2008).

Kazi
Mwaka                  Nafasi                              Mahali 
1970-1977 Police General Duties:Kazi za kawaida-Police Constable Morogoro
1977-1978 Police Instructor: Mkufunzi katika Jeshi la polisi Usalama Barabarani-
Makao Makuu
1978-1990 Research and Training In-charge: Mkuu wa utafiti na mafunzo
Usalama Barabarani -Makao Makuu
1990-1997 Police Officers Instructor: Mkufunzi wa maofisa wa Jeshi la polisi
Chuo cha Maofisa wa Polisi 
1997-2000 Officer Commanding the District: Mkuu Mbeya na Mbarari 19
wa polisi wilaya (OCD)
2000-2002 Staff Officer Operations: Kiongozi wa operesheni katika ngazi ya mkoa
Dar es salaam
2002-2003 Staff Officer: Afisa Mnadhimu wa Mkoa Dar es salaam
2003-2008 Regional Police Commander: Kamanda wa Polisi Mkoa ( RPC)
Mwanza
2008-2009 Regional Police Commander: Kamanda wa Polisi Mkoa ( RPC) 
Mbeya
2009-2012 Regional Police Commander: Kamanda wa Polisi Mkoa ( RPC)
Dodoma
2013 Advisor and couching Police: Mshauri wa polisi Makao makuu
Makao makuu Jeshi la polisi 
2013-2014 Regional Police Commander: Kamanda wa Polisi Mkoa
Mtwara
2014-2015 Chief of Inspections: Mkuu wa Ukaguzi makao makuu
Makao Makuu Jeshi la Polisi
2015-2016 District Commissioner: Mkuu wa Wilaya Musoma - Mara
2016 - 2018 Regional Commissioner: Mkuu wa Mkoa Rukwa
2019 – 2023 CCM Regional Chairman: Mwenyekiti wa CCM Mkoa
Arusha


Ukulima na Ufugaji
Mpendwa wetu kamanda Stephen Zelothe alipenda kujishughulisha na kilimo, ikiwa sehemu ya shughuli alizozipenda na kuzifanya wakati wote wa maisha yake. Alilima katika maeneo ya Lolkisalie, Lemooti na Naberera Wilayani Simanjiro Manyara na Arusha alipokuwa anaishi. Aliendelea na kazi ya kilimo hadi umauti yalipomkuta.

Ndoa
Ndugugu Zelothe Stephen Zelothe alioa tarehe 7 Januari 1984 na alijaliwa kuwa na Watoto watano (5), wanne (4) wa kiume na mmoja (1) wa kike. Alikuwa pia na mtoto mmoja (1) wa kulea. Marehemu alijaliwa kuwa na wajukuu wanane (8).

Sifa zake katika familia
Marehemu alikuwa ni mtu mnyenyekevu, anayependa ndugu, jamaa na marafiki.Marehemu aliwalea vijana na ndugu wengi katika ngazi ya familia, ukoo, Kijiji na hata katika ngazi za kitaifa pale alipokuwa katika majukumu yake ya kazi. 
Katika malezi 20 yake Marehemu aliweza kusaidia na kufanikisha maisha ya wale ambao aliwasaidia kuweza kufikia ndoto zao kwa kufikia ngazi mbalimbali za kitaifa na kimataifa. 

Wale ambao amewasaidia na kuwalea wameweza pia kufika katika viwango mbali mbali vya elimu, na vyeo katika mashirika ndani na nje ya nchi na pia kufika katika ngazi mbali mbali kwenye siasa na uongozi katika taasisi mbalimbali za serikali.

Ugonjwa 
Marehemu alianza kuugua mwezi wa Julai/Saba, hali iliyosababisha kupelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu na ikakundulika kuwa alikuwa na saratani ya tumbo. 

Alitibiwa huko na kurudi nyumbani/Tanzania na kupangiwa tarehe ya kurudi mwezi Septemba, kwa wiki tatu. Baadaye alirudi nyumbani mwezi Oktoba, kuendelea na matibabu katika hospitali ya EMMH hadi mauti yalipomkuta.

Shukrani 
Familia inapenda kuwashukuru wote waliomsaidia na kuisaidia familia katika kipindi chote cha kuugua hadi kifo, ni ngumu kumtaja kila mtu lakini tunawaomba wote mpokee Shukran zetu.

Kipekee famili inapenda kutoa Shukran za dhati kwa Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amemsaidia sana Mzee wetu kutoka ugonjwa, matibabu nchini na nje ya nchi; hakuchoka ameendelea kutukimbilia kwenye msiba na ametoa ndege iliyomleta Mzee Arusha. Kwake tumeona upendo mkubwa sana. 

Familia inamshukuru Makamu wa Rais Dr Phili Isidory Mpango, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Daniel Chongolo, Inspekta Jenerali wa Polisi Camilius Wambura,ATCL, CCM, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, madaktari na wauguzi wa Hospitali za KD na HCG India, Mzena Dar es Salaam, Hospitali ya Jeshi Lugalo Dar, Mount Meru, Viongozi wa KKKT Azania Front Dar es salaam, Viongozi wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Jimbo la Arusha Magharibi na Usharika wa Olosipa.

Ni ngumu kumtaja kila mmoja, lakini tunaomba sana wote mpokee Shukran zetu. Tunamwomba Mungu awabariki sana na mundelee na upendo huo.
“BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe”
(Ayubu 1:21b)


0 Comments:

Post a Comment