MBUNGE WA NGORONGORO AGOMA KULA, AACHIWA KWA DHAMANA,


MBUNGE wa Ngorongoro, (CCM) Emmanuel Oleshangay ameachiwa kwa dhamana majira ya saa mbili leo Agosti 23,2023 usiku ambapo amesema aligoma kula chakula kwa siku tatu alizokuwa mikononi mwa polisi.

Aidha amesema kuwa kwa siku zote hizo alikuwa akishikiliwa kwenye kituo cha polisi cha Kidiplomasia Arusha.

OleShangay amezungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuachiwa kwa dhamana ambapo atatakiwa kuripoti tena polisi siku ya jumatatu.

Wakili wake, Alayce Melau amesema masharti ya dhamana yaliyowekwa na polisi ni kitambulisho na shilingi milioni moja.

Awali muda wote ambao mbunhe huyo amekuwa chini ya mikono wa jeshi la polisi kumekuwa na taharuki hasa baada ya mawakili wake kushindwa kuwasiliana naye huku polisi wakiacha kueleza wanamshikilia kwenye oituo gani cha polisi tokea aliposhikiliwa na polisi tokea Agosti 21,2023.

'Nimeachiwa usiku huu,nililetwe saa nane usiku kutoka Karatu na mpaka hapa hapa kituo cha polisi cha diplomasia," amesema OleShangay na kuongeza

...Kwa siku tatu sijaweza kula chakula na niliamua kutokula kwa sababu haina maana huwezi kulishwa na mtesi wako kwa hiyo nimeamua kutokula na niko salama,".

Alipoulizwa ilijuwa polisi wamkamate wakati alikuwa njia kuelekea kituo cha polisi Karatu kama alivyoelekezwa na RCO alisema kuwa hata yeye suala hilo limemshangaza.

"Ndicho ninachoshangaa kwa sababu nilijua naenda kuwauliza walikuwa wananiitia nini. Lakini nashangaa baada ya kufika eneo la Marera Karatu alikuja afande Feo anaksema yeye ni msaidizi wa RCO," amesema OleShangay na kuongeza.

...Wakaniweka kwenye gari la Hifadhi ya Ngorongoro wakanipeleka  kituoni wakanihoji kwa zaidi ya saa tano nikatoa maelezo yangu lakini baadaye wakili wangu aliambiwa atoke kwa sababu hawajakamilisha taratibu zao lakini baadaye muda wa saa 7: 32 usiku wakaniondoa Karatu  tukafika hapa (Arusha) muda wa saa nane.
 
Mbunge huyo wa Ngorongoro amedai kuwa polisi walipaswa kumtaarifu kwa barua kuwa wanamuhitaji lakini wao walikuwa wakivamia nyumbani kwake jambo alilohoji kuwa walikuwa wanataka nini.

"Ukiwa upande wa wananchi ni lazima upate matatizo na hii hainirudishi nyuma hata mara moja...Nimejifunza kuwa binadamu unaweza kukaa siku tatu bila kula na hautakufa na hata ningekaa siku saba nisingekula na wala nisingekufa" amesema OleShangay.

Amesema kuwa yeye anakinga ya bunge lakini kinachomshangaza polisi ndiyo wanaolinda sheria za nchi hivyo walipaswa kufuata sheria kwa kumwandikia barua spika barua halafu spika ndiyo ampe taarifa jambo ambalo halikufanyika.


Kwa nini hawausubiri mpaka spika atoe barua ninaamini kuna presha za kisiasa lakini mimi ni mwanasiasa nitaendelea kuishi katika siasa.

Mmoja wa mawakili wake, Alayce Melau amesema kuwa mbunge huyo amepewa dhamana na atatakiwa kuripoti kituo cha polisi jumatatu.

"Masharti ya dhamana yalikuwa ni kitambulisho na shilingi milioni na anatuhumiwa kwa makosa ya uchochezi,".ameswma Melau.

Amesema kesi yao ya kutaka aletwe mahakamani itakuwa imeondoka kwa upande wake  ila inaendelea  kwa watu wengine 31 wanaoshikiliwa na polisi Karatu na Manyara.

"Tutaendelea kufuatilia ili kuona namna wote wataweza kuachiliwa," amesema Melau.


Wakati huohuo kamanda wa polisi mkoani Arusha, Justine Masejo naye ameto taarifa yake.



0 Comments:

Post a Comment