MWANAMKE MWINGINE AUAWA ARUSHA

 Mwanamke mwingine mkazi wa Njiro jijini Arusha, Janerose Dewasi (66) amekutwa amefariki dunia nyumbani kwake baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali ambapo  wanamsaka mfanyakazi wa ndani ambaye  alikuwa anaishi na marehemu huyo.




Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Justine Masejo amesema kuwa tukio hilo leo Jumatano Desemba 29, 2021 ikiwa ni  siku chache tokea ya mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite, Ruth Mmassy kuuawa huku jeshi la polisi likimshikilia mtoto wake kuhusiana na tukio hilo

Kamanda Masejo amesema mwili wa mwanamke huyo aliyekuwa anaishi na mfanyakazi wa ndani kwenye nyumba yake eneo la block D amekutwa amepigwa na kitu chenye ncha kali kwenye paji la uso huku akibainisha kuwa Jeshi la Polisi linamsaka mfanyakazi wa ndani ambaye anadaiwa kutoroka muda mfupi kabla ya kugundulika tukio hilo.

"Uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu alikuwa anaishi na mtumishi wa kazi za ndani ambaye alianza kazi wiki moja iliyopita" amesema RPC huyo.


Amesema kuwa mfanyakazi huyo alitoweka muda mfupi kabla ya kugundulika tukio hilo.

0 Comments:

Post a Comment