URUSI YATOA MASHARTI KUMALIZA VITA


Urusi imesema kuwa inaweza kusitisha operesheni "wakati wowote" ikiwa Ukraine itatimiza masharti yao.


Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema Ukraine lazima itambue Crimea kama Urusi, na Donetsk na Luhansk kama mataifa huru.


Aidha amesema Ukraine lazima irekebishe katiba yake na kukataa madai ya kuingia katika kambi yoyote (kama vile Nato, kwa mfano).


Peskov amesisitiza kuwa Urusi itamaliza "kuondoa jeshi" kwa Ukraine, na ikiwa masharti haya yatatimizwa hatua za kijeshi za Urusi zitakoma mara moja.


Msemaji huyo wa Kremlin amesema kuwa Urusi haitaki kutoa madai yoyote zaidi ya eneo nchini Ukraine.


Mzozo wa Ukraine: Mfahamu mke wa Rais wa Ukraine Olena Zelenask anayetafutwa na Urusi


Mzozo wa Ukraine:Kitisho cha Yeltsin na makosa mengine ya nyuklia ambayo karibu yangesababisha Vita vya tatu vya dunia

0 Comments:

Post a Comment