RUFAA ya Lengai Ole Sabaya kuendelea kusikilizwa kesho baada ya leo kushindwa kuendelea baada ya wakili, Majura Magafu anayeongezeka jopo la mawakili wa utetezi kuomba muda wa kupitia vielelezo vilivyowasilishwa kwenye shauri la msingi ili waweze kujiandaa na usikilizaji wa rufaa hiyo.
Aidha, Mahakama imesema haiwezi kuahirisha usikilizwaji wa shauri hilo mpaka jumatatu ijayo kwani mshitakiwa wa kwanza ana mawakili wengine wanaomwakilisha mbali ya Moses Mahuna ambaye ana kesi nyingine zinazosikilizwa kwenye mahakama ya rufani.
Wakili majura aliwasilisha ombi hilo leo Februari 14,2022 mbele ya Jaji, Sedekia Kisanya toka mahakama kuu Musoma anayesikiliza rufaa hiyo namba 129/2021 kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.
Jaji Kisanya amesema kuwa Mahakama imepitia ombi la ahirisho na kumbukumbu la shauri hilo linaonyesha kuwa lilipokuja mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa Desemba15, 2021 pande zote zilielezwa imepangwa kusikilizwa leo.
"Kwa sababu hiyo waleta rufaa walipaswa kutafuta na kuomba na kuchukua nakala za vielelezo kabla ya usikilizwaji wa shauri hili ili tunapokuja leo tuweze kusikiliza," ameeleza Jaji Kisanya na kuongeza.
...Hoja ya Mahuna kuwa na mashauri mahakama ya rufani na samasi mahakama imepokea hapa zinaonyesha alikuwa amepewa 19.1.2022 na kwa sababu hiyo ni wazi alitakiwa kuijulisha mahakama ili mahakama inapopanga usikilizwaji wake iweze kujua inakuwaje,".
...Mahakama imeweza kuangalia mleta rufaa namba moja ukiachana na wakili Mahuna ana mawakili Magafu na Fauzia na hawa wote wanaweza kumwakilisha lakin pia nami nina majukumu mengine kusikiliza mashauri,".
"Tarehe zinazoombwa nina 'session' nitaendesha Dar es Salaam ombi la kuahirisha itakuwa ni vigumu na ili haki itendeke tuahirishe siku ya leo ili mawakili waweze kujipanga namba watawasilisha hoja zao na tukutane kesho saa 3 kamili na waleta rufaa wapatiwe nakala za rufaa,".
Awali wakili Magafu aliomba mahakamani hapo wapatiwe nakala ya vielele vilivyowasilishwa kwenye kesi ya msingi ili waweze kujiandaa na ushikilizwaji wa shauri hilo la rufaa.
Aidha aliomba shauri hilo lianze kudikilizwa jumatatu ijayo Februari 21, mwaka huu kwa kile alichodai kuwa wakili mwenzake wa utetezi, Moses Mahuna ana mashauri mengine kwenye mahakama ya rufani Februari 15 na 16, mwaka huu .
"Waleta rufaa tulikuwa tuna maombi, na ombi lenyewe tulikuwa tunaomba kama itaipendeza mahakama yako shauri hili liahirishwe kwa sababu mbili za msingi," aliomba wakili Magafu mahakamani hapo na kuongeza.
... Sababu ya kwanza mimi nimeunganishwa kwenye hii kesi, sikuwepo wakati kesi inasikilizwa kwenye 'trial' mbele ya mahakama ya hakimu mkazi nimepewa 'instructions' (maelekezo) za kuwa 'join' (kuungana) wenzangu juzi na kupewa rekodi na 'judgement',".
...Lakini mheshimiwa jaji baada ya kupitia 'briefly judgement' (hukumu kwa ufupi) nikagundua rufaa hii hatuwezi kuendesha kiukamilifu kama tusipokuwa 'supplied' (kupatiwa) na vielelezo ambavyo vilipolekelewa mbele ya mahakama wakati wa usikilizwaji mahakama ya hakim mkazi,".
...Tunaomba kama itakupendeza tupate vieleleIezo ili tuweze kujiandaa kwa ajili ya kuendelea na hii rufaa. Sababu ya pili ni kwamba msomi mwenzangu Mahuna anatakiwa ku 'appear' mbele ya mahakama ya rufaa kuanzia kesho na keshokutwa,".
...Atakuwa anahitajika mahakama ya rufaa na kwa hali hiyo mheshimiwa baada ya kuwasiliana na mwenzetu na kutupa hizi samansi tumeonelea ni heri tukuombe kama itakupendeza ili tuweze kuanza kusikilizwa kwa hii kesi wote tukiwa kwenye 'position' (nafasi) nzuri hasa ikizingatiwa Mosse alikuwepo kwenye 'trial! ana vitu vingi anafahamu. Kama wenzetu hawataiuwa na 'objection' (pingamizi) tunaomba tuanze jumatatu ya wiki ijayo,".
Kwa upande wake wakili wa serikali mwandamizi, Ofmed Mtenga amesema kwa upande wao walikuwa tayari kuendelea na kesi hivyo wanaiachia mahakama iamue vile itaona ni haki na sawa kwa ajili ya pande zote mbili kutoa uwakilishi wao.
Baada ya uamuzi huo wa mahakama shauri hilo linaendelea leo ambapo Sabaya na wenzake, Silvester Nyengu na Daniel Mbura walirejeshwa kwenye gereza la Kisongo.
Rufaa hiyo inatokana na kesi iliyosikilizwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi Arusha na hakimu mkazi Mwandamizi, Odira Amworo ambapo Oktoba 15, 2021 Sabaya na wenzake wawili walihukumiwa kifungo cha miaka 90 jela kwenye makosa matatu waliyokutwa na hatia ambapo mahakama iliamua adhabu hiyo iende kwa pamoja hivyo kila mmoja atatumikia kifungo cha miaka 30.
Mahakama iliwatia hatiani kwa makosa makosa matatu tofauti ya unyang'anyi wa kutumia nguvu na unyang'anyi wa kutumia silaha.
Hakimu Mkazi Mwandamizi, Amworo, alitoa adhabu hiyo Oktoba 15,2021 majira ya saa 11:47 jioni baada ya kuanza kusoma hukumu hiyo kuanzia majira ya saa 5:56 asubuhi.
“Kama alivyosema wakili wa serikali mwandamizi, Felix Kwetukia kwamba mshitakiwa wa kwanza Lengai Ole Sabaya alikuwa mkuu wa wilaya aliyeteuliwa na Rais kitendo alichofanya kinadhalilisha taasisi ya Rais,” amesema Hakimu huyo na kuongeza.
…Na hakuna ubishi kwamba wote ni vijana na wanahitajika kama walivyoeleza mawakili wao na kwa mujibu wa sheria hakuna ubishi kwamba mikono yangu imefungwa naweza kuwafunga miaka 100 lakini kurudi chini siruhusiwi kufunga chini ya 30...
…Mbali ya kwamba wakili wa serikali ameomba viboko wachapwe na walistahili wachapwe manake nao walikuwa wanawatoa wenzao wenge…
(Mahakama kicheko)
…Lakini mawakili wenzetu wameshindwa kuinyambulisha sheria ya zamani ya watoto walikuwa wanapigwa viboko lakini sheria mpya hawapigwi viboko wamepenyea hapo angalau. Basi mikono yangu imefungwa adhabu ya chini miaka 30 na viboko…
…Kosa la kwanza kila mshitakiwa miaka 30 kila mmoja kosa la pili miaka 30 kila mmoja na kosa la tatu miaka 30 kwa kila mmoja, kwa viboko mawakili wameshinda sitatoa viboko na adhabu ziende pamoja.Mna haki ya rufaa iko wazi,”.
0 Comments:
Post a Comment