Na Gift Mongi,Moshi
MBUNGE wa Vunjo ,Dkt Charles Kimei ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais, Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi Cha shilingi milioni 500 kwa kila Jimbo ili kuiongezea uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kwa wakala wa barabara za mjini na vijijini TARURA kutokana na ufinyu wa bajeti uliokuwa unaikabili.
Serikali kupitia Ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa, (TAMISEMI) iliwasilisha taarifa rasmi bungeni kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Samia Suluhu Hassan imeamua kuongeza fedha kiasi cha shilingi bilioni 172 kutoka hazina moja kwa moja ambazo kwa mgawanyo wa kila jimbo ni wastani wa shilingi milioni 500.
Kauli hiyo iliwasilishwa na waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ummy Mwalimu ambaye aliwaeleza wabunge kuwa fedha hizo wabunge na madiwani katika halmashauri zao ndio wataamua zijenge barabara gani na kwa kiwango gani watakayopendekeza.
Dkt Kimei alisema kuwa kutolewa kwa fedha hizo kutaenda kuboresha miundombinu ya usafirishaji hususani maeneo ya Vijijini ambapo wakulima wengi wamekuwa wakipata adha ya kusafirisha mazao yao Hadi kuwafikia wateja na kuwa serikali ya awamu ya sita kama asingetaka nyongeza hiyo itoke basi isingepatikana lakini kwa sababu ya kuwathamini na kuwapenda watanzania akaona akubali kutoa fedha hizo zikaboreshe barabara zao.
"Uamuzi huu wa serikali unatokana na ukweli kuwa Mhe Rais wetu Samia Suluhu Hassan wakati anazunguka kuomba kura kwa watanzania mwaka 2015 na 2020 alijionea mwenyewe namna barabara katika maeneo mengi zilivyo na changamoto ya kutopitika hivyo kudumaza maendeleo ya wananchi ikiwemo uzalishaji na usafirishaji wa mazao ya kilimo na mifugo kuyafikia masoko kuwa changamoto pamoja na kuzifikia huduma za kijamii."alisema
Alisema uamuzi huo ni wa kihistoria, hivyo anampongeza Rais Samia kwa uamuzi huo wenye jicho mahiri la kiuchumi na hakika siku njema huonekana asubuhi na hivyo uamuzi huu unatoa ishara kuwa mambo mazuri zaidi yanakuja siku za karibuni.
" Kwa niaba yangu na wananchi wenzangu wa jimbo la Vunjo namshukuru sana Rais Samia kwa fedha hizi sisi tutaendelea kumuunga mkono na kumuombea ili tuendelee kunufaika na uongozi na utumishi wake kwa Nchi yetu."alisema
Dkt Kimei alibainisha kuwa Mhe Rais Samia anatembea katika maneno yake kuwa kazi inaendelea kupitia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 hivyo ameendelea kuwahimiza wananchi kumuunga mkono na kumuombea ili akafanye makubwa zaidi kwa nchi yetu.
Diwani wa kata ya Mwika Kaskazini Samwel Shao alisema kupatikana kwa fesha hizo kutaenda kuleta ahueni ya barabara ambazo kimsingi zimekuwa ni changamoto katika maeneo mengi.
Alisema huduma nyingi za kijamii hushindwa kuwafikia walengwa ila kwa Sasa mambo yataenda kubadilika kutokana na rais Samia kuona umuhimu wa kufanya maboresho katika sekta ya mawasiliano ya barabara na kuwa hata Kama hazitajengwa kwa wakati mmoja ila zitapunguza adha iliyokuwepo awali.

0 Comments:
Post a Comment