MCHENGERWA AZIPA MAJUKUMU KAZITO BODI ZA TTB NA TANAPA




WAZIRI wa Maliasili na Utalii,  Mohamed Mchengerwa ameitaka Bodi mpya ya Wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), kwenda kuondoa utendaji wa mazoea ili kuweka misingi ambayo itaifanya Tanzania kuwa namba moja Afrika na dunia katika sekta ya utalii.



Aidha, ameiagiza Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania, (TANAPA) kuendelea kusimamia mfumo wa kijeshi ili kuweza kufikia malengo ya kuanzishwa kwake hususani katika eneo zima la uhifadhi wa rasilimali za Wanyamapori na Misitu katika maeneo ya hifadhi zote. 



Waziri Mchengerwa ametoa maagizo hayo leo, Agosti 21, 2023 jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa hizo ambao pia Naibu waziri wa wizara hiyo Masanja alikuwepo.



Waziri Mchengerwa ameiagiza Bodi ya TTB kukaa na Menejimenti ili kufanya mapitio ya Sheria ili kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya utalii sanjari na kutatua mara moja changamoto zilizopo na kusimamia mikakati ya uwekezaji katika maeneo mbalimbali ambapo amefafanua kuwa idadi ya vivutio vilivyopo nchini hailingani na mapato yanayopatikana.

Aliitaka bodi ya utalii Tanzania kujipanga kikamilifu ili kuongeza idadi ya watalii ukizingatia kwamba idadi ya watalii 6000 wa sasa ni ndogo ukizingatia  ukubwa wa nchi, wingi wa hifadhi pamoja na vivutio vilivyopo haviendani na idadi hiyo ya watalii.



Aliitaka bodi hiyo ya utalii kufanyakazi usiku na mchana kujiboresha na kuondokana na utendaji wa mazoea ili kwenda na kasi ambayo rais Samia anaihitaji ya kutangaza vivutio na kuongeza idadi ya watalii nchini.

"Huko nyuma kupitia mitandao ya kijamii wadau wetu wa utalii wamekuwa wakilalamika sana kwamba viongozi wa bodi ya utalii wamekuwa wakisafiri kwa ajili ya kufanya shopping nje ya nchi wakati mwingine tulipata aibu nchini Korea kusini walitengeneza maboksi kutangaza utalii wa Tanzania hii ninaibu kubwa"

Ametolea mfano suala la  uwekezaji wa vyumba vya kulala wageni hapa nchini ,alisema kuna vyumba takribani 120,000 kiasi ambacho ni kidogo ukilinganisha na nchi ya Kenya ambayo inavyumba zaidi ya milioni 1.5.



"Tuna kwenda kufanya mapitio ya sheria itakayowapa mamlaka ya kuhakikisha mnaishauri serikali kwenye eneo la uwekezaji na kujua ni namna gani tunakwenda kuongeza idadi ya watalii,kuongeza vyumba vya  kulala watalii na eneo la ukarimu" amesisitiza Waziri Mchengerwa.

Amesema mpango mwingine wa TTB ni kuhakikisha inateka soko la watalii wanaotoka China kwani hivi sasa ni watalii 34,000 tu wanaokuja nchini wakati watalii wanaotoka china kwenda mataifa mbalimbali duniani wanakaribia milioni 200 kwa mwaka, hivyo ni lazima walau watalii milioni 3 kutoka China waje hapa nchini.

Aidha Mchengerwa amesema takwimu zinaonyesha kwamba bado hatujalifikia soko la watalii  wengi duniani hasa kutoka bara la Asia.

“Bila utangazaji madhubuti unaokwenda sambamba na utoaji wa huduma bora kwa watalii, Taifa haliwezi kunufaika na rasilimali za utalii zilizopo nchini hata kama uhifadhi wa rasilimali hizo utaimarishwa,” amesisitiza Mchengerwa na kuongeza

...heshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliamua kutufungulia njia kwa kuanzisha Programu maalum ijulikanayo kwa jina la Tanzania ‘The Royal Tour’’ inayolenga kutangaza vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji. Hivyo, tunao wajibu wa kuhakikisha kuwa Programu hiyo inakuwa endelevu sambamba na kuanzisha mikakati mbalimbali itakayochochea ongezeko la watalii hapa nchini pamoja na mapato yatokanayo na Sekta ya Utalii”.


Hata hivyo amezitaka taasisi hizo  kujikita katika utatuzi wa migongano kati ya binadamu na wanyamapori wakali na waharibifu kwa kuhyakikisha kuwa migogoro yote iliyopo kati ya wananchi na Hifadhi inapatiwa suluhisho la kudumu na kuzuia kutokea kwa migogoro mipya ili uhifadhi endelevu uweze kupatikana.



Kwa upande wake,  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Timetheo Mzava ametoa wito kwa bodi hizo kufanya kazi kwa bidii.



Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TANAPA, Jenerali mstaafu George Waitara, alimshukuru Rais Samia kwa kuendelea kumwamini na kumteua katika kipindi kingine cha tatu kuongoza bodi hiyo.


"Natambua Rais Samia ametuamini na sisi kazi yetu ni kuchapa kazi hatutamwangusha na imani hii tutailinda tunachohitaji kwako ni ushirikiano tu "

Waitara alitoa onyo kwa majangili walioanza kujitokeza ambao aliwaita ni wadokozi kwani kazi kubwa ya kutokomeza ujangili nchini imefanyika hasa baada ya kuzinduliwa kwa jeshi Usu.



Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TTB Balozi, Dkt. Ramadhani Dau alimshukuru Rais kwa kumwamini na kumteua kwenye nafasi hiyo huku akimwahidi Waziri, Mchengerwa kufanya kazi kwa bidii.

0 Comments:

Post a Comment