EWURA YAHIMIZA WAFANYABIASHARA WA MAFUTA KUWA NA MIKATABA NA WAUZAJI WAKUBWA

MAMLAKA ya udhibiti wa huduma za  nishati na maji, (EWURA) imewashauri wafanyabiashara  binafsi  wanaouza  mafuta ya vyombo vya moto kuingia mikataba na   wafanyabiashara wakubwa  wanaoagiza mafuta nje.

Imeelezwa kuwa hiyo itasaidia taasisi hiyo kufuatilia madai yao kuwa makampuni hayo makubwa yanawanyima mafuta jambo linalosababisha  tatizo la ukosefu wa mafuta kwenye vituo  vyao na wananchi kuteseka





Meneja wa EWURA kanda ya kaskazini, Lorivu Lon'gidu ameyasema hayo leo Septemba 12,2023 wakati akiongea na wafanyabiashara   binafsi  wa mafuta  katika kikao kazi kilichoandaliwa na EWURA kikiwa na lengo  la  kukumbushana taratibu za ufanyaji biashara ya uuzaji wa mafuta.


Amesema kuwa kikao hicho kimeandaliwa kwa ajili ya kuweza kuwakumbusha wafanyabiashara hao wajibu wao wa kuwauzia wananchi mafuta bila kubagua na kufuata taratibu na sheria.

"Kuwa  kunabaadhi ya wafanyabiashara wamekuwa hawafuati taratibu na sheria za ufanyaji wa biashara ya mafuta," amesema Long'idu na kuongeza.

...Ila pia tumewataka wafanyabiashara hawa kuwa na mikataba na waagizaji mafuta lengo la mikataba hii ni kuhakikisha upatikanaji wa mafuta,".

"Kwa sababu hawa waagizaji mafuta wakubwa  wanatabia moja, wanapoagiza mafuta lazima wajue hayo mafuta wanamuuzia nani, kuna wanyabiashara ambao wanamikataba na sisi wametupa tunayo ilituweze kufatili  lakini kuna wafanyabiasha bado hawana mikataba  na wengi wao ndio wanakosa mafuta na kuanza kulalamika,". 

"Mikataba hii ni kwa ajili ya kuhakikisha bidhaa ya mafuta inapoagizwa na hawa wafanyabiashara wakubwa kujua wanakwenda kuwauzia wafanyabiashara binafsi Kwa utaratibu gani ,ili huduma ya mafuta iweze kuwafikia wananchi  Kwa wakati na maeneo ya mbali zaidi,".


Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabishara ws Mafuta, (TAPSOA), mkoani Arusha, Ali Fivestar amesema kuwa suluhisho la tatizo lamukosefu wa mafuta ni maafisa wa EWURA kuweka mazingira wezeshi ya ufanyaji biashara hiyo.

"Nasema hivi EWURA watoke ofisini waweke mazingira wezeshi hii adhaa yote itaisha.Jawabu ndiyo hiyo.Halafu hata ukiangalia hiyo ankara ya manunuzi imekaa kimkataba,"Ali na kuongeza.

...Tuache uvivu wa kusema sisi ni marefa.Kuwa refa wakati hali ni shwari.Utadhibiti nini endapo mafuta hayapatikani?,".


Ali anasema Mada kuu ya mkutano huo ni  uhaba wa mafuta na wap kutakiwa kuwa mikataba na hao waagizaji wa jumla kwani kwa sasa wanaopata adhaa ya upatikanaji wa mafuta ni wafanyabiashara wadogo.

"Wakati hali ikiwa shwari tulikuwa tunanunua mafuta mahali popote maana tunanunua kwa fedha taslim.Kwa maana tunaweka fedha kwenye akaunti zao fedha zikionekana tunapakia mafuta kwanini iwe kipindi hiki waje na mada ya kuwa na mikataba?," anahoji Ali na kuongeza.

...Kwa kuwa EWURA ni mwangalizi wa pande zote mbili na ndiye anaetoa leseni kwa mwagizaji wa jumla na reja reja na ameweka mfumo unaoitwa NPGIS ambapo kazi kuu ya huo mfumo ni kuingiza mafuta yote yanapokelewa na yanayouzwa na ipo kikanuni na asiye peleka taarifa hizi huwa adhabu ya fine inamkabili wasimamie hilo shida ya mafuta itaisha,".

Wafanyabiashara binafsi  wengine waliouthuria kikao hicho wamesema kuwa kunabaadhi yao  wanamikataba   na wafanyabiashara hao wakubwa lakini wamekuwa wakikosa  huduma ya mafuta ,huku wengine wakizungushwa kupata mafuta hayo  na wengine  wakiambiwa walipe fedha mara mbili.

"Unakuta mimi nimelipia mafuta leo kwa uyo mfanyabiashara mkubwa  na nina mkataba lakini cha kushangaza  nikitaka mafuta nazungushwa  muda mwingine naambiwa niongezee fedha mafuta yamepanda lasivyo nirudishiwe fedha," amesema Michael Masanja mfanyabiashara binafsi kutoka Tanga na kuongeza 


 ...Unakuta kuna mtu anataka nitoe cha  juu ili nipate  ukiangalia  kituo changu cha mafuta  akina  mafuta , mkuu wa mkoa anakuja anajua nimeficha mafuta, toyo ambazo ndio wateja wetu wakubwa wanakuja wanataka kunitoa roho," .

Masanja ameiomba serikali kukaa na wafanyabiashara wakubwa wanaoagiza mafuta   kupanga bei ambayo itakuwa hamnyimi faida muagizaji na ambayo haita muumiza mwananchi  kwani kwa sasa hivi bei iliopangwa  inamuumiza muagizaji na ndio maana baadhi yao hawauzi mafuta kwa wafanyabiashara ambao ni binafsi Kwa kukwepa hasara.




0 Comments:

Post a Comment