WAKILI WA UTETEZI KESI YA SABAYA AJITOA


WAKILI Fridolin Bwemelo amejitoa kuendelea kumtetea mshitakiwa wa tatu, Watson Mwahomange kwenye kesi inayowakabili pamoja na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya na wenzake sita kwa kile alichodai kuwa ana mgongano wa kimaslahi.


Amejitoa Machi 7, 2022 mbele ya hakimu mkazi mwandamizi, Patricia Kisinda anayesikiliza shauri hilo la  Uhujumu Uchumi na Utakatishaji Fedha Namba 27/2021 kwenye mahakama ya hakimu mkazi Arusha.

Bwemelo ameieleza mahakama kuwa ameona akiendelea kumtetea Mwahomange anaweza akajiingiza kwenye mambo ambayo yanaenda kinyume na maadili na  taratibu za mahakama.



"Tumeshindwa kuelewana katika suala zima la mgongano wa kimaslahi ambalo naona naweza akapoteza haki zangu  wakati niimwakilisha au naweza kujiingiza kwenye mambo ambayo yanaenda kinyume na Taratibu za Mahakama kama Afisa wa Mahakama," ameeleza Bwemelo.


Hata hivyo wakili, Bwemelo ameiambia Mahakama kwamba kwa sasa atabaki akimwakilisha Mshtakiwa wa nne, John Odemba.

Kwa upande Wake mshitakiwa,  Mwahomange Watson ameiambia Mahakama kwamba amesikia maombi ya aliyekuwa wakili wake,  Bwemelo na hana pingamizi naye hivyo atajiongoza mwenyewe bila kutegemea wakili.

Mshitakiwa wa tatu, Mwahomange anayejitetea mwenyewe alimuhoji shahidi, Enock Togolani ambaye ni mshitakiwa mwenzake aliyesema kuwa walifahamiana baada ya shauri jilo kufikishwa mahakamani.

" Alikuja shahidi wa 13 hapa mahakamani  akaeleza kuwa mimi  (Mwahomange) mshitakisa watano, Silvester Nyengu, mshitakuwa wasita na wa saba tulipokea mgao wa shilingi milioni 90,." ameuliza Mwahomange 

Togolani akaeleza kuwa Mwahomange kwa mara ya kwanza alimuona mahakamani hapo hivyo hajawahi kugawana naye fedha.

huku akimtaka ajitambulishe majina yake ifuatavyo
Mwahomange: akimuhoji shahidi
Nitakuwa na maswali machache sana kwa shahidi
Ikumbushe mahakama majina yako 
Enock

Watson alikuja hapa mahakamani akasema mimi wewe na washitakiwa wa tatu watano was ista na wa saba no lini tuliwahi kupokea huo mgao wa miliono tisini tukiwa pamoja
S mimi mshitakiwa wa tatu kwa mara ya kwanza nilimuona hapa mahakani jivyo sijawahi 

Mwahomange ; Shahidi wa 13 wa jamhuri alisema mimi na wewe na washitakiwa wengine tulinda genge la uhalifu pamoja
Shahidi; Mheshimiwa hakimu kama nilivyoeleza mimi nimemuona Watson kwa mara ya kwanza hapa mahakamani
Mwahomange; Mara yako ya kwanza uliwahi kuniona wapi
Shahidi; mheshimiwa  hakimu nilimuona hapa mahakamani tarehe 4/6/ 2021 
Mwahomange; Kwa nini TAKUKURU walikuja tarehe 16 gerezani 
Shahidi; Walikuja kuongea na sisi na waliongea na kila mmoja kwa wakati wake na walikuja kuongea na sisi ili watuondoe kwenye mashitaka haya
Mwahomange; na kwa nini walirudi tarehe 20/ 7 /2021
Shahidi; Sijui kwa sababu sikuwaona hao watu wa TAKUKURU kwa sababu mara ya mwisho kuwaona ni tarehe 18/7/2021 kama walirudi walionana na mshitakiwa mwenyewe 
Mwahomange : Mheshimiwa hakimu kwangu ni hayo tu

0 Comments:

Post a Comment