MIRERANI, SIMANJIRO
BILIONEA, Saniniu Laizer, amefanya maombi maalumu katika eneo la mgodi wake alipouawa mlinzi wake, Manase William, (47) ambapo walishika udongo wa eneo mwili wa mlinzi huyo ulikutwa akiwa amekufa.
Bilionea Saniniu Laizer
Maombi hayo yalifanyika oktoba 7, mwaka huu katika Mgodi wa Laizer uliopo Mererani ,Mkoani Manyara, ambapo bilionea huyo pamoja na wafanyakazi wake walilaani watu waliohusika na mauaji hayo na kumuomba Mungu awabainishe kwani mpaka sasa hawafahamiki."Nimeamua kufanya maombi haya na wafanyakazi wangu ili kama kuna waliohusika wapo hapa waweze kuumbuliwa mapema na serikali iweze kuchukua hatua mapema" alisema Laizer
Akiongoza ibada hiyo mchungaji Joshua Laizer alieleza kuwa tukio hilo ni baya na linapaswa kulaaniwa na kila mtu na kumwomba mungu awaonyeshe aliyetenda uhalifu huo wa kinyama ndani ya siku saba ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Mchungji, Joshua Laizer
"Damu ya Manase inalia hapa Ardhini tutashika udongo huu mahala damu yake ilipomwagika sisi hatumjui aliyemuua tunamwomba mungu atuonyeshe ndani ya siku saba" alisema.mchungaji Joshua.
Akinukuu maandiko matakatifu ya bibilia ,alisema kumbukumbu la torati la 27 mstari 24 na 25 na 'alaaniwe mtu yoyote ampigaye mwenzake kwa siri na alaaniwe yoyote atakayemuua mwenzake pasipo na kosa '.
Kwa upande wake Bilionea Saniniu Laizer,alisema kuwa maombi hayo yamelenga mtu yoyote aliyetenda tukio hilo baya na lakinyama la kifo cha Manase ili mungu amwonyeshe hadharani na sheria ichukue mkondo wake.
Laizer alisema ameumizwa sana na tukio hilo ambalo halikuwahi kutokea katika mgodi wake ni tukio la kwanza ndio maana ameamua kufanya maombi hayo ya kulaani tukio hilo lisijirudie tena na kama kuna mfanyakazi wake alihusika ,mungu amfichue.
" Marehemu ameajiriwa na mdhamini wa mgodi wangu na hana muda muda mrefu tangu aanze kufanyakazi na alikuwa kijana mwema hana makuu na mtu yoyote ila Mimi naamini aliyehusika si mtu wa hapa ndani atakuwa ametoka nje na eneo langu la mgodi"alisema Laizer.
Aidha Laizer ameongeza kuwa yeye anamwamini mungu na Mali anayoipata inatokana na maombi ya imani yake hivyo anaamini kwa kupitia maombi hayo mhusika wa tukio hilo atapatikana na yeye katika tukio hilo anamwachia mungu .
Marehemu Manase anadaiwa kuuawa na watu wasiojulikana septemba 27 mwaka huu katika mgodi wa laizer na mwili wake kukutwa eneo la tukio na Marehemu atazikwa siku ya Jumamosi oktoba 10 mwaka huu kijijini kwao Ilkiding'a wilayani Arumeru.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Manyara ,Paul Kasabago alisema hadi sasa jeshi hilo linawashikilia watu saba wakiwemo wafanyakazi wa Laizer wakihusishwa na tukio hilo.
0 Comments:
Post a Comment