GEKUL AFANYA ZIARA JIMBONI KWAKE


Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Mhe.Pauline Gekul leo Julai 22 amefanya ziara katika katika jimbo hilo.

Ziara hiyo ilianza asubuhi na mapema ambapo Mhe.Mbunge alitembelea vikundi vya wanawake na Vijana katika kata za Maisaka, Sigino na Bagara ambao walipata mkopo wa asilimia 10 kutoka Halmashauri ya Babati.

Baada ya kutembelea vikundi hivyo Mhe.Mbunge alihitimisha ziara yake kwa siku ya leo kwakufanya Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Imbilili Jimboni Babati.

Kijiji hicho kilikua na changamoto kubwa ya ukosefu wa Maji na Maji ilikua ni sehemu ya ahadi ya Mhe.Mbunge, kwa sasa Mkandarasi wa Maji yupo site kuwapatia wananchi wa kijiji hicho Maji.

0 Comments:

Post a Comment