SHAHIDI ameieleza mahakama kuwa, alikuta aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wakipikiwa chakula na mwanaume anayeonekana kama 'shoga'.
Aidha, shahidi huyo wa 12 upande wa Jamhuri, Sabri Abdallah Sharif ,(36) amemuomba Sabaya amalizie kumlipa deni la shilingi laki mbili alizokuwa akimdai kama gharama ya kubadili jina kwenye kadi ya gari.
Shahidi hiyo alieleza hayo leo mbele ya hakimu Mkazi, Patricia Kisinda wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha, na yesikiliza shauri la uhujumu uchumi namba 27/2021.
Akiongozwa kutoa ushahidi wake na wakili wa serikali Mkuu, Tumaini Kweka, Sharif alisema kuwa alimtambua shoga huyo aliyekuwa akipika kwa muonekano wake.
Sharif alifai kuwa baada ya kumuonyesha Sabaya kadi na nyaraka za gari alimwambia anamwita mwanasheria wake aandike mkataba wa mauziano ambapo mkataba huo ulipomalizika kuandikwa Sabaya alitoka kuelekea Mlimami City kwa ajili ya kumwekea fedha Njombee
"Sabaya aliondoka dereva wake anaitwa Antorio akaniambia anaeudi wakaniacha na watu wengine na wakamuacha mtu mmoja anapika pika pale lakini ukimuona ni shoga. Ukimtazama kwa muonenakano na mavazi yake utajua huyu shoga," alieleza Sharif akitoa ushahidi wake hali iliyoibua kicheko cha chinichini mahakamani hapo.
Alifafanua kuwa aliweza kuona jikoni kwani kwenye 'apartment' za Balckwood ndani imejengwa kwa uwazi ambapo mtu akikaa sebuleni anaone eneo la kulia chakula na jikoni.
Hata hivyo shahidi huyo aliendelea kuieleza mahakama kuwa baada ya kukamilisha kubadili jina kwenye kadi ya gari msaidizi wa Sabaya, Silvester alikuwa hapokei simu ikabidi ampigie simu dereva wa Sabaya, Antorio akamwelekeza alimpe wakala, Mussa laki mbili ili akabidhiwe kadi lakini hakutekeleza.
"Utaratibu ukakamilika april 16 kadi kutoka TRA (mamlaka ya Mapato nchini) likaja jina la Sabaya nikajaribu kumpigia Silvester akawa hapokei simu kwa hiyo kuna mtu mwingine anaitwa Antorio nikamwambia kadi iko tayari wamuone agent mussa ampe laki mbili hakufanya hivyo baada ya muda ikabidi mimi nimpe agent hiyo laki 2 kadi nikawa nayo mimi," alieleza Sharif na kuongeza.
"Tarehe 16/ 4/ 2021 nilimtumia picha ya kadi ya gari Sabaya ambayo inasoma jina lake kwenye 'whats up' akaisoma. Baada ya hapo tukakutana Dodoma kwenye mambo ya CCM kwenye kumpa uenyekiti wa Taifa CCM Samia Suluhu Hassan," alieleza shahidi huyo na kuongeza
...Nilikutana na Sabaya na Silvester nikawaambia kadi ya gari iko tayari mbona hamji kuchukua wakasema wakimaliza mambo yao watakuja kuichukua. Akaniambia Silvester atamaliza kila kitu.
...Nilipata mualiko kwenye mkutano mkuu wa CCM kama mgeni. Ndiyo hatukuonana nao tena mpaka leo ndo tunaonana nitashukuru wakinilipa deni langu,"
Upande wa Jamhuri ulikuwa unawakilishwa na Wakili wa serikali Mkuu, Tumaini Kweka, Mawakili wa serikali waandamizi, Janeth Sekule, Ofmed Mtenga , Felix Kwetukia Tarsila Gervas na Wakili wa serikali, Neema Mbwana
Mawakili wa utetezi, Edmund Ngemela na Silvester Kahunduka, Faudhia Akunay, Freedolin Gwemelo na Moses Mahuna.
Kweka: Mheshimiwa Shauri linakuja kwa ajili ya kusikikizwa upande wa jamhuri tuko tayari kuendelea tuna mashahidi wawili
Ngemela: Tuko tayari mheshimiwa
Shahidi wa 12, Sabri Abdalah Sharif, (36) mfanyabiashara mkazi wa Ilala jijini Dar es Salaaam
Wakili wa serikali mkuu, Kweka akimuongoza shahidi
Wakili: Uko ilala kuanzia lini
Shahidi; mimi mzaliwa wa ilala
Wakili; Unajishughulisha na shughuli gani
Shahidi; Nauza magari
Wakili ; Hii biashara yako ya kuuza magari ya aina gani
Shahidi; Tuna ofisi inaitwa sharija motors iko maeneo ya kinondoni kata ya Bwawani
Wakili; Unauza magari ya namna gani
Shahidi : Second hand na mapya kutoka japan
Wakili: Biashara hii mmeianza lini
Shahidi ; Tuna miaka saba
Wakili : Taratibu zenu za magari zikoje
Shahidi; Barter trade anaweza kuleta ya zamani akaongeza hela tukampa mpya au yeye anaweza kutupa mpya tukampa ya zamani
Wakili; unakumbuka nini kuhusu tarehe 1 mwezi wa sita 2021
Shahidi: Nilipigiwa simu nifike TAKUKURU Ukonga Dar es Salaam ili kujieleze
0 Comments:
Post a Comment