Awali kabla ya kukamatwa mbunge Shangay, aliwaeleza wandishi wa habari jijini Arusha kuwa alifika kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Arusha, (RCO) kwa ajili ya kujisalimisha lakini akambiwa anatakiwa aende Karatu.
Mbunge huyo alikuwa ameambatana na mawakili wanaomtetea akiwemo, Joseph Oleshangay, Yonas Masyaya, Nicolas Senteu na Ngeyani Orormunyei.
“Leo nimefika kuripoti kwa RCO kama jana (Agosti 20,2023) nilivyofanya mawasiliano na Spika (wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Akson) na Waziri wa Mambo ya Ndani (Hamad Masauni) nimeripoti muda wa saa sita mchana ameniambia suala langu ameliacha kwa Afisa Upelelezi wa wilaya ya Ngorongoro a,mbapo ofisi wameihamishi Karatu,” alisema OleShangay na kuongeza .
…Hivyo ninatakiwa kwenda Karatu kwa ajili ya mahojiano . Lakini suala wanaloenda kunihoji ni la kutengenezwa kwani hata mkiangalia ukiona kuna mabango yameandaliwa kule Kapenjiro hata jina la mbunge lipo lakini ukiangalia mimi tokea nimechaguliwa sijawahi kufika kule,”.
Mbunge huyo alisema kuwa kwenye mabango yao wameandika ‘mbunge anatunyima kuondoka’ jambo alilodai kuwa hilo jambo limejengwa huku akisisitiza kuwa hata hilo tukio la Enduleni hakuwepo ni tukio lililotengenezwa huku akieleza kuwa haelewi nia ya wanaofanya hayo na kwanini watu hao wameamua kunitaja mimi.
Waandishi hao walishambuliwa na wananchi wakiwa mnadani kwenye kijiji cha Enduleni Agosti 15,mwaka huu ambapo video imesambaa mitandaoni ikimuonyesha mmoja wao, Habib Mchange wa Jamvi la Habari akitumia kipaza sauti kuwahamasisha wananchi hao kuhama.
Waandishi wengine walijeruhiwa kwenye tukio hilo na vyombo wanavyofanyia kazi kwenye mabano ni Ferdinand Shayo, (ITV) na Denis Msaky,(Mwandishi wa Kujitegemea).
Akitolea ufafanuzi taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amewakashifu polisi alisema kuwa si kweli kwani video hiyo imekatwa baadhi ya maneno kwani anachokumbuka akiwa kijiji cha Nainokanoka alipokea taarifa ya wananchi wa kijiji hicho pamoja na Nailelai kwamba askari wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,(NCAA) wanawaonea wananchi.
“Nilichosema kwa Kauli yangu kama mbunge Jeshi la polisi linaendeshwa kwa mujibu wa sheria na wanasheria zao, PGO zao wanapoenda kumkamata mtu yeyote kwenye makazi yao wanazifuata,” alisema na kuongeza.
…Hao wengine wanaoenda kuwakamata kwenye makazi yao si jeshi la polisi ninaowafahamu mimi wale nilikuwa nawazungumzia ni ‘rangers’ (askari wa hifadhi) ambao wanaenda kwenye makazi ya watu usiku wanafyatua risasi wakina mama mimba zinatoka ndiyo maanda nikasema hawa ni vibaka kama vibaka wengine ambao wanapswa kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria za jamhuri ya Muungano wa Tanzani,”.
Alisema kmuwa akiongea na wananchi hao aliwaeleza kuwa jeshi la polisi likitaka kwenda kukamata mtu ni lazima wafuate taratibu ikiwemo kuambatana na viongozi wa eneo husika akiwemo balozi na mwenyekiti.
Akielezea namna mbunge Oleshangay alivyokamatwa , Diwani wa Kata ya Elelai ,James Moringe alisema alikuwa ameongozana na Mbunge aliyekuwa anatii maelekezo ya RCO ya kwenda kuripoti kituo cha Polisi Karatu.
Hata hivyo walipofika Karatu eneo la Rhotia walisimamishwa na Polisi ambao walimchukuwa Mbunge huyo katika gari lao.
Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, (RPC) Jastine Masejo hazikuzaa matunda kwani simu yake ilikuwa inaita muda wote bila kupokelewa.
0 Comments:
Post a Comment