MUHUBIRI wa kimataifa, Temitope Balogun Joshua maarufu TB Joshua (58) amefariki dunia jana Jumamosi Juni 5, 2021 nchini Nigeriamuda mfupi baada ya kutoa huduma katika kanisa
Taarifa ya kifo chake imetolewa na kanisa lake la Scoan inaeleza kwamba "Jumamosi Nabii TB Joshua alizungumza katika mkutano wa washirika kupitia Emmanuel TV alisema 'kila jambo na wakati wake, kuna wakati wa kuja hapa kwa maombi na wakati wa kurudi nyumbani baada ya ibada'."
"Mungu amemuita nyumbani Nabii TB Joshua kwa mapenzi yake. Nyakati zake za mwisho hapa duniani alizitumia katika huduma ya Mungu. Hiki ndio kitu alichozaliwa kukifanya, alikiishi na kukifia," .
Hata hivyo, chanzo cha kifo chake bado hakijaelezwa ingawa kwenye taarifa hiyo waumini wamehimizwa kumwombea mhubiri huyo na kuwapa nafasi wanafamilia kuomboleza kifo cha mpendwa wao.
TB Joshua ni mwanzilishi wa kanisa la Synagogue Church of All Nations (Scoan) na kituo cha televisheni cha Emmanuel TV ambacho amekuwa akikitumia katika mahubiri yake na kuwavutia watu wa mataifa mbalimbali.
Mei 8, mwaka huu TB Joshua hakuonekana kwenye harusi ya binti yake , Serah aliyefunga ndoa na kijana wa kitanzania, Brian Moshi kwenye kanisa Katoliki la Moyo Safi wa Bikira Maria Unga Limited jambo lililoibua gumzo kubwa mitandaoni juu ya kutooenekana kwake.
TB Joshua alikuja nchini mwaka 2015 mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu ambapo kulikuwa na joto kali la kisiasa kufuatia kuwepo na madai ya kutoridhishwa na namna mchakato wa utoaji wa matokeo ya uchaguzi .
Alipofika kwa ndege yake binafsi alionyeshwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kwa nyakati tofauti akifanya mazungumzo na aliyekuwa mgombea wa CCM, hayati, John Pombe Magufuli kisha akakutana aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa pamoja na viongozi wakuu wa chama hicho kidha kuondoka nchini bila kutoa tamko lolote. mgombea wa CCM, Hayati John Magufuli.
B Joshua afariki dunia akiwa na miaka 57
Mchungaji mwenye ukarimu na huruma nchini Nigeria, mkulugenzi wa televisheni, na mfadhili, Temitope Balogun Joshua, anayejulikana kama T. B. Joshua, alikuwa kiongozi na mwanzilishi wa The Synagogue, Church of All Nations, kanisa kuu la Kikristo ambalo linaendesha kituo cha runinga cha Emmanuel TV kutoka Lagos.
“Hakika Bwana MUNGU hafanyi chochote bila kufunua mpango wake kwa watumishi wake manabii.” – Amosi 3: 7
Jumamosi 5 Juni 2021, Nabii TB Joshua alizungumza wakati wa Mkutano wa Washirika wa Emmanuel TV: “Wakati wa kila kitu – wakati wa kuja hapa kwa maombi na wakati wa kurudi nyumbani baada ya ibada.”

0 Comments:
Post a Comment